GE2025 Hivi wanaelewa hata maana ya maandamano, 'Malaigwanani wakemea maandamano ya Oktoba 29'

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Its Tesha

Senior Member
Joined
Oct 6, 2025
Posts
168
Reaction score
604
Viongozi wa jamii ya Kimaasai nchini Tanzania, maarufu kama Malaigwanani, wametoa tamko rasmi la kuunga mkono kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, huku wakipinga vikali wito wa maandamano unaosambazwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Tamko hilo limetolewa katika eneo la Donyomorwak, Wilaya ya Siha, Mkoa wa Kilimanjaro, wakati wa mkutano wao wa kawaida wa Orkiama, ambapo Katibu wa Malaigwanani Tanzania, Bw. Jeremia Laizer, akisoma kwa niaba ya viongozi hao, amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuchagua viongozi wanaowataka kwa amani.
Ameongeza kuwa jamii ya Kimasai itaendelea kumuunga mkono kiongozi mwenye kuweka mbele maslahi ya wananchi na kulinda amani ya taifa, akisisitiza kuwa utulivu ni msingi wa maendeleo.

Mgeni rasmi katika mkutano huo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine, amewapongeza Malaigwanani kwa msimamo wao huo na kwa kuridhika kwao na utekelezaji wa miradi ya maendeleo chini ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha, baadhi ya viongozi wa jamii hiyo wameahidi kuwa mabalozi wa amani katika maeneo yao wakati wa kipindi cha uchaguzi, wakisisitiza kuwa maandamano yasiyofuata taratibu yamekuwa chanzo cha uvunjifu wa amani na madhara makubwa kwa wanawake, watoto na wazee.
Your browser is not able to display this video.
 
Kwani ngorongoro na loliondo share zao ziko mashakani?
 

Hawa watakuwa wamevuta MPUNGA siyo bure.
 
mwaka huu mtamleta mpaka mtume muhamadi
 
Ah ha ha ha a hawa si ndo walisema samia amelowa aha Haa πŸ˜† πŸ˜„ 😜
 
Na Hawa walio andamana ilikua ni mifugo?
 
Hawa huwa wanatumiwa sana masikini alafu wenyewe hata kujitambua hawajitambui. Wanatumika kutangaza mila za Tz wanarekodiwa wanauza sura zao na hamna wanachokipata. Na mwishowe wamehamishwa kwa bakora loliondo na bado wako wanapigishwa kabobo ...maadaui bure ya bure kabisa
 
Masai hatutaki ujinga wa maandamano kijana yeyote atakaeleta ujinga lazima achezee fimbo 70 zilizonyooka.
 
Reactions: Tui
Maelekezo Maalum kuhusu tarehe 29 Oktoba.

Siku hiyo kazi ni rahisi sana

Viongozi wa CCM tunaishi nao mitaani; Nyumba zao zipo mitaani kwetu, mali zao zipo mitaani kwetu.

Ofisi za CCM zipo mitaani kwetu. Ofisi za Umma nazo zipo mitaani kwetu

VItuo vya kupigia kura vipo mitaani kwetu

Mawaziri, Wabunge na Madiwani tunaishi nao mitaani kwetu, familia zao na ndugu zao tunaishi nao mitaani kwetu. Machawa na mali zao tunaishi nao mitaani kwetu.

Ndugu watanzania, mafuta ya taa, petroli na viberiti havijawahi kuwa adimu.

Tukafanye kazi iliyotukuka hiyo Oktoba 29 hadi hawa Mafisadi watuheshimu na wakome kutuchezea na kutuua.

Share na mwenzako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…