Hivi ukweli ni upi kuhusu huyu Ngassa?

Hivi ukweli ni upi kuhusu huyu Ngassa?

mito

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2011
Posts
10,811
Reaction score
11,031
Khadija Mngwai na Joan Lema
SHAUKU ya mashabiki wa Yanga ya kumuona kiungo mshambuliaji Mrisho Ngassa akivaa tena uzi wa Jangwani huenda ikapotea baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kutamka kwamba Ngassa ni mchezaji halali wa Simba.
Ngassa alitua Yanga hivi karibuni kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Simba ambako alikuwa akicheza kwa mkopo kutoka Azam, lakini Simba ilidai ilimsainisha mkataba wa mwaka mmoja, uliopangwa kuanza kutumika msimu ujao, baada ya huu wa mkopo kuisha msimu uliopita.
TFF imesema inamtambua Ngassa kama mchezaji wa Simba kwa kuwa mkataba aliosaini na klabu hiyo upo katika ofisi za shirikisho hilo na umesajiliwa.
TFF imesema haiutambui mkataba wa Ngassa Yanga kwa kuwa klabu hiyo imemsajili kinyemela bila kuupeleka mkataba wake katika shirikisho hilo kwa ajili ya kusajiliwa kama ilivyo kawaida.
Wikiendi iliyopita, Ofisa wa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alilithibitishia Championi Jumatatu kuwa, shirikisho hilo haliutambui mkataba wa Ngassa na Yanga.
“TFF inatambua kuwa Ngassa bado ni mali ya Simba hadi sasa kwa kuwa ndiyo wenye usajili naye hapa na mkataba wa Yanga haupo.
“Ili mchezaji awe mali ya timu fulani na kutambulika TFF ni lazima mkataba wake uwe umesajiliwa na kutambulika, hivyo kwa sasa bado tunamtambua kama mchezaji wa Simba, ndiyo maana kikosi cha timu ya taifa, tumeliorodhesha jina lake miongoni mwa wachezaji waliotokea Simba,” alisema Wambura.
Championi Jumatatu lilipoutafuta uongozi wa Yanga kuzungumzia suala hilo haukutoa ushirikiano wowote. Kaimu Katibu Mkuu, Lawrence Mwalusako, alisema hawezi kuliongelea, wakati simu za Ofisa Habari, Baraka Kizuguto na Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga, mpaka tunakwenda mtamboni zilikuwa zikiita bila kupokelewa.

source:TFF yamrudisha Ngassa Simba - TEEN TZ
 
Chezea TFF ya Yanga na Yanga ya Manji wewe, lazima achezee Yanga na huyo Wambura anaweza akapoteza kibarua.
 
hivi ni kweli alisaini fomu za simba? nadhani hapa ndo utata ulipo!
 
Ngassa siyo SMART katika mambo yake; ana hulka ya kuchanganya watu kutokana na tamaa ya pesa, itafikia wakati afungiwe kucheza Soka milele na milele...kama kweli alikua amesaini Simba mkataba wa mwaka mmoja mbele ilikuaje tena akimbilie kusaini tena Yanga!!!!!.

Ni vizuri Sheria ifuate mkondo wake ili tabia hizi za kipuuzi zikomeshwe.
 
Dogo anaishia kuzunguka humu nchini na umri unaenda!
 
Mkataba wa Simba unaweza kuwa kama wa Carl Peters na Mangungo; wakati wanamsainisha ulikuwa muda muafaka wa kusaini mkataba mpya? Walimlipa kiasi gani kwa mkataba huo? Wakati wa kusaini pande zote zilifikia makubaliano? Kama yote haya yalifanyika huo mkataba ni halali, vinginevyo ni mkataba wa kilaghai.
 
nimekusoma sawia PR-N
Ngassa siyo SMART katika mambo yake; ana hulka ya kuchanganya watu kutokana na tamaa ya pesa, itafikia wakati afungiwe kucheza Soka milele na milele...kama kweli alikua amesaini Simba mkataba wa mwaka mmoja mbele ilikuaje tena akimbilie kusaini tena Yanga!!!!!.

Ni vizuri Sheria ifuate mkondo wake ili tabia hizi za kipuuzi zikomeshwe.
 
