Hivi nikifanikiwa kugusa mbingu nitakuta ni ya aina gani

wa stendi , hili ndio jibu sahihi kwa swali lako.
Dunia tunayoishi, tupo juu yake na sio ndani. Anga unaloona limetuzunguka likiwa na nyota, mwezi na jua, ni pana halina mwanzo wala mwisho. Hizo nyota unazoona angani, kiuhalisia sio ndogo kama unavyoziona, nyingine ni sayari kubwa kama hii dunia tunayoishi.

Kama alivyosema shalet, hiyo rangi ya bluu unayoona ni mwisho wa uwezo wa macho yako kuona. Inakuwa bluu kutokana na mchanganyiko wa hewa zinazoizunguka dunia.
Asante kwa mwongozo mkuu
 
Two ways to answer your question:

Biblically, mana mimi ni mkristo ukisoma katika Mwanzo (Genesis) 1:7-9
Kwamba Mungu katika uumbaji alitenganisha maji, ya juu akayaita Anga, na Anga akaliita Mbingu. Then ya maji ya chini akayaamuru yakusanyike pamoja then akayaita bahari etc, ili nchi kavu ionekane... SO, KUKUJIBU kwa upande huu mimi nitakwambia hiyo mbingu unayotaka wewe kuigusa ni maji ambayo Mungu aliyatenga. Sijajua Quran imeandikaje mana bado sijaisoma. Aliesoma atatusaidia.


But pia nikikujibu kwa upande wa Science, mimi ni fan wa kufuatilia sana mambo ya night sky, so napenda kujifunza...wanascience wao wanasema the sky (anga) sio Blue kama wewe unavoliona. We see it blue because of the distance ya naked eyes, plus remember there several layers/spheres hapo juu before kufika kule (stratosphere, homosphere etc, ziko spheres 3 kama sijakosea mpaka uvuke dunia uende kwenye ile open space kule juu) na hizi zinakazi zake, ambazo pia zinatufanya kwa njia moja au nyingine sisi hatuwezi ona kule juu kama kulivo with our naked eyes.

Kule juu ni dark tu, its not blue, wala red wala chochote, ni dark as dark..mimi nitakupa two ways to prove that, ambazo mimi binafsi nimefanya, simple, you wait on the total mid night, around 2pm, kaa kitandani angalia juu katika usawa wa dirisha lako. Why? mana muda huo kumbuka jua haliko kabisa close, liko upande mwingine na lile giza la chumbani kwako litasaidia kukublock na lights za nje, then utaona uhalisia..ama ukiona hii doesnt work, u-time mwezi (moon) around saa kumi au kumi na moja ambao bado ni mwanga kabisa au hata saa nane mchana (anytime mida ambayo jua halijazama) then chukua camera ambayo inauwezo wa kusnap moon katika umbali ule (mana sio camera inaweza), zoom the moon then you'll see how dark is kule juu, sio blue but dark.

Hizo njia 2 mimi nimeshafanya, ya usiku naifanya everyday..
Nimekupata mkuu lakini kwa maelezo yako hapa kwayo mbingu tuionayo huko juu ni maji
 
Hakuna juu wala chini. Simply because dunia inazunguka jua na kujizungusha katika muhimili wake kutafuta mchana na usiku. So sababu ya kujizungusha there are times juu ni chini na chini ni juu. So hakuna juu wala chini...ukitaka kuelewa hili, uwe unafatilia position za nyoto katika vipingi tofauti katika masaa hata miezi. . Utagundua kuna nyota ambazo ukiziona January to July etc, huzioni tena mpaka tena next year katika miezi fulani ndo unaziona tena. .. Au position ya visible planets (venus, mars, jupiter, ) when do they arise and when do they disappear, na locations zao time to time zinapokua visible..ukifatilia utajua mzunguko wa dunia, kama now tuko kwenye kona, now tuko straight and so forth.

Kuelewa hivi vitahitaji uwe mfuatiliaji pia kwa vitendo.
Sayansi naweza amini amini kuna chembechembe za uongo kidoogo,,,
 
Unazifahamu poles 2 za dunia? Ingekuwa dunia inaenda juu then chini as its evolution huoni kama glaciation ingekuwa sehemu flan za equator n not ktk poles?ukiacha gravitational force, Unajua km angle of reflection ni factor ya poles 2 kuwa na barafu? Unajua angle of reflection in geography maana yake nn? Ukijibu hyo maswali unaweza kujiuliza juu ya dunia ni wapi?
Hapo chacha,,
 
pole! tongo tongo unalodai kuwa nalo si dogo, ni zege. jitahidi kusoma vitabu vya jiografia. hakuna mbingu inayogusika kisayansi, ubluu uuonao ni mwisho wa upeo wa macho yako. kiimani ulivyofundishwa endelea kuamini.
Amen
 
