Hivi wapinzani wa nchi hii wanasimamia nini au mlengo gani?

KIBEHA

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
259
128
Habari wana jamvi?
Napenda nisieleweke vibaya au nina mlengo flani bali hii hoja imenisukuma kuandika leo kwa mara ya kwanza japo ni muda wa mrefu nimekua humu.
Ni jambo la wazi tumekua na upinzani wa kisiasa kwenye nchi hii kwa muda mrefu na kazi zake zinajulikana pia ni jambo la afya kwa Taifa letu.

Huwa napata wakati mgumu sana kujua wapinzani wa CCM mfano CHADEMA, NCCR-MAGEUZI na CUF kujua wanasimamia falsafa gani au mrengo gani hasa katika nchi kama yetu ambayo watu wengi wa "mijini" wanaonekana ni "wajuaji" wa maswala ya kitaifa na kimataifa.

Mfano wapinzani wa nchi ambazo tunajifunza democrasia tayari vyama vinajipambanua kwa mitazamo yao japo kunasehemu mirengo inayoelekeana wanaweza kuungana kwa manufaa ya Taifa sitaki kuweka mifano manake inajulikana na wengi tunaujuzi huo wakuelewa ninachomaanisha.

Sasa hapa kwetu Tanzania nawauliza wapinzania wa CCM tunasimamia nini au mrengo gani,kam ni ufisadi,je tunajua dhana nzima ya ufisadi?, je ni utawala bora na tunajua dhana nzima ya utawala bora? na ni muda gani tutaacha kudandia mambo ya kwenye mitandao ya kijamii na kujikita kwenye maswala hasa yanayo hakisi upinzani kwa CCM.

Maana CCM ndiyo chama dola sasa km tunakuwa wapinzani wa "watu" na sio CCM napata wakati mgumu sana kuelewa wapinzani wa CCM wanasimamia nn,kuongoza nchi ni kuiondoa CCM na sio vinginevyo nijuavyo mimi.
Napenda tujadili kwa hoja kama kuna makosa tusahihishane kwa hoja
 
Kuna kipindi walilalamika mchanga unaibiwaa, leo unazuiwa wanalia mchanga unazuiwaa

Mlengo mkuu ni kuwa tofauti na chochote kutoka kwa serikali hata kama wao walikiunga mkono jana
Aseee ssa mnazuia wakati nchi yenu bado haina uwezo wa kuchakata huo mchanga wenyewe ssa si tunakosa vyote pesa ya kodi na vilevile mchanga unarundikana tu wakati ungeingiza pesa kwa sasa huku bado tunaanda mazingira ya kuchakata ssi wenyewe
 
Sasa hapa kwetu Tanzania nawauliza wapinzania wa CCM tunasimamia nini au mrengo gani,kam ni ufisadi,je tunajua dhana nzima ya ufisadi?, je ni utawala bora na tunajua dhana nzima ya utawala bora? na ni muda gani tutaacha kudandia mambo ya kwenye mitandao ya kijamii na kujikita kwenye maswala hasa yanayo hakisi upinzani kwa CCM.

Inasikitisha.CHADEMA enzi za slaa ilikuwa na itikadi inayoeleweka na kila mtu.Itikadi yao ilikuwa kupambana kwa nguvu zote na ufisadi na mafisadi na kuwaumbua pasipo hofu wala kutafuna maneno au midomo.Sasa hivi chukua hata horuba zote za lisu na mbowe walizohutubia hata kama hizo hotuba ni za masaa mawili huwezi kukuta hata neno moja lenye herufi FISADI wamelitamka kwenye hotuba.Hotuba zao zina kila aina ya porojo koko za maneno lakini yasiyotamka neno FISADI au ufisadi popote.

Upinzani kwa ujumla umebakia kudakia matukio tu.Raisi akikohoa wanaanza kwa nini kakohoa.Vichwa vya habari vitajaa mitandaoni na magazetini kwenye magazeti yenye mlengo wa upinzani.Rais akicheka wataanza kuuliza kwa nini kacheka inakuwa ndio vichwa vya habari vyao.

