Mwaka 2016 kuna mzee mmoja aliekua boss wangu mwaka 2015 ila akafukizwa kazi kwa wizi Magufuli alipoongia ikulu. Mzee akanialika kikao na semina za one coin pale Golden Jubilee Tower ili nijiunge.
Mzee alitumia kila mbinu kunikamata nikamkatalia, Golden Jubilee nilienda siku 2 baadae nikaacha kwenda maana niliona napoteza tu muda wangu.
One coin iliwaliza watu wengi sana. Kuna jamaa yangu mmoja nilimuomya kua hii ni ponzi/pyramid scheme akanikatalia, baadae alikuja kukubaliana na mimi baada ya kua hela zake zimeliwa.