binti wa kirombo
JF-Expert Member
- May 17, 2016
- 847
- 959
Alikutana na wewe ukiwa kijana kabisa, ukiwa ndiyo unayaanza maisha ndani ya chumba kimoja na kitanda tu.
Unamkumbuka yule mwanamke, yeye alikua bado anaishi na wazazi wake lakini alijitahidi kujiiba, akaja kwako kukufulia na kukupikia, akitimiza majukumu yote kama vile mke wako.
Alijua huna pesa, mshahara wako mdogo lakini alikuamini, aliamini katika ndoto zako, hivyo alivumilia. Hakuomba kikubwa, hakutaka vikubwa, alikataa vikubwa kutoka kwa wakubwa kwaajili yako, alijua ipo siku mtakua pamoja.
Unamkumbuka yule mwanamke,
alikukubali ulivyo, akawakataa wale wenye hela, aliweka matumaini ya maisha yake kwako. Unamkumbuka yule
mwanamke kweli?.
Unakumbuka siku alipokufumania akakusamehe na ukamuahidi hutorudia tena. Achana na hayo maana yameshapita lakini unakumbuka namna alivyojitoa kwako, alivyojishusha. unakumbuka namna alivyoacha kwenda kufanya kazi mkoani ili tu kuwa karibu na wewe.
Hivi unajua kuwa yeye ndiyo Mama watoto wako, unakumbuka lakini mateso
aliyoyapitia kipindi cha ujauzito. Unakumbuka kweli namna ulivyoanza kuchepuka ukisema huwezi kuvumilia wiki, mbili, tatu alipojifungua na ukamsaliti.
Unakumbuka lakini kuwa yeye ndiyo alikushauri mnunue kiwanja ili mjenge, unakumbuka lakini namna alivyokua anashinda site na mafundi mpaka nyumba yenu sasa imekamilika na unataka kumfukuza.
Unakumbuka lakini wewe ndio
ulimlazimisha aache kazi ili alee watoto kwasababu tu ya wivu wako. Unakumbuka ulisahau kabisa alikua na akili ya kufanya biashara lakini ulimkataza, unamkumbuka yule mwanamke lakini wa kipindi kile?...
Unamkumbuka yule mwanamke namna alivyo vumilia mengi na wewe. Unakumbuka lakini shida alizopata wakati wa ujauzito wa mtoto wenu wa kwanza, mtoto ambaye unasema unampenda kuliko kitu chochote.
Unamkumbuka yule mwanamke, alivyogombana na ndugu zake kwaajili yako tu, unamkumbuka kweli hembu leo muangalie namna alivyochoka kwa manyanyaso yako. Si mmeshajenga, mna magari na maisha mazuri kwanini hana furaha, kwanini unamuacha ateseke. Kwanini sasa unamuona hana thamani tena kwako. Unamkumbuka lakini? unasema eti hakuvutii tena na sio wa type yako, lakini unakumbuka jinsi alivyokuwa na mvuto kipindi kile?.
Unamkumbuka yule mwanamke lakini, hembu muangalie tena na kaangalie picha zake za hawali, muangalie tu, kumbuka namna alivyokua mmbichi wakati unamuona mara ya kwanza na kumtamani, unaona alivyosinyaa sasa.
Nadhani sasa unamkumbuka, sasa hembu muangalie huyo ambaye unajifanya unampenda sasa. Unadhani angekupenda kama angekukuta miaka kumi / mitano au mitatu iliyopita?.
Kipindi ukiwa huna gari, nyumba wala kitanda, kipindi kile unakaa na kulala chini!.
Nakukumbusha tu kwamba maisha ni hatua na hakuna kitu kizuri kama kutafakari ulipotokea na kuwa karibu na wale waliokufikisha hapo ulipo. Tambua kuwa huyo mwanamke anajua njia mlizopitia mpaka kufika hapo mlipo, anaweza kukuelekeza tena na ukiwa naye kamwe hutapotea kitu. Lakini huyo unayejidi naye sasa hajui hata ulipotoka achilia mbali njia mlizopita.
Najua umemkosea sana ila leo mwambie "" Nakupenda "" na "" Samahani kwa yote niliyo kukosea "" Kuanzia hapo utaona tabasamu jipya toka kwa mwanamke wako na ile furaha iliyo toweka kipindi kile itarudi tena...
* *#JIFUNZE* *..