Yaani upinzani hauna agenda
 
Habari wana jamvi?
Napenda nisieleweke vibaya au nina mlengo flani bali hii hoja imenisukuma kuandika leo kwa mara ya kwanza japo ni muda wa mrefu nimekua humu.
Ni jambo la wazi tumekua na upinzani wa kisiasa kwenye nchi hii kwa muda mrefu na kazi zake zinajulikana pia ni jambo la afya kwa Taifa letu.
Huwa napata wakati mgumu sana kujua wapinzani wa CCM mfano CHADEMA, NCCR-MAGEUZI na CUF kujua wanasimamia falsafa gani au mrengo gani hasa katika nchi kama yetu ambayo watu wengi wa "mijini" wanaonekana ni "wajuaji" wa maswala ya kitaifa na kimataifa. Mfano wapinzani wa nchi ambazo tunajifunza democrasia tayari vyama vinajipambanua kwa mitazamo yao japo kunasehemu mirengo inayoelekeana wanaweza kuungana kwa manufaa ya Taifa sitaki kuweka mifano manake inajulikana na wengi tunaujuzi huo wakuelewa ninachomaanisha.

Manake CCM ndiyo chama dola sasa km tunakuwa wapinzani wa "watu" na sio CCM napata wakati mgumu sana kuelewa wapinzani wa CCM wanasimamia nn,kuongoza nchi ni kuiondoa CCM na sio vinginevyo nijuavyo mimi.
Napenda tujadili kwa hoja kama kuna makosa tusahihishane kwa hoja
mkuu kasome ilani ya uchaguzi ya chadema/ukawa au ACT hizo za 2015..... pia pitia bajeti kivuli za upinzani za kila mwaka na pia pitia hotuba za kambi rasmi juu ya wizara mbalimbali ndio utaelewa nini hasa tunakisimamia.

kichekesho mmezuia mikutano, bunge mmezima ssa wapi watanzania watajulishwa kuhusu mambo mbalimbali ya upinzani. ACT walifanya kongamano la bajeti mkawazuia... so jipe homework soma katiba soma ilani soma hizo review za bajeti n.k hapo ndio utajua hasa tunataka nni
 
Inasikitisha.CHADEMA enzi za slaa ilikuwa na itikadi inayoeleweka na kila mtu.Itikadi yao ilikuwa kupambana kwa nguvu zote na ufisadi na mafisadi na kuwaumbua pasipo hofu wala kutafuna maneno au midomo.Sasa hivi chukua hata horuba zote za lisu na mbowe walizohutubia hata kama hizo hotuba ni za masaa mawili huwezi kukuta hata neno moja lenye herufi FISADI wamelitamka kwenye hotuba.Hotuba zao zina kila aina ya porojo koko za maneno lakini yasiyotamka neno FISADI au ufisadi popote.

Upinzani kwa ujumla umebakia kudakia matukio tu.Raisi akikohoa wanaanza kwa nini kakohoa.Vichwa vya habari vitajaa mitandaoni na magazetini kwenye magazeti yenye mlengo wa upinzani.Rais akicheka wataanza kuuliza kwa nini kacheka inakuwa ndio vichwa vya habari vyao.

Yaani upinzani hauna agenda
Ufisadi??? ile hotuba ya lema alipoita lugumi ni ufisadi mlizuia ya nni?? bungeni mnyika ulisoma hotuba yake kuhusu richmond na skendo nyingine za ufisadi kuwa bunge lihakikishe maafikiano yanatekelezwa!!!! mkuu mbona mnajitoa ufaham au kisa bunge limezimwa ndio mnataka mtake advantage??

Pia kuhusu dk slaa muache unafki kipindi slaa yupo wee yehodaya ulimtukana sana humu ukimuita mwanapropaganda na ukasema yye mwenyewe fisadi kwa kuwa anajilipa ruzuku ya chama na anamlipa mkewe pia ssa najiuliza kipi kimekupata leo hii unaona slaa anamoral support ya kupinga ufisadi ilihali alipokuwepo ulimuita yye mwenyewe fisadi???? muache unafki ccm ina maana hta mbowe akihama leo mtasema ENZI ZA MBOWE CHAMA KILIKUWA TISHIO!!!

mkuu kabla hujasema hatuna itikadi je ilani ya uchaguzi ya 2015 uliisoma??? nipe hta rekodi ya kuwa ushasoma hta bajeti kivuli moja kabla hujajaj kuropoka humu
 
Inasikitisha.CHADEMA enzi za slaa ilikuwa na itikadi inayoeleweka na kila mtu.Itikadi yao ilikuwa kupambana kwa nguvu zote na ufisadi na mafisadi na kuwaumbua pasipo hofu wala kutafuna maneno au midomo.Sasa hivi chukua hata horuba zote za lisu na mbowe walizohutubia hata kama hizo hotuba ni za masaa mawili huwezi kukuta hata neno moja lenye herufi FISADI wamelitamka kwenye hotuba.Hotuba zao zina kila aina ya porojo koko za maneno lakini yasiyotamka neno FISADI au ufisadi popote.

Upinzani kwa ujumla umebakia kudakia matukio tu.Raisi akikohoa wanaanza kwa nini kakohoa.Vichwa vya habari vitajaa mitandaoni na magazetini kwenye magazeti yenye mlengo wa upinzani.Rais akicheka wataanza kuuliza kwa nini kacheka inakuwa ndio vichwa vya habari vyao.

Yaani upinzani hauna agenda
Walivyomuondoa Zitto hawana kitu.
 
Habari wana jamvi?
Napenda nisieleweke vibaya au nina mlengo flani bali hii hoja imenisukuma kuandika leo kwa mara ya kwanza japo ni muda wa mrefu nimekua humu.
Ni jambo la wazi tumekua na upinzani wa kisiasa kwenye nchi hii kwa muda mrefu na kazi zake zinajulikana pia ni jambo la afya kwa Taifa letu.
Huwa napata wakati mgumu sana kujua wapinzani wa CCM mfano CHADEMA, NCCR-MAGEUZI na CUF kujua wanasimamia falsafa gani au mrengo gani hasa katika nchi kama yetu ambayo watu wengi wa "mijini" wanaonekana ni "wajuaji" wa maswala ya kitaifa na kimataifa. Mfano wapinzani wa nchi ambazo tunajifunza democrasia tayari vyama vinajipambanua kwa mitazamo yao japo kunasehemu mirengo inayoelekeana wanaweza kuungana kwa manufaa ya Taifa sitaki kuweka mifano manake inajulikana na wengi tunaujuzi huo wakuelewa ninachomaanisha.
Sasa hapa kwetu Tanzania nawauliza wapinzania wa CCM tunasimamia nini au mrengo gani,kam ni ufisadi,je tunajua dhana nzima ya ufisadi?, je ni utawala bora na tunajua dhana nzima ya utawala bora? na ni muda gani tutaacha kudandia mambo ya kwenye mitandao ya kijamii na kujikita kwenye maswala hasa yanayo hakisi upinzani kwa CCM.
Manake CCM ndiyo chama dola sasa km tunakuwa wapinzani wa "watu" na sio CCM napata wakati mgumu sana kuelewa wapinzani wa CCM wanasimamia nn,kuongoza nchi ni kuiondoa CCM na sio vinginevyo nijuavyo mimi.
Napenda tujadili kwa hoja kama kuna makosa tusahihishane kwa hoja
Nchi hii hakuna upinzani wakweli Bali kuna wadandiaji wa kweli.
 
