Hivi UVCMM huwa mna ujasiri kweli wa kuwasifu Mwl Nyerere,Mandela,Lumumba nk..??

carnte

JF-Expert Member
Aug 8, 2017
362
425
Najiuliza hili baada ya kukuta tuhuma fulani kuwa Mhe Lazaro Nyalandu mbunge,kuleta wazo la kupeleka mswada wa katiba mpya bungeni ni chuki binafsi dhidi ya selikari na hofu yake dhahiri mara Mhe Rais atakapoanza uchunguzi kwenye wizara aliyowahi itumikia ya maliasili na utalii...ili kama akiwa mtuhumiwa kama ilivyotokea wizara nyingine basi hii liwe kama self defense kua anaonewa
Hivi UVCCM kweli kwa akili ya kawaida na Pesa za selikari zilizogharimika kiwafanya muwe na uwezo wa kujenga hoja na kupambana na mazingira ya aina mbalimbali kwa kutumia elimu mlizopata kutatua changamoto,hili la katiba sio muhimu mpaka aseme muheshimiwa Raisi?
Haya kesho akisema ni la muhimu na linakuwa kipaumbele na si viwanda tena mtakuja kupongeza?
Basi mkae kimya pale kunapokua na mgongano wa masilahi,kwanini basi kumchukia mtu mwenye nia njema kwa sababu tuu hampendi basi hata akilngea jema ni ovu
Nayaongea haya kwa ushahidi,kama mna dhamiri mtatafakari,mfano hai ni msanii Ney wa Mitego alipotoa wimbo...masaa machache mkatoa mapovu muda baada ya Mhe Raisi kuusifia mkabadilika
Mfano mwingine ni mikataba na sheria mbovu ambazo Leo zinatuweka hapa tulipo kama za madini,watu wenye nia njema wa CCM na upinzani walipopinga mlizomea...Leo hii nanyi mnalalamika
Yako mambo mengi mnatia aibu,labda mtasema kwa nini nimetoa haya ya moyoni

Nchi yoyote isiyo na Vijana wanaoweza kujenga na kutetea hoja ,lakini pia Vijana wanaokuwa na mawazo mbadala ya kujenga hasa yanayotofautiana,itabaki masikini milele,sidhani kama Mhe Raisi anafurahia kuongoza watu wanaomwambia na kumpigia makofi na nderemo kwa kila kitu,sidhani ,itakuwa ni sawa na kuongoza viumbe wengine na si binadamu,kama mnapinga haya niambieni lini mmewahi kumkosoa Mhe Raisi...Je ni kweli Raisi hawezi kukosea

La pili ni kwamba,pamoja na nyie kuwa ni UVCCM,Lakini bado tunawahitaji katika jamii kwa michango yenu chanya ambayo sio ya kisiasa moja kwa moja,nina mashaka uwezo wa kufanya haya unaweza kupungua
Leo watu ambao wanaonekana kidogo tuu kutofautiana na Mhe kama akina Bashe wanaonekana maadui...tujifunze kitu,hawa wabunge na viongozi wetu wazee wakiwamo mnaowataja kama kina Karamagi washakosea,hawawezi kufuta wameandika kwa kalamu ya wino,sisi Vijana tuna nafasi ya kurekebisha
Ujinga wa kushabikia mambo kwa mihemko ya uchama au kupata cheo Fulani unatuweka kwenye aibu kubwa kuwa,kama tungebadilishana nyakati na kuwa kipindi cha kina Mwl Julius Nyerere au Kawawa labda nchi ingekuwa bado kwenye ukoloni au tungeshaiuza nchi
Mnapata wapi ujasiri wa kuadhimisha siku za mashujaa kama kina Mandela,Mwlm Julius K Nyerere,Lumumba no
Nasikitika kwa sababu kwa mfumo wa nchi yetu wengi wenu mnakuja kuwa viongozi wetu tena kwenye mambo nyeti,sio hatari hii,au ndio baadae tuanze kuulizana tena kwanini tumefika hapa???

So sad
 
Back
Top Bottom