Hivi PSSSF bado haijalipa?

Hivi PSSSF bado haijalipa?

anti-war

Member
Joined
Mar 9, 2018
Posts
47
Reaction score
34
ZA asubuhi wadau, naomba kuliza swali nililoulizwa "hivi hadi tarehe ya jana 6/8/18 bado PSSSF hawajawalipa warithi na wastaafu pesa kama ilivyokuwa awali?
 
umeulizwa na nani? nenda psssf kwa majibu ya uhakika
 
Ukistaafu awamu hii ya tano, utakufa kwa msongo wa mawazo. Mifuko ya hifadhi ya jamii iko hoi.
 
ZA asubuhi wadau, naomba kuliza swali nililoulizwa "hivi hadi tarehe ya jana 6/8/18 bado PSSSF hawajawalipa warithi na wastaafu pesa kama ilivyokuwa awali?
Unauliza pesa gani mkuu,pension ya kila mwezi au ya mkupuo?Maana ya kila mwezi wameshalipa,tena tarehe zile zile kama kawaida.Ila nahisi amalgamation bado haijakamilika,bado wamelipa kama PSPF,PPF nk.
 
pension ya kila mwezi, mumewe alikuwa mwalimu
 
Mkuu kwani mme wake alikufa lini na tarehe yake ya kujihakiki ni lini?The point here is,anayelipwa pension ya kila mwezi ni mstaafu mwenyewe sio mwenza.Mwenyewe akishakufa, payment inaishia kwenye tarehe ya kujihakiki,tena kwa vile hawawezi ku-establish kwamba mwenyewe ameshakufa.

Hata hivyo kama mnataka kujua hasa kilichotokea,ingieni kwenye tovuti ya shirika ambalo huyo mama mme wake alikuwepo,kamà ni NSSF ingia kwenye tovuti yao,naamini wanayo,mtapata namba ya kupiga bure, wapigieni mtapata jibu.Naamini kwamba PSSSF hawako fully operational kwa sasa, maana hata tovuti hawana.
 
Haupo sawa, LAPF walikuwa wakilipa wajane wenye watoto chini ya 18 yrs malipo ya mwezi.
 
Inaumiza sana chief!! Kuna mzee alistaafu mwaka jana, hajalipwa mafao yake hadi leo. Anadaiwa kodi ya pango na hana hela ya kulipa. Ni maumivu.
Mkuu mm mwenyewe nina mzazi wangu toka mwaka jana hadi leo hii haijajulikana fedha zake anapata lini, lakini kwa viongozi kisiasa unashangaa huu ucheleweshwaji haupo kbs!
 
Haupo sawa, LAPF walikuwa wakilipa wajane wenye watoto chini ya 18 yrs malipo ya mwezi.
Siwezi kubisha kama una uhakika LAPF wanafanya hivyo mkuu,labda ni kweli.Unajua, mazoea ni mabaya,si unajua tumezoea kwamba mpaka mtu anastaafu hana watoto wadogo,na nadhani hata mashirika hayo yanaamini hivyo.Hata hivyo nadhani itabidi huyo mama approve kwamba ana watoto wadogo wa mnufaika.
 
Mkuu mm mwenyewe nina mzazi wangu toka mwaka jana hadi leo hii haijajulikana fedha zake anapata lini, lakini kwa viongozi kisiasa unashangaa huu ucheleweshwaji haupo kbs!
Wanalipana wenyewe, na inasemekana ucheleweshaji huu unatokana mifuko kukosa fedha za kulipa, kwani fedha zote serikali imekopa na haijalipa, na haijulikani inalipa lini. Mifuko inaidai serikali fedha nyingi sana. Wastaafu wanateseka sana.
 
Mkuu kwani mme wake alikufa lini na tarehe yake ya kujihakiki ni lini?The point here is,anayelipwa pension ya kila mwezi ni mstaafu mwenyewe sio mwenza.Mwenyewe akishakufa, payment inaishia kwenye tarehe ya kujihakiki,tena kwa vile hawawezi ku-establish kwamba mwenyewe ameshakufa.

Hata hivyo kama mnataka kujua hasa kilichotokea,ingieni kwenye tovuti ya shirika ambalo huyo mama mme wake alikuwepo,kamà ni NSSF ingia kwenye tovuti yao,naamini wanayo,mtapata namba ya kupiga bure, wapigieni mtapata jibu.Naamini kwamba PSSSF hawako fully operational kwa sasa, maana hata tovuti hawana.
asante ntalifanyia kazi
 
Yan kwakweli Mungu atusaidie sana. Hii nchi imefika mahala inaumiza sana mioyo ukiifikiria, mtu unafanya kazi kwa tabu halafu unastaafu tena unateseka na visent vyako halafu tunajisifu kuwa tunajali wanyonge kweli? Hebu Raisi wa wanyonge aliangalie hili kwa jicho la pembeni, Yan kuna rafiki yangu kajifungua kafatilia fao la uzazi wanamwambia bado kanuni mpya hazijatoka sasa km walikuwa hawajajipanga na kuandaa makanuni mapema kwann waliunganisha mifuko haraka, Kuna siri gani iliyojificha? Ee Mungu tutie nguvu sana sana
 
Back
Top Bottom