Hivi Tanzania Law Society ni kwa ajili ya Taifa au Magufuli?

H.T.P

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,169
1,298
Ujue huyu bwana asipokumbushwa kwamba, alipiga push-ups kuomba kura na kukariri salam za makabila karibia yote ili kuwaaminisha kwamba ni mwenzao, atatufikisha pabaya sana.

Kauli zake za kimungu zinaligawa taifa kabisa na itatengeneza uadui mkubwa sana katika taifa hili, kwanza ameanza kutengeneza ukabila ambao nyerere aliupigania kwa miaka mingi ufe, angalia teuzi zake, hadi mkuu Wa majeshi anatoka kwake, ila hajui analigawa jeshi vipandevipande, kuna siku atabaki yeye na mkuu Wa majeshi.

Ukimuangalia usoni amedhamiria kabisa kuhakikisha anauua upinzani, hapendi kukosolewa, hapendi kuonywa, hapendi kupewa mtazamo tofauti na wakwake!

Anawapa viburi watu wake wakaribu, Magufuli usipoangalia, utadhibitiwa na Mungu muumba kwasababu sisi wanyonge, hatukuwezi kwasasa. Muangalie Makonda anavyodhalilisha watu tena kwa jeuri na makusudi!

Leo Magufuli anasema MTU anayetoka upinzani Never sipitishi jina lake!! We ninani Magufuli? iangalie Pua yako inatazama wapi? Usimkufuru Mungu kwa kuchukua cheo chake.

Nakuonya na nakukumbusha, m ni kiumbe Mdogo sana kwako ila, aonywaye Mara nyingi akishupaza shingo itavunjika; amesema Mungu.
 
Eti anatamani malaika washuke mbinguni waje wazime mitandao ya kijamii, mara ooh natamani kuwa IGP niwanyooshe wanaosindikiza Ndugu zao, mkuu wa nchi anatamani wananchi wake wapigwe na polisi, huyu kuna kitu hakipo sawa
 
Natumaini mkulu alijichanganya tu kwa hiyo kauli. ktk dhama hizi za vyama vingi ili mipango na malengo yako yafikiwe lzm ushirikiane na upinzani. Hebu fikiria siku wabunge wengi wakitoka upande usio wako, mambo yako utayaoitishaje?. Ni vyema mh. akaanza sasa kuwapa nafasi wapinzani hasa kwenye nafasi za kura badala ya kujiapiza haiwezekani ilihari 2020 hatujui nini kitatokea.
 
Tanzania Law Society?????

Imeanzishwa lini hiyo maana niliona hata sizonje anatamka hivyo tena kwa kurudua rudia!
 
Natumaini mkulu alijichanganya tu kwa hiyo kauli. ktk dhama hizi za vyama vingi ili mipango na malengo yako yafikiwe lzm ushirikiane na upinzani. Hebu fikiria siku wabunge wengi wakitoka upande usio wako, mambo yako utayaoitishaje?. Ni vyema mh. akaanza sasa kuwapa nafasi wapinzani hasa kwenye nafasi za kura badala ya kujiapiza haiwezekani ilihari 2020 hatujui nini kitatokea.
2020 kitakacho tokea kiajulikana, nacho ni ccm kutangazwa washindi tena kwa kura nyingi zaidi kwani dola imeshikwa kisawa sawa na ushindi wao upo huko kwenye dola na siyo wingi wa kura.
 
Huyu hasikii hata akisikia hazingatii hata akizingatia anakurupuka na akikurupuka anakosea akikosorewa ndio huaga chanzo cha vita.
 
2020 kitakacho tokea kiajulikana, nacho ni ccm kutangazwa washindi tena kwa kura nyingi zaidi kwani dola imeshikwa kisawa sawa na ushindi wao upo huko kwenye dola na siyo wingi wa kura.
mku umesema kweli na hivi watanzania walivyolala usinginzi mzito basi 2020 ni CCM tu
 
Back
Top Bottom