Hivi TRA wanapataje kodi sasa hivi?

ZE NDINDINDI

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
1,885
4,012
Bishara zimedoda,hali tete kila kona ya nchi hadi sekta ya usafirishaji
Kwenye mambo ya kinywaji ndo vichekesho,ma bar yanfungwa,hotel zimefulia hata vile vibanda vya mtaani vilivyokuwa vinapiga faida ya boksi la viroba 2300 sasa viko hoi

sasa kama pombe zinachangia kwa kiasi kikubwa pato la TRA na leo bar na kumbi za starehe zinapigwa vita left and right hawa jamaa wa mapato wanaingizaje hela au ndo wanategemea kile kitengo cha Traffic kubambikizia mang'ombe yenye magari faini za buku 30?

Awamu hii ishafeli, wabunge kubalini arudie uchaguzi kama alivyosema na uwe wa haki na huru tuone uhalisia wa watu wanavyomchukulia huku kitaa.
 
Kwani umesikia serekalini watu wamekosa mshahara.Just wait and see
 
Siku nikiona serikali imeshindwa kulipa wafanyakazi wake ndiyo nitajua hali ngumu lakini kwa porojo hizi bado sana tuliambiwa tangu mwaka jana kuna njaa sijui imeishia wapi
 
Hawajashindwa kulipa mishahara ...walichoshindwa ni kuajiri na kuongeza mishahara kwa waliopanda madaraja na kuna watu wanadai malimbikizo kibao...walichoweza ni kukata asilimia 15 za bodi.Bado huamini kama wamefeli
 
Back
Top Bottom