Nsaji Mpoki
JF-Expert Member
- Nov 5, 2007
- 396
- 65
Majuzi tuliona spika na naibu wake wakifinyanga haki bungeni na wakatakiwa kujiuzulu. Mara yakaanza mauaji yanayohusiana na sababu za kidini tukataka waziri wa mambo ya ndani ajiuzulu.
Haukupita muda waziri wa maji naye akatakiwa kujiuzulu kwasababu haiingii akilini miaka 50 watu hata wa jiji kama la dar es salaam wakose maji safi na salama. Wakati hilo likiendelea watoto zaidi ya laki 3 wakafeli mtihani wa kidato cha nne tukataka waziri mhusika ajiuzulu.
Hivi sasa kuna mgogoro mwingine, hatari kama ule wa mizozo ya kidini ambao unachochewa na waziri mwenye dhamana ya michezo.
Huyu nae badala ya kusimamia haki amejitosa kuhakikisha kambi moja inashinda. Kwenye taarifa za habari za jana zilizorushwa na vituo vya televisheni mmeona wale vijana wanaosadikiwa kukutwa na meno ya tembo walivyouawa na wananchi wenye hasira.
Leo asubuhi kwenye kipindi cha tuongee asubuhi cha star tv mmemsikia nape akisema muundo wa wizara zetu unachangia kwa kiasi kikubwa kutokuwa na mtiririko mzuri wa kushughulikia masuala ya vijana na ajira. Huyu ni msemaji mkuu wa chama tawala.
Kama hali ni hii tumebaki na nini sasa ambacho tunaweza kujivunia? Na kwanini mhe. Rais asiamue tu kuwapumzisha kazi viongozi hawa badala ya kuendelea kuunda tume za kutafuna fedha?
Wakati umefika kwa waliopewa dhamana ya kuongoza taifa hili kuona kuwa madaraka waliyonayo yanatoka kwa wananchi na kwamba wanapaswa kuwajibika kwa makosa yaliyotokea.