Hivi nini kifanyike Haya makanisa na Misikiti kila kona yawe kichocheo cha Maendeleo?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,735
Yaani nimegundua watu wanawaamini viongozi wa dini kuliko wanasiasa.
Wakiagizwa kitu kwa mgongo wa Imani wanakifanya kwa moyo wote kuliko kwa mgongo wa kisiasa.

Nadhani hawa watu pia wananafasi ya kufanya Ili kuwe na Mlipuko wa Maendeleo na Mabadiliko Chanya.

Kama Mtu mmoja anaweza kuwahadaa waumini wakusanyike Kwenda Iraq Bila Tiketi nao wakatii.
Kama mtu mmoja anaweza kuwaamrisha waumini wakeshe barabarani wakizuia Umeme Usipite
Kama mtu mmoja anaweza kuwaamrisha wanakwaya Kuimba mapambio kituo cha polisi badala ya kufanya shughuli zao.
Kama mtu mmoja anaweza kuwaaminishia Watu na kuwachomea ndani ya nyumba,
Kama mtu mmoja anaweza kuwakusanya vijana wa kike na wa kiume wenye nguvu Kukesha porini
Kama mtu mmoja anaweza kuwafanya wanadamu kujizuia kula siku 40 bila kulalamika.

Basi kwa misingi hiyohiyo kumbe hawa watu wanaweza kuhamasishwa kufanya vitu vikubwa katika nchi yao kama vikundi.

cc
5191291_fbimg14927961721360229_jpeg99787360e3ee299fa09e7421efc43cdf
 
Inabidi viongozi wa Makanisa na Misikiti wakazanie kutoa eimu ya Uraia kwa wapigakura kwamba wasichague watu kwa vigezo vya Kapero,Ubwabwa,Pombe,T-Shirts na Rushwa.Vilevile wasisitize kuzilinda kura zao ili zisiibwa.wawe wakakamavu kwa gharama yoyote ile.Hapo ndio watasaidia kupata viongozi bora ambao watatuongoza kwenye maendeleo.
 
Kuna baadhi ya mambo mazuri ya kitaifa yasiyo na uhusiano wowote kisiasa wala wa kidini lakini yanauchanya ndani yake kwa maana ya maendeleo yanatakiwa yawe ni lazima kuhamasishwa makanisani na misikitini kwa watu wa makundi yote...

Hiyo ni fursa kubwa, Misikiti na makanisa inashamiri kila kona ya nchi.
wananchi wakihamasika kwenye maendeleo hata SADAKA hazitakuwa shida...
 
Siasa ndio kila kitu.
Pasipopatikana viongozi wazuri wa kisiasa hakuna maendeleo yoyote yatakayopatikana.Viongozi wa kisiasa ndio wanapanga uchumi uendeshejwe.Lazima wananchi wajue watu sahihi wa kuwaongoza na wawe tayari kuwachagua na kuhakikisha watatangazwa washindi.

Viongozi wa dini wakihamasisha wananchi walitambue hili watakuwa wameisaidia sana Tanzania kuondokana na maadui watatu wa taifa yaani umaskini,Ujinga na Maradhi.
 
Kuna baadhi ya mambo mazuri ya kitaifa yasiyo na uhusiano wowote kisiasa wala wa kidini lakini yanauchanya ndani yake kwa maana ya maendeleo yanatakiwa yawe ni lazima kuhamasishwa makanisani na misikitini kwa watu wa makundi yote...

Hiyo ni fursa kubwa, Misikiti na makanisa inashamiri kila kona ya nchi.
wananchi wakihamasika kwenye maendeleo hata SADAKA hazitakuwa shida...
Toa mfano wa mambo matatu tu ambayo hao viongozi wa dini wanaweza kuwahamasisha waumini wafanye kwa maendeleo ya nchi zao.
 
Back
Top Bottom