"Kila anapopita,Lowassa anaungwa mkono kwa kasi ya kutisha. Katika mikutano kadhaa,wananchi walikua wanaulizwa nani rais wap jibu linatoka Lowassa," ameeleza mjumbe mmoja wa kamati ya kampeni. Kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM anasema, "sauti hizo za Lowassa ndio rais, zimetikisa sana kambi ya kampeni. Yaan kila tunakopita,ukiwauliza nani rais wao,sauti zinasikika wakimtaja mpinzani wetu...inatisha."
Tayar wapiga kampeni wamezuiwa kuuliza swali hilo,ili kuepusha chama hicho na aibu.
Mwanakamati huyo ambayo hakutaka kutaja jina lake gazetini ametaja moja ya ya kisa hicho, kua ni kile kilichotokea, mjini Songea ambako picha za video zilisambazwa zikionesha wananchi wakijibu "rais ni Lowassa" kama ilivyotokea Katika mkutano wa Songea,Jumatatu ya wiki hii,ambao mpiga kampeni wa chama hicho Dr Emmanuel Nchimbi aliuliza, "rais ni nani," wananchi wakajibu "Lowassaaaa."
Pamoja na Nchimbi kuzima hoja hiyo kwa kujibu mwenyewe na baadhi ya watu wachache kuwa rais ni magufuli,tayar jibu Lowassa liliwazidi nguvu.
"Ukiacha majibu hayo bado tunatishika sana tunapoona umati ukiwapokea wagombea wetu hasa magufuli na mgombea mwenza, Samia, walipokea walipokelewa kwa alama za vidole viwili ikiwa ni alama zinazotumiwa na Chadema," alidokeza kada huyo. "!nabidi tujipange sana na kuwa makini na wapambe wetu,wakiendelea kutumia matusi tutashindwa uchaguzi na hatutakua na wa kumlilia,inavyo onekana wa nchi hawapendi matusi, sababu tumekuwa tukikutana na wananchi walioshika mabango yakinukuu matusi ya mkapa hii inatupa wakati mgumu sana."