Debrah01 umejibu vizuri sana na kitaalam, ila sina uhakika kama mleta mada atakuwa amekupata. Ukiangalia maswali yake utaona anahitaji maelezo ya awali (basics) ya mambo ya anga. Pia kwa lugha rahisi ili angalao apate kile kitakachopunguza kiu yake.
Kweli kabisa mkuu ameshanitoa tongotongo nawashukueu sana mlio nielimisha
 
Mkuu ukiona hivyo ujue mleta uzi "ameingia mwezini"
Heshma ni kitu cha bure mkuu
Kama umeshindwa cha kuongea bora ungekaa kimya tuu kama wengine usicoment ili na wewe uonekane umechangia mada,,
 
Katika uumbaji wa mungu vipo vinavyoonekana karibu hadi tunaiga na kuumba na sisi binadamu lakini katika muonekano wa mbingu nikiangalia sana nashindwa kuelewa kuwa mungu aliyumia materials gani,,namaanisha kuwa mbingu tunayoiona huwa niya aina gani,yaani ni ngozi au zege au kitambaa au leizer au plastic au playwood au ni nylon,,wajuvi maomba mnitoe tongotongo
Mwisho wa siku tutaishia kusema ' Akili zake hazichunguziki' zaburi136:5 & zaburi 139:6
 
Katika uumbaji wa mungu vipo vinavyoonekana karibu hadi tunaiga na kuumba na sisi binadamu lakini katika muonekano wa mbingu nikiangalia sana nashindwa kuelewa kuwa mungu aliyumia materials gani,,namaanisha kuwa mbingu tunayoiona huwa niya aina gani,yaani ni ngozi au zege au kitambaa au leizer au plastic au playwood au ni nylon,,wajuvi maomba mnitoe tongotongo
tumblr_static_tumblr_static__640.jpg
 
Two ways to answer your question:

Biblically, mana mimi ni mkristo ukisoma katika Mwanzo (Genesis) 1:7-9
Kwamba Mungu katika uumbaji alitenganisha maji, ya juu akayaita Anga, na Anga akaliita Mbingu. Then ya maji ya chini akayaamuru yakusanyike pamoja then akayaita bahari etc, ili nchi kavu ionekane... SO, KUKUJIBU kwa upande huu mimi nitakwambia hiyo mbingu unayotaka wewe kuigusa ni maji ambayo Mungu aliyatenga. Sijajua Quran imeandikaje mana bado sijaisoma. Aliesoma atatusaidia.


Quraan inasema katika Sura ya 23 (almuuminuun) katika aya ya 17 inasema"And we have created above you seven layered heavens,and never have we been of (our) creation unaware(Na kwa yakini tumeziumba juu yenu njia saba.na hatukuwa wenye kughafilikika na viumbe.
Tafsiri ya haraka inasema bila shaka tumeumba juu ya wanadamu njia saba. Step by step(moja baada ya nyengine)na hizi zilizotajwa hapo ni tofauti katika surat ya 71(surat Nuh).
Ambayo pia inasema yeye mungu kaumba mbingu saba katika tabaka tabaka(from area to area) Hapo juu anaelezea njia.kuna njia saba na kuna mbingu saba,vitu tofauti hivyo!. Mbingu saba zipo juu ya njia saba na njia saba zipo chini ya mbingu saba.Njia saba mungu ameziumba from bottom of the earth to 640 kilometres.Mungu kaumba tabaka saba kutoka katika tumbo la ardhi umbali wa km 640,kutoka tabaka kwenda tabaka.Ya kwanza kabisa inaitwa Troposphere ipo 13 miles kutoka katika tumbo la ardhi,tabaka hili ndiyo iliyobeba 99.99ya hewa zote .Asilimia 78% ni hewa ya Nitrogen,asilimia 21% ni Oxygen na asilimia 0.03 ni Carbon dioxide.asilimia % zilizobaki ni hewa nyengine.Juu yake kidogo kuna Stratosphere tabaka ambalo mfumo wa tabaka anga katika hali ya usafiri huwa inatumika,pia njia za mawasiliano katika hewa,hapo ndiyo kuna anga la kitaifa na kimataifa.Baada ya hiyo juu kidogo kuna ya tatu inaitwa Ionosphere ni tabaka ambalo lina hali ya mfumo wa umeme Radio zote na simu zote zinapatikana duniani kwa kutumia tabaka hilo ni tabaka ambalo lina mfumo wa hali ya kiumeme.kuna ya nne inaitwa Thermosphere hii ndiyo inafanya mfumo wa hali ya joto ila nayo maelezo yake ni mengi hayatoshi kwa hapa.kuna Ozone Layer ndiyo inasababisha kuzuia dunia isiangukiwe na mawe makubwa na tabaka hili lina kazi saba(labda kwa maelezo zaidi usome pia mambo ya ULTRAVIOLET. Baada ya hiyo kuna Thermosphere na Exosphere.Japo sijazigusia nyengine mkuu kwa mfano pia na mbingu ila suala kama hili unaweza pia kuanzisha mada maalum kuliko kuwa mchangiaji.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom