Hivi vipodozi ni hatari sana

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,171
9,386
Salam,

Jana mama watoto aliniomba nimnunulie Lotion inaitwa Coco Pulp. Nimeiona anaitumia miezi Kama 2 hivi. Kwa kuwa afya yake haipo sawa,ilibidi nitekeleze

Cha ajabu nilipofika kwenye maduka ya vipodozi wakasema hawana Kila duka. Walikuwa Wana niambia nenda duka la pili, hadi nikafika duka la nane. Nikiwa nawauliza kuna kitu nilihisi kuwa wananidanganya.

Duka la nane, nilimkuta mtu mzima mwenzangu, huyu ndio akaniambia ukweli kuwa hayo mafuta yapo ila hawawezi kukuuzia wanakuogopa kwa kuwa yamepigwa marufuku.

Sasa najiuliza hivi vipodozi vinaingiaje? Mwezi mmoja uliopita nilisoma gazetini kuwa Product za Grace Sabuni na Lotion za zoa zimepigwa marufuku. Ajabu bado zimegaa madukanina barabarani.

Hivi tatizo liko wapi?
 
TBS naTFDA hawajui kazi zao... Wao kazi kuvaa suruali za vitambaa zilizonyooshwa kwa pasi ya mkaa na kuishia kukaa ofisini tu , wakati huku field wanyonge wananyongwa na vipodozi feki.
 
Kuna tume ya kupambana na madawa ya kulevya nchini. Umewahi kujiuliza madawa ya kulevya huingia vipi nchini wakati kuna tume ya kupambana na mambo hayo?

NB: Bidhaa za zoazoa hazijapigwa marufuku popote pale.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom