Hivi wabunge wa CCM wako kwa ajili ya maslahi ya wananchi au ya Chama?

H.T.P

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,169
1,298
Mara nyingi najiuliza maswali ambayo naamini humu kuna great thinkers ambao wanaweza kunisaidia.

Kazi kubwa ya wabunge ukiacha kutunga sheria ni kuishauri serikali bila kujali unatoka chama gani

Sasa kinachonishangaza kwa wabunge wa CCM kwanini yakitokea mambo ya kuikosoa au kuishauri serikali wanafumba macho na kuwaachia upinzani wahangaike wenyewe?
 
Ukiwa ccm sharti ukubali itikadi ya zidumu fikra za mwenyekiti.wengi wao wanaendeshwa kwa remote ukionekana watofauti watakuita lumumba.
 
Mkuu unajua kitu inaitwa "msimamo wa chama"...? ndo kusema wanaongozwa na taratibu..itikadi na miongozo ya chama chao!
 
Personally CCM wananikwaza sana hata kama sikuwachagua ..........

Mr President why this minister ? Yaani katika CCM wooooooooooooooooooooooooooooote umemuona huyu anatufaaa
 
inasikikitisha sana aisee na hii ni kwa Tanzania tu.sijawahi kuona nchi nyingine kwa suala kama hili la kitaifa wao wamekaa kimya tu daaah
 
CCM ni chama kilichokwisha jifilia, tatizo ni kuwa, tukiona kinapiga mateke tunadhani bado kipo hai. Wangeutumia muda huu kujisahihisha zaidi kuliko kuwabana wapinzani wao. Kila kosa wanalolichukua huwa linawaumiza zaidi
 
Hii ni kama mme wa wake wawili wote wanashindana kuonekana bora kwa mme!!!Na hata mme afanyeje hawawezi elewana hata sekunde moja bila mmoja wao kujishusha kwa kuingiliwa na sauti za busara kwenye celeberum yake.
 
Mara nyingi najiuliza maswali ambayo naamini humu kuna great thinkers ambao wanaweza kunisaidia.

Kazi kubwa ya wabunge ukiacha kutunga sheria ni kuishauri serikali bila kujali unatoka chama gani

Sasa kinachonishangaza kwa wabunge wa CCM kwanini yakitokea mambo ya kuikosoa au kuishauri serikali wanafumba macho na kuwaachia upinzani wahangaike wenyewe?
Nimewahi kuuliza huko nyuma kwamba mbunge aliyeenda Bungeni kwa kuiba kura atamtumikia na nani kati ya mtu aliyemsaidia kuiba kura na mwananchi aliyemnyima kura?Kadiri tunavyoendelea kuchekelea na kufumbia macho uchakachuaji ndivyo tunavyoongeza idadi ya wabunge na viongozi wengine wanaotumikia chama na serikali zaidi kuliko wananchi waliopaswa kuwachagua
 
Back
Top Bottom