Hivi wanaume hampendi mwanamke mwenye mapenzi ya dhati?

The Donchop

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
294
378
Habari wanajukwaa?
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa muhanga kwa kumpenda sana mwanaume kiasi cha yeye pia kujua hilo.
Kiukweli alinipenda na kunionyesha kunijali sana. Alisimamia kila nilipokuwa na shida.
Lakini baada ya kukaa muda mrefu tukiwa kwenye mahusiano, mwenzangu amebadilika sana.
Hanipendi tena ingawa anajua wazi ninampenda kwa dhati na wala sifake upendo wangu.
Ninawaza sijui ni sababu ya kumpenda sana mpaka leo amekuja kunichukia, sielewi kabisa.
 
hataki ndoa huyo kwa hiyo anaanza kukupotezea ili akikumwaga usiumie sana
 
Wanaume tunapenda mwanamke mwenye mapenzi ya dhati ila tatizo huwa tunapata viburi sana maana tunajua hamuwezi kufanya kitu

Ila kwa suala lako
1. Huenda kuna mambo ameyaona kutoka kwako kwa sasa hajayapenda
2. Huenda kampata mwingine
3. Hakuwa na nia ya kuoana na wewe

Cha kukushauri kaa nae chini na fanya uwezalo kama mwanamke ili awe kuwa muwazi akuambie tatizo nn na muangalie jinsi ya kulitatua
 
Hebu jaribu kuangalia hali maisha yake binafsi kama biashara,kazi,hali ya kiuchumi,familia yao,masuala ya dini n.k

Mwanaume huanza kumchoka mwanamke baada ya muda kwasababu ya "distractions", nguvu na hisia zake amezielekeza kwenye mambo mengine muhimu especially hali ya sasa.

Au kuna uwezekano amekuzoea kiasi cha kukuchoka.

Yote katika yote, endelea kum-support ila usijipendekeze utaharibu kila kitu. Ni bora ukae nae mbali kuliko kujipendekeza.
 
Back
Top Bottom