Mwakaboko King
JF-Expert Member
- Apr 22, 2015
- 1,099
- 207
Tunaendelea kujifunza kwa watu waliofanikiwa na viongozi wetu waliotutangulia kuanzia kwenye vitabu vitakatifu hadi waasisi wa Taifa Letu kuwa ujenzi wa Taifa Imara sio lelemama na wala sio Kula na Kunywa bali ni kufunga mkanda na kujikana wenyewe kwa kuchagua Dira sahihi tunayotaka kuifuata. Katika hili Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ina dhamira ya dhati ya kuijenga Tanzania yenye neema. Hili halina Ubishi, Rais wetu ameamua na anasonga mbele hakuna wa kuzuia Safari ya Tanzania Mpya kama alivyowahi kusema Baba wa Taifa katika Hotuba zake kuwa Kupanga ni kuchagua, Mafanikio hayaji kwa kupiga domo ila kwa Kufanya Kazi, ni muda wa kazi kwa kwenda mbele. Kila mtu anajua hata kama vyura wanapiga kelele nyingi kiasi gani Tembo lazima anywe maji hakuna namna, Tanzania Kwanza.