Hivi Sare za shule na viatu, hairuhusiwi kuchangishwaa??

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
15,002
2,000
Katika kile ambacho kinaelezwa na serikali kuwa elimu ni bure kwa shule za msingi na sekondari bado kumekuwa na suntofahamu ya wazazi na walimu.

Wazazi wengi ambao wanafurahia tamko hilibla serikali, lakini bado kuna ukakasi.
Serikali imesema haitaki kusikia habari ya michango yoyote mashuleni, sio ada, dawati, mlinzi, mpishi, chakula, jembe, fagio, na vingine vingi.

Wakuu wa shule wengi kwa sasa wanaandaa join instruction kwa wanafunzi wa sekondari, lakini bado wanashindwa kuluweka suala la sare za shule kama sehemu ya mchango.
Kuna baadhi yao wanasema serikali itagharamia mpaka nguo za shule za wanafunzi.

Hivyo tunaomba serikali iweke wazi ni michango gani itagharamia na ambayo haitogharamiwa na serikali.

Nawasilisha.
 

KXY

JF-Expert Member
Dec 31, 2011
877
250
Serikali ilishatoa tamko, sare shule inatakiwa ieleze kitambaa gani kinatakiwa ili wazazi wanunue wenyewe. Shule haziruhusiwi kuchangisha na Serikali haitatoe hela za sare za shule au za michezo wala vifaa vya usafi.
 

Mshinga

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,536
2,000
hii ndio nini?

hakuna mchango wa sare na haukuwahi kuwepo popote.

hizo zilikuwa biashara za kuwalazimisha wanafunzi kununua sare za shule katika miradi ya walimu kwa bei kubwa na misare ya ovyoovyo.

sare ni lazima kila mwanafunzi kuwa nayo ila sasa washone wenyewe makwao.
 

MAFILILI

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
2,373
2,000
Vipi kuhusu tabia ya kuwatuma watoto wa shule za msingi kwenda shule na vidumu vya maji na fagio??? Navyo ni marufuku??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom