Hivi Simba watauenzi kweli mchango wa Mafisango? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Simba watauenzi kweli mchango wa Mafisango?

Discussion in 'Sports' started by Anselm, May 25, 2012.

 1. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kuna mtu aliwahi kutoa pendekezo humu kuwa Simba ianzishe mashindano maalumu kwaajili ya kuuenzi mchango wa Mafisango lakini naona tumeutia kapuni mazima.
  Jamani ni ukweli usiopingika kuwa jina la Patrick Mutesa Mafisango huwezi kulitenganisha na mafanikio ya Simba kwa msimu huu wa 2011/2012 tukianzia na yale ya Kagame (kufika final),kutwa bingwa wa Ligi ya Vodacom na kufikia hatua ya 16 bora kwenye mashindano wa Kombe la Shirikisho Africa,sote ni mashahidi wa zile jitihada zake binafsi zilizokuwa mara kwa mara zikibadili matokeo ya Simba yaliyokuwa yanaelekea kuwa hasi na kuwa chanya ghafla.
  Binafsi pamoja na kuwa na itikadi ya mlengo wa opposite na Simba lakini nilikuwa namkubali sana Marehemu, lakini najiuliza je kuitoa katika mpango wa kutumika jezi No. 30 iliyokuwa inavaliwa ndo kitu pekee walichoweza kufanya kwa aliyekuwa mchezaji wao mahiri ambao wenyewe walimbatiza jina la "jembe"?
  Iliniwia vigumu kuamini kuwa Simba ilishindwa kutoa siyo tu rambirambi bali hata Mwakilishi anayeeleweka kutoka katika ngazi ya juu ya uongozi kuambatana na mwili wa Marehemu katika safari yake ya mwisho humu Duniani,najiuliza hivi kama Viongozi kadhaa wa juu to mention few Nyange na Rage pasipo ulazima wowote waliweza kuambatana na Mafisango alipokuwa hai na team kwenda Shandy kiasi cha kushindwa kuwa accomodated na kulazimika kulala kwenye makochi reception walishindwa nini kwenda na mwili wa Marehemu mpaka Kinkola?,au ndo zile za kujuana wakati wa raha tu wakati wa shida atajijua mwenyewe na familia yake.....haya na suala la rambirambi nalo.....ni aibu kwa Club kama Simba ambayo dhahiri inaonyesha ndo team iliyoongoza kwa mapato katika mchezo wa Soka hapa Tanzania kushindwa kupeleka hata senti 5 kwa familia ya Marehemu kama rambirambi,na je ziko wapi zile rambirambi zilizotolewa na wadau mbalimbali tokea ulipotangazwa msiba ule mpaka pale TCC tulipokuwa tunamuaga "Jembe"? kwanini hata zile basi hazikuwakilishwa kwa familia ya Marehemu? haya si ndo yaleyale ya kina Mtitu,JB,Ray na wengineo wa Kamati ya msiba wa Kanumba na rambirambi zake.
  Kwanini lakini sisi binadamu tunakuwa hatuna uoga na Mwenyezi MUNGU kabisa?
  Haya hata wiki 2 hazijaisha tayari viongozi,wanachama na mashabiki wa Simba wameshasahau msiba wa "Jembe" lao na sasa wako kwenye maandalizi kabambe ya kuangusha bonge la sherehe la kusherehekea mafanikio yaliyochangiwa na Marehemu,hivi kweli kwa mwenendo huu nikisema vilio vyao vya siku ile pale TCC vilikuwa ni vya kinafiki kuna mtu anaweza kunibishia?

  Nawasilisha.
   
 2. M

  Masuke JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Hata wasipouenzi viongozi, najua mashabiki hasa tuliokuwa tukihudhuria uwanjani tutakumbuka mchango wake daima alipokuwa akipeperusha bendera ya Simba, kuhusu rambirambi lazima familia yake wataipatia fedha iliyopatikana hata mapato yatakayotokana na mechi ambayo inatarajiwa kuchezwa kati ya APR na Simba lazima atapata, mchango wake hakika ulikuwa ni mkubwa sana maana nakumbuka mechi nyingi ambazo Simba ilishinda goli moja mfungaji ni yeye au ametoa pasi ya mwisho.
   
 3. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kwanza nafurahi sana kuona kuna wana'simba wanaokumbuka mchango wa Marehemu Pat' katika mafanikio ya Simba lkn kukumbukia mchango wake tu ilhali familia yake inateketea kwasababu iliyokuwa nguzo yake imeondoka inakuwa haisaidii kitu kwanza it's very unfair,nikimnukuu Mgosi anayecheza DC Motema Pembe ya kule Congo familia ya Mshikaji kule ni dhorfulhali,inaonekana kila kitu ilikuwa ni yeye na kwakupeleka mwili kule bila support yeyote ilikuwa ni sawa na kuongezea jeraha kwenye jeraha.
  Habari za kusema kuwa rambirambi watapewa, lini? ,raha ya rambirambi ni pale wafiwa wanapokuwa bado kwenye majonzi mazito mnawapiga na kifuta machozi kiasi kwamba wakati wanapoendelea na tanga masuala ya chakula kwa waombelezaji inakuwa siyo issue tena,sasa nyie mnasema sijui vitu gani....hizi habari zenu bwana pelekeni Dar-Live kesho,sisi waelewa tunajua kuwa hiyo ndo imetoka lkn amin-amin nawaambia kama Viongozi wa Simba hawataliangalia hili kwa umakini Marehemu kule atasononeka sana na atawalaani na mtapoteza mafanikio yote miliyoyavuna msimu huu,TAKE MY WORDS!
   
 4. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  View attachment 54665
  Mdau wa Simba akimmwagia mahela (takribani 100,000/= Patrick Mafisango enzi za uhai wake baada ya goli lake la juhudi binafsi kuipatia Simba point 3 muhimu katika mojawapo ya michezo ya Ligi iliyomalizika.
  Katika kipindi kifupi sana tokea kifo chake viongozi wa Simba wanaonekana kumsahau kabisa,inasikitisha sana.
   

  Attached Files:

 5. N

  Ngarna JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,975
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  Anselm wewe ni mnafiki hakuna asiyekujua.Msiba wa Mafisango hauna hata wiki
  mbili umeanza uchuro.Mambo ya Simba waachie Simba.Mipango yote mazishi na rambirambi
  imesimamiwa na Mzee Kinesi na kesho pesa zilizotengwa zitakabidhiwa wa familia ya marehemu.So
  piss wacha crocodile tears.Shughulika na migogoro yenu.
   
 6. N

  Ngarna JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,975
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  Piss off wacha uchuro.
   
 7. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye red....nashangaa Simba wamesahau kabisa kuwa walipatwa na Msiba,wako busy kuandaa Part Dar
  Live,kuna mambo ya Simba ya kuwaachia Simba wenyewe lkn mengine kamwe hatu/sita kaa kimya,mimi najua tatizo letu tunaweka mapenzi mbele sana kiasi kwamba hata kama Viongozi wetu wanaharibu sisi huona wanatengeneza tu wewe rambirambi zimekusanywa kuanzia siku inatoka habari za msiba mpaka pale TCC tulipokuwa tunamuaga kwanini hazikupelekwa na Mwili,walibaki nazo kwa madhumuni gani kama siyo ya kuzifanyia editing? hivi ngoja nikuulize Ngarna umeshawahi kufiwa ghafla na uliyekuwa unamtegemea kwa namna yeyote ile?,kwa jinsi Mafisango alivyokuwa ndo kila kitu katika familia yake umeshafikiria kuji'position kwenye nafasi ya familia yake kwa kipindi hiki? embe tafakari kwanza siyo unatapika tu.
   
 8. M

  Masuke JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Mkuu mimi nafikiri tungeongea kuhusu mechi ya kumchangia kati ya Simba na APR kama itakuwepo lakini tukianza kuhoji kuhusu rambirambi labda mimi sielewi maana ya rambirambi na hela inayopatikana kutokana na rambirambi sijui inafanya kazi gani, mimi ninachoelewa hela ya rambirambi ni kuhudumia wakati wa msiba kama vinywaji kama maji, chakula, usafiri, maturubai, viti na gharama zingine kulingana na mahitaji na kiasi kinachobaki ndo hukabidhiwa familia ya marehemu. Kwa msiba wa Mafisango sijui ni kiasi gani kilikusanywa na kiasi gani kilibaki sasa mkuu unapokomalia familia isaidiwe kutokana na michango ya rambirambi hiyo familia itasaidiwa hadi lini maana si kila mara michango ya rambirambi itakuwa inafanyika kwa hiyo si busara kuwaulaumu Simba kwa nguvu namna hiyo, ni kweli kama hela ilibaki inabidi ipelekwe na kama kuna hela ambayo Simba walikuwa wakidaiwa na marehemu inabidi walipe pia lakini kuwalaumu eti familia yake inateseka na yeye ndo alikuwa tegemeo sio haki, watu wangapi wanakufa makazini na ofisi ikishatoa mchango wa rambirambi ndo imetoka nani anaenda kusaidia hiyo familia, nadhan tunakiwa kujua kuijengea misingi familia yako wakati wa uhai wako ni jambo la maana na sio kutarajia rambirambi itasiadia familia.

