Hivi Rais Mama Samia atawaruhusu wapinzani kuanza kupiga danadana na kupanda na kushuka katikati ya uwanja?

Katika hali isiyotarajiwa na wenge Mama ameanza vizuri sana kuanzia aliposhika kijiti kuingia uwanjani, kwanza akaipaisha jinsia ya kike kuwa inaliweza kulisakata gozi.

Na ndani ya masaa machache akaachia shuti baya sana upande wa TPA na likamng'oa mtu na hapo hapo akajigeuza na kuangalia winga ya kushoto TAMISEMI nako ni hatari sana.

Nauliza kiuharisia kuwa kama Mzee baba akuwapa hata pumzi ya kubetua tu je Mama atawaruhuusu wapinzani hili nao waanze kupasha misuri, hasa ukizingatia kuwa misuri yao imepoa sana kwa kukaa benchi kwa muda mrefu.
Kama sio mpigaji awazue ya nini sasa.Aliyesema atauwa upinzani kaondoka kauacha upinzani
 
Usitegemee Jambo Kama Hilo mkuu.iko hivi,kikazi mama Samia ni rais wa JMT maana yake anawatumikia watu wote ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania,lakini kiutawala anatawala kwa misingi ya ilani ya ccm,desturi za ccm na miiko ya ccm.hawezi kuweka misingi ya utawala nje na ilani ya chama,nje ya Mila na miiko ya chama.Na Kama ikitokea kufanya nje ya hapo,maana yake ameamua kuvunja ilani ya chama,desturi za chama na miiko ya chama.je itawezekana afanye hivyo! yaani aikane na kuipa kisogo nyumba iliyomlea na kumhifadhi hata Sasa alipo!?
 
Haki za kidemokrasia hutolewa kwa mujibu wa katiba na sheria zilizopo na wala siyo na Mama.Watanzania wenye fikra finyu kama wewe ni janga kwa maendeleo ya Taifa hili!
 
Back
Top Bottom