Hivi viwanda mfu mkoani Tanga ni mali

mr wilehard

Member
Jun 29, 2015
49
23
Tangu nimefika mkoani Tanga zaidi ya mwaka sasa nimeshuhudia idadi kubwa ya viwanda vikiwa vimekufa na vingine magofu kabisa.

Kwa wale mnaoishi mkoani hapa ni mashahidi,vingi ni viwanda vya watu na mashirika binafsi.

Viwanda hivi kama vikifufuliwa hata robo tatu yake ni ajira ya kutosha kwa hawa vijana mkoani hapa na jirani.

Pato la taifa na kuongeza bidhaa za ndani pia ni faida sababu zilizopelekea kufa ni siasa kuzidi uchumi.

Uagizwaji wa bidhaa kutoka nje na wazawa kupenda vya nje kuliko vya ndani.
Si tu Tanga bali TZ nzima,serikali ifanye bidii kuvifufua.
 
Serikali ya mkoa kwa kushirikiana na Wizara Husika (wizara ya uwekezaji na ile ya viwanda na biashara), TIC na wadau wengine waje na sababu zilizopelekea kufa kwa hivi viwanda. Baada ya wapo waweke mkakati wa kuvihuisha viwanda hivi. Kinachosikitisha ni kuwa, miundombinu muhimu yote ipo, nikimaanisha barabara, umeme, maji, simu, n.k. Hiyo tunapata hasara kubwa sana kama taifa.
 
Kiwanda cha foma kimehamishwa DSM

Kiwanda plywood kimebaki gofu

Kiwanda cha chuma kimehamia DSM

Kiwanda cha mbolea kimekufa mazima

Kiwanda cha vitenge (Mo) kinasuasua

Kiwanda cha cement Rhino - nadhani watauza mitambo wameshindwa kukimalizia.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom