Hivi yale makosa waliyoyapotezea waamuzi katika mechi ya Simba, ingekuwa ni Yanga wangesemaje leo?

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Najaribu kuwaza kwa sauti jinsi Simba walivyonyimwa penalty na hawakulalamika.

Na si kwa mechi ya jana tu, hata mechi za ligi ya nyumbani, Simba wamekuwa wakichezewa rafu mbaya hasa Miquisonne na Morrison tena eneo la 18 lakini waamuzi huwa wanapotezea. Kwa kweli Simba ni timu kubwa na huwa mara nyingi hawalalamiki.

Najiuliza ingekuwa hawa jamaa zetu, je wangetishia kujitoa kwenye mashindano?
 
hahaha. mkuu kama ulikuwa kwenye akili yangu. wakati yanga wanalalamikia penalty na mbeya city pamoja na prisons, simba halalamiki mbele ya al ahly bingwa wa afrka na mshindi wa 3 wa dunia
 
Wangetangaza kuwauwa marefa kwa kuwapiga kabari.
Simba kama klabu pia wanapaswa kupeleka shauri kwa tff waamuzi kuwalinda wachezaji wa Simba kwa faulo wanazofanyiwa kisha marefa wanaacha.

Marefarii wasipotoa adhabu itapelekea wacheza wanaofanya faulo kuona waposahihi.
Wachezaji watakapopata majeraha wataakaa nje,na kupelekea kushuka viwango vyao kwa kukosa kucheza kwa muda.
Kwa viwango vya wachezaji wa Simba kuna uwezekano wa kuuza awa wacheza kwenye klabu yoyote Africa na nje ya Africa.
Marefarii wawalinde wachezaji wa Simba kutokana na ngumi zinazorushwa na wakina Niyonzima.
 
Kumbe kwenye majukwaa mengine huku huwa una michango mizuri hivi!!
Kongole kwa mchango bora kabisa.
 
Simba hawa hawa au wengine!!!! Hapo tu umelalamika indirectly. Na mmekaa kimya kwasababu mmepata point 3 ila ingekuwa tofauti manara angekuwa wa blue sasahivi.
 
Back
Top Bottom