Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,301
- 33,920
Baada ya kukutana na hii Posti na nyingine nyingi hapa JF, nimejiuliza ni kitu gani hasa Lissu alichowafanyia wana CCM na baadhi ya marafiki zao kufikia kumchukia kiasi hiki?
Siku ya kwanza Lissu aliposhambuliwa tuliona "huruma" za wana CCM kwa Lissu, lakini kadri tunavyoambiwa kwamba hali ya Afya ya Lissu inazidi kuimarika ndipo tunaona zile chuki na hasira za wana CCM na marafiki zao dhidi ya Lissu zinarudi kwa kasi ya ajabu.
Humu JF sasa kumesheheni mabandiko yanayoandika wazi wazi kwamba Lissu kajitakia kushambuliwa na hakuna faida yoyote ile atakayoipata zaidi ya familia yake kupata shida. Mengine yanaashiria kwamba Lissu alikuwa "kibaraka" wa wazungu hivyo kwa nini leo hawamsaidii badala yake CHADEMA wanataka serikali ndiyo ibebe gharama za kumtibia wakati Lissu alikuwa anaipinga!
Kila ukisoma mabandiko ya wana CCM hata ya yule kijana mzee W. J. Malecela al maarfu Le mutuz unapata picha kwamba kama Lissu angeuawa siku ile kuna watu wangeweka na sherehe majumbani mwao kusheherekea kifo cha Lissu.
Lakini swali la kujiuliza ni kwa nini CCM wana hasira na chuki kwa Tundu Lissu kwa kiwango hiki. Ni nini hasa alichowafanya hadi wanamchukia kiasi cha kuona mateso anayokabiliana nayo hivi sasa si kitu?
Huyu mwenye hili bandiko alikuwa anajibu hoja ya habari iliyoandikwa kwenye Mwanahalisi na Ansbert Ngurumo kwamba kati ya Lissu na Rais Magufuli nani anastahili kuombewa.Hivi kwa akili zako unaweza ukaombea mpuuzi mmoja uache Rais wa Taifa zima!!