Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,684
- 149,887
Kama mnadhani hakuna haja ya Bunge kujadili mwenendo wa Spika na Naibu wake,
basi tujue tu tunajidanganya na si ajabu hata kabla Bunge hili la Bajeti halijafika mwisho,wabunge wengine hasa wa upinzani wanaweza tena kuingia matatizoni.
Ni wazi pia kanuni za Bunge zinazokipa kiti madaraka makubwa ya kuweza hata kuzima hoja muhimu za wabunge zisipopitiwa upya,lugha za kuudhi Bungeni haziwezi kwisha kwame.
Kinachofanyika Bungeni ni kujadili na kutafutia ufumbuzi matatizo yanayojitokeza lakini sio kujadili na kutafutia suluhu kiini au chanzo matatizo haya.
Na hapa nasema mapema kabisa kuwa sitashangaa kina fulani wakachokozwa makusudi ili tu kuwatia hasira alafu baadae waje waadhibiwe.
Spika,Naibu Spika na wenyeviti wa Bunge mkitenda haki mna nafasi kubwa sana ya kuepusha yote haya vinginevyo kila wakati mtakuwa na kazi ya kuhukumu watu.
Unapoona unaongoza vikao vya mara kwa mara vinavyokutana kwa lengo la kuadhibu wabunge,basi inabidi wewe mwenyewe pia ujitathimini kama kweli unatosha kwenye hiyo nafasi.