rodrick alexander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 16,357
- 22,502
Hili swali nimejiuliza leo baada ya kwenda kituo cha uwekezaji TIC na kukuta shughuli zote zimesimama baada ya umeme kukatika.
Nikajiuliza kama mwekezaji anafika mara ya kwanza na kukutana na hali hiyo tena kwenye kituo cha uwekezaji anapata picha gani? Sana sana atajua hii nchi sio nzuri kiuwekezaji kwa sababu umeme ambao ni muhimu sana upatikanaji wake ni wa shida.
Nashauri kama kweli Tanzania inahitaji wawekezaji wasifikiri watawavutia kwa matangazo bali kwa kuboresha huduma zao kama upatikanaji wa umeme wa uhakika na bei nafuu, maji ya uhakika na bei nafuu, upatikanaji wa wafanyakazi wenye ujuzi, kuwepo na miundombinu mizuri na ya uhakika.
Kuondoa urasimu kama kupunguza muda wa kusajili biashara na mambo mengine yanayofanana na hayo.