Aseee ssa mnazuia wakati nchi yenu bado haina uwezo wa kuchakata huo mchanga wenyewe ssa si tunakosa vyote pesa ya kodi na vilevile mchanga unarundikana tu wakati ungeingiza pesa kwa sasa huku bado tunaanda mazingira ya kuchakata ssi wenyewe
Hebu toa kwa ufupi unadhani kipi ni bora kwa kodi Na huo mchanga. Best solution kama mpinzani wa mipango ya Sasa.
Suala la wao kutokulipa kodi wamewahi kueleza kama Ukiifuatilia. Zzk alituambia kuwa huko UK wamegawana faida huku wakiwa huku wanasema wanapata hasara. Wao acacia wakajibu hiyo tuhuma cha ajabu hadi kesho hakuwahi kukili kama aliwaelewa au LA. Tatizo la malalamiko mengi ya wapinzani wetu wakielewa hawarudi kuelimisha umma walioupotosha. Mfano buzwagi wanasafirisha madini na ndege kila siku, baada ya kuelewa kuwa sio kweli hawajawahi kuwaelemisha wananchi kuwa Ile ni passenger plane na Kuna wakaguzi wa serikali taa hadi mtu wa TMAA alipofafanua juzi Kati mlolongo wote.kutofautisha usafirishaji wa madini kwa chopper na abiria kwa ndege
 
Inasikitisha.CHADEMA enzi za slaa ilikuwa na itikadi inayoeleweka na kila mtu.Itikadi yao ilikuwa kupambana kwa nguvu zote na ufisadi na mafisadi na kuwaumbua pasipo hofu wala kutafuna maneno au midomo.Sasa hivi chukua hata horuba zote za lisu na mbowe walizohutubia hata kama hizo hotuba ni za masaa mawili huwezi kukuta hata neno moja lenye herufi FISADI wamelitamka kwenye hotuba.Hotuba zao zina kila aina ya porojo koko za maneno lakini yasiyotamka neno FISADI au ufisadi popote.

Upinzani kwa ujumla umebakia kudakia matukio tu.Raisi akikohoa wanaanza kwa nini kakohoa.Vichwa vya habari vitajaa mitandaoni na magazetini kwenye magazeti yenye mlengo wa upinzani.Rais akicheka wataanza kuuliza kwa nini kacheka inakuwa ndio vichwa vya habari vyao.

Yaani upinzani hauna agenda
Enzi JK alikuwa mpole wakina Lisu walimwita rais dhaifu a.k.a Mr chekacheka,,hiv Sasa kaja JPM mkali wanasema Dikteta .Nchi hii hakuna upinzani
 
Habari wana jamvi?
Napenda nisieleweke vibaya au nina mlengo flani bali hii hoja imenisukuma kuandika leo kwa mara ya kwanza japo ni muda wa mrefu nimekua humu.
Ni jambo la wazi tumekua na upinzani wa kisiasa kwenye nchi hii kwa muda mrefu na kazi zake zinajulikana pia ni jambo la afya kwa Taifa letu.
Huwa napata wakati mgumu sana kujua wapinzani wa CCM mfano CHADEMA, NCCR-MAGEUZI na CUF kujua wanasimamia falsafa gani au mrengo gani hasa katika nchi kama yetu ambayo watu wengi wa "mijini" wanaonekana ni "wajuaji" wa maswala ya kitaifa na kimataifa. Mfano wapinzani wa nchi ambazo tunajifunza democrasia tayari vyama vinajipambanua kwa mitazamo yao japo kunasehemu mirengo inayoelekeana wanaweza kuungana kwa manufaa ya Taifa sitaki kuweka mifano manake inajulikana na wengi tunaujuzi huo wakuelewa ninachomaanisha.
Sasa hapa kwetu Tanzania nawauliza wapinzania wa CCM tunasimamia nini au mrengo gani,kam ni ufisadi,je tunajua dhana nzima ya ufisadi?, je ni utawala bora na tunajua dhana nzima ya utawala bora? na ni muda gani tutaacha kudandia mambo ya kwenye mitandao ya kijamii na kujikita kwenye maswala hasa yanayo hakisi upinzani kwa CCM.
Manake CCM ndiyo chama dola sasa km tunakuwa wapinzani wa "watu" na sio CCM napata wakati mgumu sana kuelewa wapinzani wa CCM wanasimamia nn,kuongoza nchi ni kuiondoa CCM na sio vinginevyo nijuavyo mimi.
Napenda tujadili kwa hoja kama kuna makosa tusahihishane kwa hoja

Kwanza ni kuonyeshe udhaifu wako wa kufikiri. Unaposema wanadandia mambo ya mitandao, let me be honest you have used very little brain to think. Hivi unaelewa maana ya mtandao? wewe umetumia chombo gani kutufikishia taarifa yako? wapinzani watumie chombo gani kwa hao wananchi wa vijijini uliwataja kufikisha ujumbe wa kile walinacho kisimamia kama mikutano imepigwa marufuku? ni lini ungejua kama nchi hii kuna ufisadi kama siyo hao wapinzani unao wabeza. Guys lets be serious
 
Inasikitisha.CHADEMA enzi za slaa ilikuwa na itikadi inayoeleweka na kila mtu.Itikadi yao ilikuwa kupambana kwa nguvu zote na ufisadi na mafisadi na kuwaumbua pasipo hofu wala kutafuna maneno au midomo.Sasa hivi chukua hata horuba zote za lisu na mbowe walizohutubia hata kama hizo hotuba ni za masaa mawili huwezi kukuta hata neno moja lenye herufi FISADI wamelitamka kwenye hotuba.Hotuba zao zina kila aina ya porojo koko za maneno lakini yasiyotamka neno FISADI au ufisadi popote.

Upinzani kwa ujumla umebakia kudakia matukio tu.Raisi akikohoa wanaanza kwa nini kakohoa.Vichwa vya habari vitajaa mitandaoni na magazetini kwenye magazeti yenye mlengo wa upinzani.Rais akicheka wataanza kuuliza kwa nini kacheka inakuwa ndio vichwa vya habari vyao.

Yaani upinzani hauna agenda
Nilipokuwa nikisikia kuwa Watanzania wamesoma lakini hawakuelimika mimi nilikuwa nikikataa. Kuna wakati niliambiwa kuwa ikitokea kuna kuajili wakafika Waganda, Watanzania na Wakenya, Wakenya Na Waganda watachukuliwa kwanza hata kama level yao ni moja. Mimi nikasisitiza kuwa wao ni lugha tu lakini Wtz tu vizuri.

Kama mtu aliwasikia Chadema wakilaumu Ufusadi akatoka Na kusema Ufisadi ndio itikadi ya hicho chama ujue hajui maana ya itikadi.

Mimi kutokuwa mpinzani sipo vizuri wa kuzisemea itikadi za wapinzani ila siku zote huwa najaribu kuwaona wakikinzana Na chama tawala kwa vitu lukuki vinavyopelekea jamii kukosa haki zao kama RAIA Huru wa Tanzania. Kuzuia kunyanyaswa, kuonewa, kutopata huduma za kijamii Mbali mbali, kutawaliwa kibabe, kifalme nk nk.
Ufisadi ni moja ya vitu mamia viashiria (indicators) zinazosababisha maendeleo yasimfikie mwananchi. Unapochukua pesa au mali iliyokusudiwa kuhudimia mwananchi unakuwa umefisadi. Lakini unaweza kuchukua mali iliyokusudiwa kwa wananchi ukaipeleka kwa kikundi fulani tu na wengine wakakosa kiupendeleo sio ufisadi lakini ni kikwazo kwa maendeleo ya wengi, mfano kujenga uwanja wa ndege mkubwa ambapo ndege kubwa sio muhimi sehemu hiyo maadamu ni kwa kabila lako. Unaweka taa za tarafic kwa watu wanao pita uchochoroni maafamu ni kwenu hutaitwa fisadi utaitwa vinginevyo na hilo wapinzani kulishupalia ni lao. Kujali matajiri kwa kugawa mapato ya taifa kwa yatayowafaidia wao ambapo mkulima ajisikia hapati picha atakavyo faidika na hicho, mfano kununua ndege, sio ufisadi lakini haugawi pato la taifa kwa kujali walio wengi (wakulima). Wapinzani ni monitors wa maximum collection if resources and maximum delivery of services to the people. Vipo vipingamizi Vinci humo na vinabidi vikemewe na hicho vipingamizi wasio jua huviita MATUKIO. Matukio yasipotokea hakuna tatizo, linapotokea tatizo hu brend tukio, tukio ndio Wapinzani wanakuwepo kwa taratibu zao kupigia kelele ili matukio yasiwepo au yapungue.
 
