Hivi wapinzani kwa sasa hoja yao kuu ni ipi?

lifuen2015

Member
May 15, 2015
93
13
Nakumbuka mchago mkubwa wa kambi ya upinzani,katika kuharakisha maendeleo ya Tanzania yetu,lakini kutokana na jitihada za wazi kwa sasa,za serikali ya awamu ya tano,ambazo hata nje ya nchi zinajibainisha wazi,swali kuu najiuliza,nini hoja kuu ya kambi ya upinzani kwa sasa,na je umakini wa serikali ya sasa na kujichanganya kwao wakati wa uchaguzi kambi ya upinzani,je ndo tuseme?kunawakwamisha kupata hoja kama ilivyo kuwa zamani?
 
Nakumbuka mchago mkubwa wa kambi ya upinzani,katika kuharakisha maendeleo ya Tanzania yetu,lakini kutokana na jitihada za wazi kwa sasa,za serikali ya awamu ya tano,ambazo hata nje ya nchi zinajibainisha wazi,swali kuu najiuliza,nini hoja kuu ya kambi ya upinzani kwa sasa,na je umakini wa serikali ya sasa na kujichanganya kwao wakati wa uchaguzi kambi ya upinzani,je ndo tuseme?kunawakwamisha kupata hoja kama ilivyo kuwa zamani?
Hoja kubwa sasa ni bokpa bomoa kwa kutumia masterplan fake
 
Du kweli wewe Div 5 mambo ya kusema yapo mengi zaidi ya IPP,tulia bunge lianze utayaona.
 
mikataba mibovu ya madini na gas
sheria mbovu
namna ya kuboresha elimu
ukosefu wa nishat
barabara mbovu
ukosefu wa ajira kwa vijana
nime taja pa kuanzia, lakini zile zama za kupayuka ovyo ovyo billa hoja ya msingi na research ya kutosha naafikiri vimefikia ukomo, tutashuhudia baadhi ya wabunge wakimaliza miaka mitano bila kuongea lolote, but all in all yakuongea ni mengi,
 
Wapinzani bado wanawajibu wa kuifanya serikali ya Dr. Magufuli eingoze kasi ya mabadiliko na yaende mbali zaidi. Watanzania wanataka mabadiliko zaidi ya haya and now.
 
Hizi kanyaboya za serikali ya awamu ya 5 ndo zimekutia upofu kiasi hiki,kha!!

Subiri bunge lianze
 
Wanaota Vyeo ambavyo waligawana kwa ahadi ya MROHO wa Madaraka waliyempa kura zao
 
Walau umekili mwenyewe kwamba hoja zao sasa kwa kiasi fulani sasa zinajibiwa. Lakini nikukumbushe tu, bado hoja zipo maelfu! Kwa leo nakupa hoja moja tu, KATIBA MPYA ILIYOTOKANA NA MAONI YA WANANCHI(KATIBA YA WARIOBA)
 
Upinzani lazima wahoji ulaghai wa serikali ya awamu ya tano wa elimu bure wakati michango ya chakula,mlinzi,mpishi,dawati na ujenzi uko palepale!
 
Inabidi kama mtamzania siku zote uukubali upinzani, si wa kubezwa, ni kwa ajili ya kusimamia serikali na matendo yake
 
Oky nimeelewa japo inabidi,wajifunze ujenzi wa hoja zaidi,si mtindo wa kuparamia na kupaza sauti,huku wakisema mafisadi,wanawajua,maana serikali ya sasa wakileta uongo ukweli wataombwa majina,sasa kama ni propaganda tu itakuwa shida kwao,umhimu wao unatakiwa ila wajipange,na pia Lowassa aliwapunguza nguvu hasa kusemea ufisadi,nawaza kwa sauti hivi watalisemea kwa sauti kweli na boriti jichoni?nawaza tu kwa sauti
 
Kwa sasa hakuna upinzani wa kweli maana wamepoteza dira baada ya kuukubali na kuukumbatia ufisadi
 
Kuzurura na kamera za waandishi Wa habari kama mawaziri Wa Pombe.
Wahariri sijui bado wana waandishi baada ya kuwabooked everyday na mawaziri wapya
 
Back
Top Bottom