Hivi TUCTA Wana Maana Gani?

Hivi TUCTA Wana Maana Gani?

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
651
Reaction score
854
Katika risala yao kwa mgeni rasmi, katibu mkuu wa TUCTA alisikika kutoa ombi kwa mgeni rasmi kuhusiana na uwiano wa wanafunzi wa kike na wale wa kiume vyuoni.

Kwamba, wanafunzi wa kiume ni karibu mara mbili ya wanafunzi wa kike. Kwa hiyo ombi likatolewa ili idadi ya wanafunzi wa kike ipande juu.

Walikuwa na maana gani hawa TUCTA kwa hili?
 
Wafute mitiani kwa Wasichana itasaidia kufika wengi vyuo vikuu , mana kinachokwamisha ni kufeli mitian japo wamepewa vipaumbele.
 
Wasifanye mtiani wa kidato cha nne na cha sita
 
Kwasasa HV vyuoni wasichana ni wengi kuliko wavulana kwenye masomo ya biashara.
Tatizo wasichana wengi inawachukua muda mrefu kumaliza sababu ya kucarry sup zao kila mwaka.
 
Tucta waliishiwa ya kuandika kwenye risala
Hawakuishiwa ila hawawezi kuyaandika yaliyo ya maana kwasababu akili zipo parking ccm. Mjue kwamba wenye vyeo katika vyama vya wafanyakazi na vyuo vya elimu ya juu ni makada wa ccm, na hawawezi nyoosha maneno.

Jana Arusha na mvua yote ile na baridi juu, watu wamevalishwa t-shirt zao zile wa watumishi wakaambiwa wasivae masweta au jacket eti t-shirt maandishi yake hayataonekana. Wanatetemeka meno yanagongana wakiwa wanaandamana. Jana lazima ngiri haikuchagua me au ke, kulaalek.....
 
Na Morogoro? Hujawaona MASHABIKI WA YANGA walivojaza uwanja na Kapelo ZAO!
 
Na Morogoro? Hujawaona MASHABIKI WA YANGA walivojaza uwanja na Kapelo ZAO!
Sikuangalia Tv Mkuu wangu. Mi naamini zile kapelo na t-shirt zinanenewa. Haiwezekani kabisa mtu akishazitinga asisikie baridi wala jua.. Yaani watu wanakuwa kama wanatembea wakiwa usingizini. Halafu wanajutaga balaa baada ya siku hiyo kwisha. Jana walijua kichele kitaongezeka, subutu......

Stress yao jana haikuwa na kipimo baada ya hutba ya Pogba. Watoto jana mchana hadi jioni lazima walikula makwenzi ya heshma baada ya wazazi kurudi kutoka Mei Dei.
 
ulitaka wamuulize kuhusu fao la kujitoa??? mtukufu saa ingine ujumbe wa mei mosi katoa yeye nyie muungeni mkono.
 
Maskini ss wafanyakazi sjui tulimkosea nn huyu baba
Na bado....lakini huwezi jua, mvumilivu hula mbivu japokuwa zinakaribia kuoza. Kitu nina uhakika nacho ni kuwa, hata kama miundombinu ambayo ni muhimu kuliko maslahi yenu itakuwa haijakamilika, mtakula shavu 2019/20 kwasababu ya yale mambo yetu....

Mtapofushwa, mkishapiga kura, anaondoa salio aliloongeza halafu mnabaki tena kulialia.
 
Zero brain, hawa hawawezi kuwafikia akina Mgaya, all are just the puppets of the surpreme
 
Nashukru Mungu jana nimejiepusha na mikauli yote ya hawa matapeli mpk sasa sijui walisema nini.
 
Back
Top Bottom