Kwa kifupi, Tanzania nzima yaani serikali na vyama vyote vya siasa vyote hatuelewi tunachosimamia.
Mfano, katiba na utendaji tofauti,

Chama tawala ( fifiemu ) ndiyo kabisa zero brains tangia 1980s

Vyama vya upinzani navyo naona ni harakati na kwenda kwa matukio kama series za kikorea.

Kwa kutolea mfano ile kauli ya Mzee wa Ruksa , Mzee Mwinyi, kuwa nchi inaenda kama.gari imekatika sukani, inatoa picha gani kwa fifiemu?
Jibu, ni kuwa hata fifiemu hawana dira, sera wala muelekeo.Yaani mambo yanaendeshwa kwa sera ya bora liende.

Hata, leo hii ukimuuliza kijana unayemuona anashupaza shingo na kupanua kinywa kwa nguvu sana kuhusu chama chake awe wa fifiemu au ukawa muulize muelekeo au mstakabali wa.chama chao hatakueleza atakuambia tu tunataka kuchukua nchi.
Wakati huohuo huyo wa ukawa atakuambia , tunajiandaa kuandamana nchi nzima, mara tunataka kuwasha moto nchi nzima.

Kwa kifupi, Tanzania tumeishapotea katika ulimwengu wa siasa na duniani.
 
Zzk naye kapiga U-TURN nyingine ya mchanga, and almost everybody in the opposition camp jumped into the bandwagon!
Hawa jamaa ni vichekesho sana, hawajitambui!
 
halafu tulivyo na akili mbovu tunawaminisha watu kuwa tutaingia ikulu, sijui kwa gia ipi na kwa mkakati upi.

nichokiona kwetu ni kuwa tumekuwa watu wa kusubiri matukio ndo tupate cha kusema. imefika hadi atua tunaiombea mabaya serikali ili tupate cha kuongea.
 
Inasikitisha.CHADEMA enzi za slaa ilikuwa na itikadi inayoeleweka na kila mtu.Itikadi yao ilikuwa kupambana kwa nguvu zote na ufisadi na mafisadi na kuwaumbua pasipo hofu wala kutafuna maneno au midomo.Sasa hivi chukua hata horuba zote za lisu na mbowe walizohutubia hata kama hizo hotuba ni za masaa mawili huwezi kukuta hata neno moja lenye herufi FISADI wamelitamka kwenye hotuba.Hotuba zao zina kila aina ya porojo koko za maneno lakini yasiyotamka neno FISADI au ufisadi popote.

Upinzani kwa ujumla umebakia kudakia matukio tu.Raisi akikohoa wanaanza kwa nini kakohoa.Vichwa vya habari vitajaa mitandaoni na magazetini kwenye magazeti yenye mlengo wa upinzani.Rais akicheka wataanza kuuliza kwa nini kacheka inakuwa ndio vichwa vya habari vyao.

Yaani upinzani hauna agenda
teh teh teh.
umamaliza mkuu mpaka nilisha amua bora tu nibaki bila chama.
 
Enzi JK alikuwa mpole wakina Lisu walimwita rais dhaifu a.k.a Mr chekacheka,,hiv Sasa kaja JPM mkali wanasema Dikteta .Nchi hii hakuna upinzani
....kufanya mambo kwa kiasi ndiyo kunahitajika..hatuhitaji kiongozi dhaifu/mzembe wala kiongozi dikteta uchwara....
 
Back
Top Bottom