Tafuta sheria, taratibu, kanuni na miongozo ya soka ........
mkataba wa simba unaweza kuwa kama wa carl peters na mangungo; wakati wanamsainisha ulikuwa muda muafaka wa kusaini mkataba mpya? Walimlipa kiasi gani kwa mkataba huo? Wakati wa kusaini pande zote zilifikia makubaliano? Kama yote haya yalifanyika huo mkataba ni halali, vinginevyo ni mkataba wa kilaghai.
 
Dogo anaishia kuzunguka humu nchini na umri unaenda!

Huyo si dogo hivi sasa!Ni kibabu na ana watoto wanaoonekana wakubwa kuliko yeye!Uliza watu wa Mwanza watakuambia.Hata hivyo bado hajitambui!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Tafuta sheria, taratibu, kanuni na miongozo ya soka ........

Let's assume the lad has a valid contract with Simba; his declaration that he likes Yanga, Simba has no option than accepting his decision. Simba may claim for any damage so caused.
 
Huyo si dogo hivi sasa!Ni kibabu na ana watoto wanaoonekana wakubwa kuliko yeye!Uliza watu wa Mwanza watakuambia.Hata hivyo bado hajitambui!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
wivu tu.!
 
Let's assume the lad has a valid contract with Simba; his declaration that he likes Yanga, Simba has no option than accepting his decision. Simba may claim for any damage so caused.
....fine, no doubt that a contract can be discharged by breach, but also a person can be liable for the contract signed if there is a failure to comply with terms therein..... there fore Ngassa regardless declreared that he like Yanga or whatever no body coerced him to sign Simba, since he did it deliberately he deserve proportionate reward.
 
Khadija Mngwai na Joan Lema
SHAUKU ya mashabiki wa Yanga ya kumuona kiungo mshambuliaji Mrisho Ngassa akivaa tena uzi wa Jangwani huenda ikapotea baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kutamka kwamba Ngassa ni mchezaji halali wa Simba.
Ngassa alitua Yanga hivi karibuni kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Simba ambako alikuwa akicheza kwa mkopo kutoka Azam, lakini Simba ilidai ilimsainisha mkataba wa mwaka mmoja, uliopangwa kuanza kutumika msimu ujao, baada ya huu wa mkopo kuisha msimu uliopita.
TFF imesema inamtambua Ngassa kama mchezaji wa Simba kwa kuwa mkataba aliosaini na klabu hiyo upo katika ofisi za shirikisho hilo na umesajiliwa.
TFF imesema haiutambui mkataba wa Ngassa Yanga kwa kuwa klabu hiyo imemsajili kinyemela bila kuupeleka mkataba wake katika shirikisho hilo kwa ajili ya kusajiliwa kama ilivyo kawaida.
Wikiendi iliyopita, Ofisa wa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alilithibitishia Championi Jumatatu kuwa, shirikisho hilo haliutambui mkataba wa Ngassa na Yanga.
"TFF inatambua kuwa Ngassa bado ni mali ya Simba hadi sasa kwa kuwa ndiyo wenye usajili naye hapa na mkataba wa Yanga haupo.
"Ili mchezaji awe mali ya timu fulani na kutambulika TFF ni lazima mkataba wake uwe umesajiliwa na kutambulika, hivyo kwa sasa bado tunamtambua kama mchezaji wa Simba, ndiyo maana kikosi cha timu ya taifa, tumeliorodhesha jina lake miongoni mwa wachezaji waliotokea Simba," alisema Wambura.
Championi Jumatatu lilipoutafuta uongozi wa Yanga kuzungumzia suala hilo haukutoa ushirikiano wowote. Kaimu Katibu Mkuu, Lawrence Mwalusako, alisema hawezi kuliongelea, wakati simu za Ofisa Habari, Baraka Kizuguto na Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga, mpaka tunakwenda mtamboni zilikuwa zikiita bila kupokelewa.

source:TFF yamrudisha Ngassa Simba - TEEN TZ

NGASSA ana akili za ki-CCM, hana jipya!!
 
Let's assume the lad has a valid contract with Simba; his declaration that he likes Yanga, Simba has no option than accepting his decision. Simba may claim for any damage so caused.

Wakati anasign huko LION akili yake ilikuwa MAKALIONI?
 
Back
Top Bottom