  Mafisango alikuwa mchezaji tegemeo wa Simba hadi anapata umauti hilo halina ubishi na mimi kwa mechi zote ambazo nimeshuhudia alikuwa ni msaada mkubwa sana kwa timu, ubingwa huu una mchango mkubwa wa Mafisango na kama hiyo mechi itakuwepo mimi mwenyewe niko tayari kulipia hata watu wengine kama watano ili mradi hela iwe nyingi hilo ndo la msingi lakini kuhusu hela za rambirambi labda tungejua kiasi gani kilikusanywa na kiasi gani kilibaki na Simba wana mpango gani nacho hapo ndo tutaweza kulaumu otherwise lawama zako si sawa kwa sasa.
   
 9. N

  Ngarna JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,975
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  Unafiki ni ugonjwa mbaya sana.Anselm Yanga mlisaidiaje Jela Mtagwa na Allan Shomari ambao wanateseka hadi
  leo licha.ya kuchezea na kusaidia sana Yanga.Au uwanachama umeanza mwaka huu.
   
 10. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Lichaya kwamba tuliwasaidia sana hasa Allan Shomari alipokuwa na matatizo yake yamacho(kama hukuwa na habari) lkn mifano yako hailingani kabisa,hawa Jamaawalicheza mpira mpaka wakastaafu,kwa kutumia mpira walifanikiwa kutimizamalengo yao mengi tu,mtoto wa kwanza wa Allan Shomari anaweza kuwa age-matewangu kwahiyo obvious anatakiwa awe anamsaiidia Baba yake kipindi hiki lknMarehemu "Jembe" ameacha vitoto vidogo,

  Familia-Mafisango.jpg
  Embu angalia jinsi familia yake ilivyopoteza matumaini,hapa walikuwa wanamzika Marehemu,kama huyo Dogo wa kulia aliyefanana na Marehemu sana anaonekana anatamani angekwenda naye tu

  Fikiria Ngarna ungeondokewa na uliyekuwa unamtegemea at5-10 years of age leo hii usingekuwa hata unatoa maoni humu JF,sawa sisemiSimba ndo wachukue jukumu la kulea familia ya Marehemu 1 kwa 1 lkn hatawangeonyesha kuwa wapo pamoja nao basi hasa katika kipindi hiki ambapo msibabado mbichi,hivi kweli kabisa habari za Simba na Mafisango zimeishia pale TCCsiku ile tunaaga,eti baada ya kuona watu tunaongea sana jana ndo wameibuka nakusema rambirambi zipo,shillingi ngapi....siri yao,hata kwa familia yake pia nisiri? na kwanini lakini zisiwakilishwe mapema,zinasubiri nini?
   
 11. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,640
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Tatizo la wachezaji wa ukanda huu ni kuendekeza starehe na kusahau ndugu zao na nyumbani kwao. Naomba mnisamehe sana kwa kusema haya!
   
 12. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #12
  May 28, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  wewe ni mnafiki sana tena ni mtu wa kuogopwa sana sana sana??
  Au ndio nyani halioni kund***??

  Nimesoma coment zako zote mpaka thread uliyo ianzisha vimekaa kinafiki sana?
  Yaani wewe ni zaidi ya mshirikina??

  Wewe siyo kiongozi wa simba? Siyo mwanachama wa simba? Na hata siyo mpenzi wa simba?
  So mipango ya simba juu ya marehemu unaijua?? Acha unafiki kijana ndiyo mana litimu lenu migogoro haiishi kamwe??
  Vip? Kwani wewe ni yanga asili au yanga masalia??

  Swala la kusherehekea ubingwa ndani ya dar live ni mipango iloyokuwepo hata kabla hawajaenda kucheza mech sudan.
  Tuliza nyoro kikana.
   
 13. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mesage kalikali za namna hii ni dalili kuwa lile nililolikusudia (la kufikisha ujumbe kwa Wahusika wa Simba) limeanza kutimia,mnamsahau vipi jembe katika kipindi kifupi cha wiki 2 tu? na rambirambi zipelekwe kwa ndugu zake,acheni wizi...hata hamuogopi kula pesa za Marehemu,mtalaanika ohooo!
   
 14. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  ni kipi unachokiona kikali kwako hapo katika hiyo post hapo juu.

  Ok!! Wanasimba wamesha msahau mafisango. Inawezekana wewe una majibu na malengo mazuri na nin? Kifanyike juu ya mafisango??

  Inawezekana mawazo na malengo yako yakawa msaada mkubwa kwa wana simba.

  Kama siyo mnafiki na mzandiki na kama una nia njema na mafisango hebu funguka ni nin?? Kifanyike au ulipenda wana simba na uongozi kwa ujumla nin wakifanye??

  Nasubili hekima na busara zako mkuu
   
 15. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #15
  May 28, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,991
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Msipende kukuza mambo jamani.
   
 16. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ewaa hapa sasa umenifurahisha,mimi napenda tubishane kwa hoja siyo maneno makali'makali ooh mnafiki mara mshirikina haisaidii kitu,mimi nilitegemea wana'simba wenyewe ndo mngekuwa mstari wa mbele kukemea uovu wa viongozi wetu,mimi binafsi huwa si'support ujinga hata kama unafanywa na Viongozi wa Club niipendayo.

  Sasa bwana kwenye issue ya Mafisango jinsi Simba walivyou'treat msiba wake mimi sijapendezewa kabisa,nikikumbuka mchango wa Mshikaji katika mafanikio ya Simba ya msimu huu naona kwa kila hali hawajamtendea haki Marehemu kule alipokwenda na hata familia yake aliyoiacha hapa Duniani,yafuatayo ni baadhi ya mambo hayo:-
  1. Kwa mtazamo wangu naona Simba hawakufanya vizuri kutotoa uwakilishi mzito kusafiri na mwili wa Marehemu,nimejaribu kujiuliza ni sababu gani iliyowafanya washindwe kutoa hata mwakilishi mmoja kutoka kwenye ngazi ya juu ya uongozi kipindi hiki ambapo team haipo kwenye mashindano yeyote sijapata jibu.
  Huku ni kuonyesha kutojali tofauti na Rwanda (Marehemu alipokuwa anachezea team ya Taifa),chama cha soka cha kule kilitoa uwakilishi wa maana sana kuonyesha walivyouthamini mchaango wake kwa team ya Taifa.
  2. Rambirambi: Mashuhuda kule Kinkola wameshuhudia Mzee Kinesi na Mwakilishi wa wachezaji Boban wakikabidhi mwili wa marehemu kwa familia yake barehanded(mikono mitupu) na baada ya hali ya sintofahamu kujitokeza pale ilibidi Mzee wa watu ajipigepige angalau atoe chochote alichokuwa nacho kutoka katika mfuko wake binafsi,rambirambi zilikusanywa kuanzia pale msiba ulipotangazwa mpaka siku tunaaga pale TCC,zimekwenda wapi? kwanini zisingepelekwa na mwili kuwapunguzia machungu wafiwa?
  3. Mgosi(mchezaji wa zamani wa Simba) ameshaleta taarifa juu ya uhitaji wa msaada kutoka katika familia yake soma hapa Shaffih Dauda in Sports.: FAMILIA YA MAFISANGO YAOMBA MSAADA SIMBA NA AZAM
  Kukaa kimya kwa uongozi wa Simba kwenye hii issue na kwenyewe kuonaonyesha kutoitendea haki familia yake,Mafisango alikuwa ni Mwajiriwa wa Simba kwahiyo lazima atakuwa ameacha stahili zake, kipindi hiki wakati msiba ukiwa bado wa motomoto ilikuwa ndo kipindi cha kupeleka stahili zote zilizokuwa zinamhusu Jembe.
  4. Suala la kuandaa Part katika kipindi hiki (kifupi baada ya msiba) pia mimi sikuona ulazima wake,hali hii ilisababisha hata kuwakosa baadhi ya wachezaji ambao hawakuona sababu ya kusherehekea ilhali bado wana machungu ya msiba na wengine ambao walikuwa team ya Taifa.
  Isitoshe sherehe ile ilivuruga hata program ya mazoezi ya team ya Taifa kwani kina Kaseja walikuwa tayari wana mawazo ya namna watakavyokuwa wanakatisha mitaa ya Dsm kama Man City walivyokuwa wakikataza mitaa ya jiji la Manchester.

  Sasa nini kilipaswa kufanyika:-
  1. Watu wazima Rage na Kaburu au hata mmojawao walipaswa kuusindikiza mwili mpaka Kinkola,kuonyesha ushiriki wa team kikamilifu...wangeshindwa kabisa basi hata yule kiongozi wa kamati ya ufundi ya team Maestro ambaye ndo alikuwa karibu na wachezaji angekwenda,ingeleta uzito fulani.
  2. Wengi wetu tumeshawahi ku'experience issue za misiba,unapopata msiba kuna gharama(zinazohusiana na msiba direct) huwa zinaanza mara moja, kwa kuwapelekea rambirambi zote zilizokuwa zimekusanywa mpaka wakati ule ingesaidia kupunguza mzigo wa msiba ule kwa wafiwa.
  3. Stahili zake zifuatiliwe na kuwakilishwa kwa wafiwa,kama kuna pesa yeyote Marehemu alikuwa anaidai Simba ni wakati wa kuilipa familia yake pamoja na PPF/NSSF zake,MUNGU awasaidie wawe na uoga wa kudhurumu haki ya Marehemu ambayo familia yake inaweza kunufaika nayo.
  4. Katika kufanyia kazi ombi la familia uongozi wa Simba unaweza kuandaa mechi ya kimataifa ya kirafiki kati yake na team nyingine 1 ambayo Marehemu aliwahi kuchezea mathalani APR au TP Mazembe na mapato yatakayopatikana kwenye hiyo mechi yakawakilishwa kwa wafiwa,fikiria zikipatikana 50M zikawakilishwa kwa familia yule mtoto wake wa mwisho si atakuwa na uhakika wa kusoma mpaka mbelembele huko.
  5. Busara kidogo ingetumika hii part ya Dar-Live ingesogezwa mbele na kupisha siku hizi ambapo bado watu wanamkumbuka Jembe,pia ingesaidia kutovuruga program za Kim katika kipindi hiki ambapo tunajiandaa na mechi ngumu dhidi ya Ivory Coast,habari nilizozipata ni kuwa imebidi kocha aahirishe program ya mazoezi ya leo ksbb idadi kubwa ya wachezaji wa simba wamekesha na pombe jana kwenye Part.

  Naomba niishie hapa,kama unanijibu nijibu kwa hoja siyo matusi tafadhali...kila mtu anajua matusi
   
 17. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #17
  May 28, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 849
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Mkuu umekosoa na kushauri vizuri sana! Mimi niko upande wako pia (Mtani wao), sikupendezwa kabisa na jinsi watani wetu walivyolichukulia suala hili la msiba wa "Jembe".
  Nilimshuhudia Rage pale TCC akilia; Kaseja akilia na kujinasibu kuwa alikuwa rafiki yake wakaribu; Pawasa runingani Clouds) akiongea kwa huzuni na hisia kali, kuwa yeye ndiye aliyemleta Tanzania (Simba) na wengineo wengi!
  Kilichonishtua sana ni kumteua Boban kuwakilisha!
  Swali: Ina maana watani wetu, yale yalikuwa machozi ya samaki??
  Matusi hayana tija, kama una hoja ya kujitetea fanya hivyo, vinginevyo kubali yaishe!
   
 18. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #18
  Jun 12, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mimi bado na Watani tu,
  Familia ya Mwendazake "Jembe" Paty Mafisango(R.I.P) wameibuka tena na kudai mpaka muda huu hawajapokea hata buku kutoka kwenye uongozi wa team aliyokuwa anachezea Mpendwa wao Simba Sports Club,kwa mujibu wa Mdogo wa Marehemu aliyekuwa anaishi naye hapa Dar Orly Elemba amesema licha ya kuona rambirambi zilivyokuwa zinamiminika wakati wa msiba wa Kaka yake anashangazwa na ushirikiano haba anaopewa kutoka kwa viongozi wa team hiyo ambapo sasa imefikia stage hata akiwapigia simu hawapokei.
  Habari nyingine zinasema Simba wametumia hela hizo kwa matumizi mengine na sasa hivi wanahaha kutafuta pesa nyingine za kuipoza familia ya Mwendazake.

  Chanzo: Gazeti la Mwanaspoti la leo; Simba wauchuna na fedha za Mafisango
   
 19. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,491
  Trophy Points: 280
  viongozi wa simba na hata wachezaji wenzake hawakufanya kitu cha maana kitendo cha kusheherekea ubingwa wakati ni wiki mbili tu mwenzenu ameaga dunia si cha kiungwana na mpaka sasa hivi wameshindwa kupeleka rambirambi inatia aibu na inawavunja moyo wachezaji wengine wataona kumbe wanathaminiwa pale tu wanapoipa klabu mafanikio Rage aache porojo zake siku ile kumbe yale machozi yalikuwa ya kinafiki lakini hata kocha James Siang'a alipougua simba hawakutoa msaadawowote
   
Loading...