Hivi wa kuu hii nikweli?

Kitoabu

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,786
7,356
Wakuu mwenzenu kuna jambo lime niweka njia panda kwahiyo naitaji msaada wa kitaalam zaid. Hii yaweza fika mwezi wa pili cja muingilia mkewangu tatizo likiwani kuharibika kwa mimba mimba hiyo ilikua ya miezi minne ika toka sasa nili kua nataka kufaham mambo mawili 1..... Nikitugani hua kina sababisha mimba kutoka? 2..... Nihivi ndugu zake ( bibi, shangazi, dada) wame2shauri 2c ingiliane kwamuda wa miezi sita sasa hiinikweli au ndio mila2? Naomba jamani kujua,maana akili inani2ma kugonga lakini niogopa
 

King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,801
24,510
Kwa nini msionane na gynae akawashauri baada ya kuwachunguza? Achana na stori za kitaa, watu wamesomea kazi yao miaka 7, wape uwanja wakusaidie. Kuna sababu lukuki za kuharibu mimba. Kesho watakuambia alikuwaga anatoa mimba ndo.maana zinatoka, utawasikiliza na utaumia.
 

measkron

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,782
2,397
Kwa nini msionane na gynae akawashauri baada ya kuwachunguza? Achana na stori za kitaa, watu wamesomea kazi yao miaka 7, wape uwanja wakusaidie. Kuna sababu lukuki za kuharibu mimba. Kesho watakuambia alikuwaga anatoa mimba ndo.maana zinatoka, utawasikiliza na utaumia.

kwa kweli King'asti shosti umesema yote: ngoja nimuongezee:
Kuambiwa msikutane kwa kipindi cha miezi sita baada ya momba kuharibika ni sawa kwani ni muda wa kuupa mji wa uzazi kupona na kurudia hali nzuri ya kuweza kubeba ujauzito tena.
sababu zilizofanya mimba itoke ni nyingi sana na inabidi kwenda kwa daktari kupimwa na kupata ushauri hii ikiwa ni pamoja na kuangalia kama ana uvimbe, fibroids, ugonjwa wa zinaa, shingo ya kizazi na pia huenda mkeo aliugua akiwa mjamzito na akapewa dawa hatujui, je alipata uchungu na damu kutoka ndio ujauzito ukaharibika au alienda chooni kujisaidia then alipojikamua na mimba ikatoka ikiwa ni mtoto atatoka na nyumba yake? yote haya ni maswali ambayo daktari inabidi mumueleze yoooote ndio aweze kufanya vipimo na kubaini sababu.
Kingine kuhusu kutokutana kimwili mkeo akiwa mjamzito pia inategemea ni sababu gani ilisababisha mimba ya mwanzo kuharibika, kama ana tatizo katika shingo ya kizazi na ikalazimu kushonewa hutaruhusiwa hadi atakapojifungua, kwenye mbegu za kiume kuna kitu inaitwa Prostaglandin... na hii inaweza kuanzisha uchungu wa kujifungua, hivyo kwa mtu ambaye tayari ameshapata tatizo la mimba kuharibika na sababu haipatikana huwa wanashauriwa kutojamiiana hadi atakapofikia umri fulani wa ujauzito. Pia anaweza kupewa dawa Progesterone suppliment, Duphaston ambapo mara nyingi pia imeonekana mama anayepata tatizo la kuharibika kwa mimba huenda kichocheo kinachotakiwa kuwepo kwa wingi kukuza ujauzito kimepungua na hivyo anapewa suppliment.. WAHI KWA DAKTARI KAMA ALIVYOSEMA HUYU HAPA.
 
Last edited by a moderator:

hippocratessocrates

JF-Expert Member
Jul 1, 2012
3,598
1,533
Mkuu Kitoabu, na majibu mazuri ya King'asti, measkron ningependa kuongezea kuwa;

Mimba kutoka,
Tatizo hili(kutoka/kuharibika kwa ujauzito) yaanimimba ya wiki 28..hutokana na mambo/vitu mbalimbali vikiwepo.

-Magonjwa ya Kurithi(Autoimmune diseases kama APS)
-Matatizo ya kimaumbile(hasa katika kizazi)
-Madawa (Baadhi ya dawa kutumika katika ujauzito)
-Magonjwa ya zinaa, UTI(infections)

Hayo ni baadhi ya MACHACHE yanayoweza kusababisha mimba kutoka, lakini jambo la muhimu hasa ni kujua mimba/ujauzito ulitoka/kuharibika katika umri gani wa mimba "miezi mingapi"

Mara baada ya mama/mwanamke kushika ujauzito/mimbamabadiliko mbalimbali hutokea ili kusaidia katika ukuaji wa mtoto aliye tumboni(tumbo la uzazi).Hayo huwa katika upumuaji, mfumo wa damu, mfumo wa uzazi n.k.
Hali hii hurudi katika hali yake ya awali taratibu na takribani baada ya mwaka mmoja hali ya mama aliyejifungua(Fiziolojia-yaani utendaji kazi wa mwili) huwa sawa na ya mwanamke yeyote asiye na ujauzito.Hata hivyo baadhi ya wanawake hupoteza ujauzito kabla ya kujifungua..Hii haimaanishi hali ya utendaji kazi wa mwili hurudi papo hapo, na hivyo angalau kwa miezi sita huweza kuvumilika(tolerated).
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom