Hivi Tanzania kuna ma-engineer au mafundi repair?

Hivi Tanzania kuna ma-engineer au mafundi repair?

kukumdogo

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2011
Posts
2,894
Reaction score
2,806
Kwakweli nimekuwa nikijiuliza sana hili swali kama sisi watanzania tunao engineers, hii ni kwasababu hakuna hata kitu kimoja wanachotengeneza au ambacho wamegundua.

Ukiwauliza wanakuambia mitambo ya kutengenezea vitu au hata spare hakuna! Hivi kwanini wasiitengeneze hiyo mitambo au ndio wanafundishwa kufunga bolt na nuts tu?

Kwakweli tunaomba tuonee mchango wa maengineers katika kutatua suala la umaskini katika nchi. Hata kuunda baiskeli wasomi wetu wa vyuo hawajui.

Cha ajabu zaidi ikitoka technolojia mpya kama simu au nini yani wao ndio wakwanza kushangaa. Hivi kukopi na kupesti vilevile hamuwezi? Mnaojiita maengineer kwanzia leo tutawaita mafundi repair maana hamna uwezo wa kuunda zaidi ya kurepair.
 
Wanaweza wakakutengenzea chochote unachotaka kwenye karatasi. Hapo ndio mwisho wa elimu ya Tanzania. Makaratasi huyaweka kwenye makabati yakijaa huyachoma moto ikisha wanakimbilia kwenye siasa.

Wasomi wetu wengi saivi wanaokolewa na google
 
Wanaweza wakakutengenzea chochote unachotaka kwenye karatasi. Hapo ndio mwisho wa elimu ya Tanzania. Makaratasi huyaweka kwenye makabati yakijaa huyachoma moto ikisha wanakimbilia kwenye siasa.

Wasomi wetu wengi saivi wanaokolewa na google
Majengo ni makaratasi.., usiwe Kama mbwa!
 
Nafikiri ungeenda katika vyuo kuangalia kumbukumbu za project zinazofanywa na wanafunzi wa mwaka wa mwisho kila mwaka kisha utapata jibu na pengine mada yako itabadilika kwa nini serikali au mfumo wa elimu hauendelezi project zilizofanywa na wanafunzi wahandisi ili kuendeleza taifa?naweza kukupa mfano mmoja,kuna jamaa mmoja alikuja na project rahisi yakuzalisha umeme kisha usambazwe katika wilaya yake,ila serikali ilimjibu hilo haliwezekan na hata alipoenda SIDO hakupata ushirikiano,sasa utasemaje kuwa wahandisi wote wako kama unavyosema japokuwa nakubaliana na wewe kuwa kuna vyuo vinatoa wahandisi katika fikra zakiutawala zaidi na siyo vitendo na pia kuna wahandisi wana mawazo yakuwa katika level ya utawala tu wakishamaliza chuo(hapo ni tatizo la mfumo au binafs) na pia kuna wanaoshindwa kuleta kile walichojifunza shulen kwenye uhalisia(haya ni matatizo yakukariri sana)...kwa hiyo ndio kusema usiliweke hili jambo kwa ujumla wake huo bila kujiuliza vyakutosha.
 
jinsi hoja yako ilivyo unaongelea mechanical engineers. kwa kuelewesha wana jf ungetoa mfano wa nchi za afrika ambazo mainjinia wao wameunda kitu ili angalau waumie kuwa kwanini wao hawawezi. ungeenda mbali zaidi kwa kuuliza engineers wa bongo walioko nje wana mchango gani huko. tuendelee kuchangia. tusitukanane kwa kuwa tunatofautiana uelewa
 
jinsi hoja yako ilivyo unaongelea mechanical engineers. kwa kuelewesha wana jf ungetoa mfano wa nchi za afrika ambazo mainjinia wao wameunda kitu ili angalau waumie kuwa kwanini wao hawawezi. ungeenda mbali zaidi kwa kuuliza engineers wa bongo walioko nje wana mchango gani huko. tuendelee kuchangia. tusitukanane kwa kuwa tunatofautiana uelewa

Nataka kuona baiskeli imechorwa MADE IN TANZANIA
 
... hakuna hata kitu kimoja wanachotengeneza au ambacho wamegundua.
Huenda umekaa nyumbani kwako ukitegemea utaletewa vitu vinavyoundwa. Jaribu kutembelea vyuo vinavyofundisha Uhandisi, hasa wakati wa maonyesho ya DITF maarufu kama maonyesho ya Sabasaba. Usiwe unabeza eti kwa sababu wewe hujaona au kusikia, jitahidi utafute habari na maarifa, usisubiri kuletewa! Binafsi ni mhandisi, na ninakuhakikishia tembelea karakana za DIT na kama ukitaka UDSM, tembelea workshop ya Technology Development and Transfer Centre (TDTC) ya CoET, utakuta vitu unavyodhani havifanyiki!
 
Kweli ubongo wako ni mdogo kama user name yako,Tanzania kuna ma Engineer wengi tu na very potential ila watu waluosoma course ya sound kama yako tender wanawapa watu wa nje.
 
Ninataka kuleta changes niwe miongoni mwa watu watakaozalisha products ambazo ni Made in Tanzania it always begin with you especialy when you something you love problems becomes challenges na nina imani nitafika tu niwe na kiwanda changu ambacho kila kitu kitakuwa made in TZ. Chuma ambachi ni Malighafi kubwa kwa viwanda kinakuwa planned to be exported na wako wanajenga railway hadi Bandarini but tutapambana tu. Mungu nisaidie niwe vile ninavyoota daima niache kuwa mtumwa nijitume.
 
kuandika made in tanzania ni rahisi kwa kuwa hiyo inafanywa na wachora maandishi ambao sio engineers. hakuna injinia ambaye anahitimu bila kutoa mchango wake ni nini atafanya kutumia elimu yake. vyuo vinavyotoa mainjinia hayo yapo na ni mengi kwa idadi ya wahitimu. tatizo ni mfumo wetu elimu na matumizi ya rasilimali. ni kiasi gani cha fedha kinatengwa kwenye elimu ukilinganisha na kinachotumika kimyakimya kwa masuala binafsi ya wakubwa? hata hayo maandishi ya made in tanzania yanahitaji pesa. je utatoa ya kwako mfukoni (kwanza huna uwezo kwa kuwa milo yako ya siku haitimii)kulipia? Sioni kama kuna mantiki kuwalaumu engineers. hata hivyo tunaona wanavyotoa michango yao sekta nyingine japo wewe unapendelea bolt na baiskeli na maandishi yake. kuna majengo. barabara. umeme nk. kutumia Google ni sawa kwa kuwa is there kwa ajili hiyo na ndo matumizi yake. labda tungepata ni kipi kipya cha maendeleo ambacho wanasiasa wametengrneza. ungechukuwa hizo billions za bmk ukawapa engineers ungeona wonders hapa hapa bongo badala ya hongkong. kama kwenye siasa ndo unaona fedha yote inapelekwa na huku kwako kukavu unasubiri ufe kwa njaa ndo uingie siasa?
 
tatizo ni mfumo mbovu wa elimu tz hata ukienda na project yako inapigwa na chini
 
Pole kwa uelewa wako mdogo. Tatizo ni miundombinu ya hapa kwetu. Ukitaka kuunda kitu hapa gharama za uzalishaji zitafanya hiyo kitu isipate soko. Bei inaweza fika mara kumi ya kugiza kitu namna ile ile toka nchi zilizoendelea. Miundimbinu yao inarahisisha uzalishaji. Umeme rahisi, usafirishaji rahisi, matumizi ya robots kwenye uzalishaji, uwepo wa mitambo ya kuzalisha vipuri n.k. Kwa taarifa tanzanian engineers walioko nje wanafanya vizuri sana. Mfano Selekwa and Warioba walioko USA. Hata kuna fani nyingi kwenye engineering. Mbona civil engineers wameunda majengo kibao huoni? Electrical engineers wanakaribia kukamilisha network ya umeme nchi nzima. Nyumbu waliwahi kuunda gari lakini gharama za hiyo project siyo rafiki kuwa endelevu. I hope that opens up your litle thinking.
 
Back
Top Bottom