Hivi umanisikia lakini???............

sakapal

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
1,804
Reaction score
1,425
Habari zenu wana MMU, I salute you all!!!!

Kichwa hiki cha habari kimenifanya nikumbuke tangazo moja la mtandao wa simu za mkononi, hapa kazini kwetu imetokea kweli yaani habari yenyewe ilikuwa hivi,...........

Ilikuwa asubuhi saa mbili nanusu,
Bosi: Sasa John mimi naona tangu uajiriwe umekuwa huna muda na kazi zako kabisa, kutwa ni kushinda na laptop yako ambayo umekuwa ukija nayo na kuondoka nayo kila ikifika jioni. Kazi zako haziendi na kazi nyingine zinazotakiwa kupitiwa na wewe ili ziendelee zionakwamia kwako.
John: Mmmm............ (huku macho yote na vidole vikiwa kwenye laptop yake).
Boss: Hata wafanyakazi wengine wakikuuliza kuhusu maswala ya kazi wewe hata kuwajibu hauwajibu, mara ya kwanza tulifikiri ni bubu, lakini ukifika muda wa kutoka unaongea na watu wenye magari kuomba lifti ukiwa unarudi nyumbani. Na baadhi ya wafanyakazi wenzako wameshanilalamikia wakikupa lifti hushuki kwa sababu unakuwa umekomaa na laptop yako na kuwasababishia usumbufu wa kukushusha kinguvu kwenye magari yao.
John: Mmmmmm.........(huku macho yote na vidole vikiwa kwenye laptop yake).
Boss: Sasa basi menejiment imeamua kukuachisha kazi na tumeamua kumuajiri kijana mwingine ambaye ni rafiki yako Julius.
John: Mmmmmmm.................(huku macho yote na vidole vikiwa kwenye laptop yake).
Boss: Hivi? umenisikia lakini?
John: Mmmmmm.............(huku macho yote na vidole vikiwa kwenye laptop yake).
Hii iliwafanya watu hapa ofisini kwetu kupunguza muda wa kuingia mitandaoni muda wa kazi labda uwe likizo.

Yaani huwezi amini John aliendelea kuja kazini kwa siku tatu baada ya kufukuzwa kazi na laptop yake. Hadi pale Bosi alipohamisha meza na kiti cha John na kupaacha wazi ndipo alipogundua kuwa ameachishwa kazi. Kijana huyu kachanganyikiwa sasa ndo anakumbuka umuhimu wa kazi kwani hata hela ya kula hana, aliendelea kuja ofisini na kumuomba bosi amrudishe kazini ila imeshindikana. Mie nikajaribu kufananisha na lile tangazo la modem ya internet ambayo inaeleza mke akimwambia mumewe kuwa anaachana nae na ameamua kutoka na rafiki yake kwa kuwa mume hana muda na mke na watoto kisa modem ya internet. Sasa nimeiona kwenye kufukuzwa kazi hivi ikitokea kama hivi hadi mtu akafukuzwa kazi au kupoteza mke hii kampuni yenye modem wanamfidia? au kumlipa damage zozote? maana alikuwa mteja mzuri na mkubwa hata akapoteza mke/kazi.
 
labda tuanze na John, je atalipa fidia kwa usumbufu na muda wa muajiri alioutumia vibaya kipindi chote alichokuwa akihangaika na laptop yake? mi niko kwenye mkutano hapa kwenye hotel moja lakini ninalaptop najitia niko bize lakini kumbe nahangaika na jamii forums
 
Ni kukosa kiasi,na wapo wengi mfano wa John mtu anaingia kazini kabla ya hata ya kuanza kuangalia mambo ya ofsini yeye na face book kiasi kwamba mteja akitokea anamuona ni kikwazo anaona anampotezea muda wa kwenda kuchat.vikwazo vya nchi yetu kuendelea ni vyingi sana mojawapo ni tabia ya watu wa jinsi hii.Jaribu kufikiria umefungua kiofsi chako unaajiri mtu halafu unakuta wateja wamesimama na yeye yuko bussy na laptop kisa ana chat.
 
Hayo uliyoyanena nakuleta hapa jukwaani ni kweili tupu kwani siku hizi watu wanashindwa kufanya yale majukumu mazito ya familia, kazi zao wanashinda kwenye mtandao tu wengine wanadilriki hata kusema uongo kwa mabosi wao kwamba wameshfanya kazi walizopewa kumbe hawajafanya hiyo yote ni hii technologia mpya ya mawasiliano yaani utandawazi ulvyoingia umefanya nchi nyingi zinazoendelea kuwa duni kutokana na watu kutojishughulisha kwa kuleta maendeleo nchi kwao, nahata sasa vijana na wanafunzi wengi hawazingatii masomo yao wao ni facebook kwenye simu basi hakuna kusoma wala kufanya kazi sasa unategemea mtoto huyo atafaulu na kufika ngazi ingine ya juu, hapana ndo mana ufaulu sikuhizi umekuwa ni wa mgogoro sana. asante kwa mada yako nimeipenda sana
 
Watu dizaini hiyo
uwe nae ofisi moja halafu mna share computer ndo utapata habari yake
we una kazi zinakusubiri
yeye yupo bize anabishana siasa jf lol
 

Ati?!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…