Hivi ni vita kali sana inatakiwa ujipange

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
HII NI VITA KALI SANA, INATAKIWA UJIPANGE
Kuwa bora ni vita kali sana, kwa sababu kila kinachokuzunguka kinakulazimisha kuwa kawaida.
Kuwa tofauti ni vita kali sana, kwa sababu kila mtu anategemea uwe kama wengine walivyo.
Kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako ni vita kuu kuliko zote utakazokuja kupigana kwenye maisha yako.
Vita hii itaanza na wewe binafsi, utapambana na mawazo yako, kuna ambayo yatakuambia inawezekana na nenda. Kuna mengine yatakuambia ya nini kujitesa na wakati maisha yenyewe ni mafupi. Unahitaji kushinda vita hii ndani ya akili yako kwanza.
Halafu unakuja nje ambapo kuna maadui wengine wengi wanakusubiri kwa hamu sana wazigaragaze ndoto zako. Wataanza kukuambia huwezi, haiwezekani, hujui unachofanya, wenzako walijaribu na wakashindwa. Safari inaweza kuishia hapa, ila kama utakuwa na moyo na kuendelea bado vita haijaisha.
Ukiianza safari utakutana na vita nyingine kubwa sana. Hii ni vita ya changamoto, kushindwa. Ni vita ngumu sana na njia pekee ya kuishinda ni kutokukata tamaa, kuwa king’ang’anizi na kuwa mvumilivu. Ni vita ngumu mno na inawashinda wengi. Lakini hata utakaposhinda vita hii bado sio mwisho.
Ukishafanikiwa kuna vita nyingine kubwa sana, na hii ni vita ya kulewa mafanikio, kuona wewe ndio umeshaweza kila kitu. Hapa unasahau kufanya vile ambavyo vimekufikisha kwenye mafanikio yale na hivyo unaanza kuporomoka kwa kasi kubwa sana. Kushinda vita hii ni kutokubweteka na mafanikio yoyote yale, hata yanapokuwa makubwa kiasi gani. Wewe endelea kuweka juhudi bila ya kujali umefikia kiwango gani. Endelea kuwa tofauti kila siku.
Hii ni vita kali sana ambayo haina mwisho, ni ngumu na ukizubaa kidogo tu inakumaliza. Unahitaji kujitoa sana na kuwa tayari kufanya lolote ili usiondolewe kwenye njia hiyo uliyochagua.
Kama watu 100 watapanga kufikia mafanikio, hivi ndivyo vita hii kali itakavyowapangua;
50 watashindwa kwenye vita vya ndani ya akili zao wenyewe. Wataona haina maana na ni bora kuendelea kuwa kawaida. Wanabaki 50.
30 watashindwa kwenye vita ya kukatishwa tamaa na wengine. Hawa watakubaliana na maneno ya kutisha watakayoambiwa na hawatachukua hatua. Wanabaki 20.
15 wanashindwa kwenye vita ya changamoto na ugumu wa safari. Wanakata tamaa wakiwa wameshainza safari. Wanabaki 5.
4 wanashindwa kwenye vita ya kulewa mafanikio. Wanakazana sana na kufikia mafanikio ila baada ya hapo wanapoteza au wanashindwa kukua zaidi. Anabaki 1.
1 ndio anafikia mafanikio ya kweli na anakuwa ameshinda vita zote.
Nina hakika huyu mmoja ndio wewe kwa sababu kuna watu 99 wanaokuzunguka hawapati maarifa unayopata wewe.
 
Taabu kweli! Mie thread za hivi nashindwa kuzisoma, hata kama story nzuri utachoka tu, jaribu kufupisha au kuiandika vzr zaidi
 
Amina. Bilashaka wewe pia ni mpiganaji na nàamini hili umejifunza kwenye harakati za kuangaaika. Naungana nawe kabisa na hongera kwa kuleta kifungua ufahamu hiki mbele ya jamii hii, Mungu akubariki sana.

Katika kitu cha ajabu sana ambacho hunishangaza chini ya jua kila mwandamu ana ndoto za kuwa ngazi fulani. Ajabu zaidi watu wengi ndoto zao zimekufa nao wako kwenye taabu zisizopimika wanajuta na kulia wanajiliwaza kwa maneno dhaifu kama Mungu hakupenda, sikusomeshwa na kadhalika!
Kama alivyosema Muweka bandiko vita ni kali sana tena sana. Kushinda lazima uwe na nguvu ya rohoni, kwenye maumbile ya binadamu roho pekeyake ndiyo inaweza kushinda kikwazo chochote. Ikiwa kitatoka katika nafsi yako au kwenye mazingara yako. Asikudanganye mtu awaye yeyote mafanikio ni zao roho na sio mwili Hivyo kufanikiwa lazima roho iwe kiongozi na sio mwili. Fikra zinafuata mazingira zinafanya fair reasoning, zonapima urefu wa vikwazo na kutoa maamuzi; hapa sipiti na hapa napita Hivyo kukwamisha mafanikio.

Roho haina hicho hii ni kwa sababu energy level iliyonayo ni kubwa kuliko ya mwili,kikwazo ambacho mwili haupita roho inapita na ndiyo maana kufanikiwa ni rahisi.

Bila kuopareti kwenye ngazi ya roho kupata mafanikio ndiyo maana wanaojua utaratibu huu wana kwenda kwa wakuu wa gizaa kuomba nguvu za roho ili kuvuka na tunaona wengi wakivuka. Mwili peke yake hawezi kukuvusha.
Wengine wanasema mafanikio unaweza kuyapata tu ukiwa kwa Mungu au Shetani na si Vinginevyo, kiuhalisi sasa shetani ni nani na Mungu ni nani? Jibu rahisi ni Roho zinazoongoza maumbile ya ulimwengu, ikimaanisha kuwa mafanikio ni zao la rohoni.

Hivyo basi ukitaka kufanikiwa kupitia Mungu fuata utaratibu wake na ukitaka kufanikiwa kupitia shetani fuata taratibu zake. Either way there price to pay! No free lunch !

Nakushukuru tena kwa bandiko lako tamu sana Asante.
 
Asante sana kwa maoni yako mazuri.
 
Natamani ungeendelea kuandika mkuu, thnxs sana
 
Waafrica wengi ni wavivu wa kusoma. Hatupendi kusoma. Walisema ukitaka mtukana mtu mweusi mwandike kwenye kitabu/maandishi.

Hujui ukiwa na IQ ya kutosha (sio lazima uwe genius) utaweza kupanga unachoongea/kuandika! Ndo maana ukiandika hovyo hatusomi tunajua n pumbu tu!
 
Yaani umehit mulemule maana kuishinda nafsi nakufikia mafanikio nivita ngumusana hapa kikubwa nikuwa na maamuzi sahihi lkn pia kupunguza kuombaomba ushauri kwawatu maana wanachangia sana kuwavunja watumioyo nahasa ukiomba ushauri wakitu ambacho mtuhanataaruma nacho utaishia kukatishwa tamaa tu chamsingi jifunzekuchukuwa maamuzi nakuyatekeleza ww kamaww maana watuwengi wameshindwa kufikia malengo yao kwakukatishwa tamaa nawatu wanao waomba ushauri japokuwa nenolangu sio sheria lkn epukasana ushauri wawatu maranyingi unakatisha tamaa
 
Vilevile akilizakuambiwa changanya nazakwako ukiombaushauri ukaona unapotoshwa au unapotezwa basi achana naushauri HASI tafuta ushauri CHANYA kikubwa jifunze kuishinda nasfiyako ukiona inakusababisha kushindwa Vita ya mafanikio wekabidii kwakile unachokiamini kwamba kitakufikisha kwenye safari ya mafanikio hata biblia inasema lolote mkonowako utakalotaka kulifanya naulifanye kwabidii zote
 
Asante sanaaaaaa kwa maoni yako mazuri na uelewa wako uliompana. Thats good.
 
Vilevile akilizakuambiwa changanya nazakwako ukiombaushauri ukaona unapotoshwa au unapotezwa basi achana naushauri HASI tafuta ushauri CHANYA kikubwa jifunze kuishinda nasfiyako ukiona inakusababisha kushindwa Vita ya mafanikio wekabidii kwakile unachokiamini kwamba kitakufikisha kwenye safari ya mafanikio hata biblia inasema lolote mkonowako utakalotaka kulifanya naulifanye kwabidii zote
Asante sana..
 
Waafrica wengi ni wavivu wa kusoma. Hatupendi kusoma. Walisema ukitaka mtukana mtu mweusi mwandike kwenye kitabu/maandishi.
Aaah!! Utatukanwa wewe tu!!
Kwa upande wangu mie andika upuizi woote sisomi ila ukinitukana hata kwenye ukurasa wa 615 mstari wa 9 kati ya mistari 25 na nane la 6 kati ya maneno 12 kwa kitabu cha kurasa 924 nitajua tu!
Na hapo ndipo nitacoment jibu kwa herufi kubwa 'MWENYEWE'
 
Back
Top Bottom