Hivi ni muda gani sahihi wa kuanzisha mahusiano mapya?

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,662
Habarini wana MMU!

Katika mahusiano ya Mapenzi kuna kitu kimoja kikubwa sana! nacho ni kuachana na Mpenzi wako! Tukubalie kuwa hata kama mlipendana vipi na mpenzi wako,alikupenda vipi au ulipenda vipi lakini lazima itafika mda mtakuja kuachana na mpenzi wako!

Haijalishi ni kiasi gani mlioneshana Mapenzi na mmedumu kwa mda gani lakini lazima mtakuja kuachana!

katika kuachana inategemea na njia au kisababishi cha nyinyi kuachana! Ugomvi,kifo ni sababu kubwa ambazo hufanya wapenzi kuachana! Haijalishi walipendana sana au vipi lakini kifo kikitokea kwa mmoja wenu atakuacha na wewe utabaki peke ako,na sio kila ugomvi lazima mmachane lakini kuna ugomvi mwingine hupelekea kuacha ukiwa umesababishwa na kuchokana au kitu kingine!

Pamoja na sababu nyingi ambazo husababisha wapenzi kuachana,Je ni mda gani sahihi wa kuanzisha Mauhusiano mapya mara baada ya kuachana na mpenzi wako?

Tukumbuke kuwa mzizi wa kumpenda mtu hutokana na Kutamani hakuna real love inayo anza bila tamaa...unaweza kujikuta umemtamani girl fulani au boy fulani na baadae kujikuta una mpenda kabisa!

Je ni mda gani sahihi sasa wa kuanzisha mauhusiano mapya?
 
Hakuna formula!! Utakapokua umeridhia unaanzisha hata kama ni dakika 1 imepita
 
muda sahihi wa kuanzisha mahusiono ni kipindi cha masika jua linapo kuchwa mvua zikinyeesha kunakuwa na unafuu wa kuanzisha mausiano maana ndio kipindi cha maindi kuota!
 
Maumivu ya uhusiano wa kwanza yakiisha, unaweza kufugua ukurasa mpya maana kichwa kinakuwa kimetulia. Lakini kuwa makini na huko uendako maana kunaweza kukuvundia pia.
 
Kuna wanaoingia kwenye mahusiano mapya siku 1 baada ya kuachana na wazamani, Kuna wengine hukaa mda mrefu na kuna wengine kutokana yaliyomsibu kwenye uhusiano uliopita anaamua kukaa bila kuwa na uhusiano kabisa...
 
Ni vyema kusubiria mpaka pale utakapokuwa umejiridhisha kweli kuwa mmeachana na hamna namna nyingine mkaweza kurudiana kama kuachana kwenu hakujasababishwa na kifo, maana unaweza kuanzisha mahusiano ukajikuta umeangukia kwenye mikono ya wanyang'anyi.
 
Back
Top Bottom