Hivi wanawake mimi niliwakosea wapi

Uelekeo

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2026
Posts
213
Reaction score
299
Mama zangu shangazi zangu dada na wadogo zangu wa like nawasalimia, ima kwa wema au kwa ubaya yote poa tu

Hivi Mimi niliwakosea wapi maana yaani dah!

Iko hivi:
Asilimia 80 ya mishe zangu zinazoungua ni wanawake wananiharibia

Kuna kipindi nilipata dili fulani hivi ambapo lingetiki ningepiga maisha kiasi fulani, tukawa tumeshamaliza kila kitu na mzee mzima Ila kitendo Cha kumshirikisha mke wake tu akaweka ngumu ikawa imeisha hiyo

Nyingine nilipata eneo mahali nje kidogo ya mji Kama hekari 3 hivi eneo maini kabisa rutuba ya kutosha siku naenda kumalizana na muuzaji nimpe chake nimiliki eneo na hati ya mauziano iko tayari Mara kajitokeza sijui ni shangazi yake au mama mdogo kamwambia help mdogo Sana hiyo acha Kuna mtu atatoa Mara 2 ya hela yangu picha likaungua Ila ni roho mbaya tu hakuna Cha mtu aliyelihitaji eneo

Niliwahi kukwama kipindi fulani nikamkopa best yangu kiasi fulani Cha fedha kweli alinisaidia Ila si akaenda kumwambia wife wake? Shida ikajitokeza nilipochelewa kidogo tu kurejesha fedha mshkaji wala hakua na mom's Tena ananipa moyo "komaa mwanangu Wala usiwaze" Ila wife wake alivyokutana na wife wangu Sasa si akamropokea mbele za watu eti acheni utapeli rudisheni hela zetu halafu hata wife wangu hakua anajua Kama nimemkopa mwana

Visa ni vingi Ila acha niishie hapa

Yaani ni wanawake wachache Sana nimefanya nao biashara tukamaliza salama bila kutibuana
 
Wapo wachache sana wenye rizki mantasha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…