KENGE 01
JF-Expert Member
- Mar 12, 2021
- 1,769
- 4,389
Mishale ya Usiku mnene mziki wa taratibu wa mwanamama ( "Celine Dion-Power of love" ) unasikika kwa mbali kwenye redio...gafla nashtushwa na mlio wa simu ulioita mara 3 mfululizo,,Wakati usingizi unatawala kichwani kwa unyonge nanyanyua simu na kutazama ni SHEM wangu anaepiga!!wakati bado sijakaa sawa natafakari Kunani?Mbona simu za usiku wa manane?SHEM akapiga tena ndipo nikapokea kusikiliza Kunani??
Sauti ya kukwaruza ikiambatana na Vilio ndio ilikua inasikika kwenye simu SHEM aliishia kutamka maneno mafupi tu kwa uchungu na kilio "AMEONDOKAAAA" sauti ya Shem iliendelea kujirudia ikiniita "Shem!!ameondokaa" ikiambatana na vilio vikali sana mithili ya mtoto alienyimwa ziwa na mamaye ilihali anasikia njaa....Nikiwa nimepigwa butwaa nisielewe kipi cha kufanya nikamwambia "Shem basi punguza jazba unieleze nani kaondoka na kaenda wapii??Hakuna jibu la maana Shem alilonipa zaidi ya kilio cha "AMEONDOKA AMEONDOKA"
(Shem wangu uyu ni dada wa Mke wangu,Mke wangu alienda nyumbani kwao kujifungua na mpaka dakika iyo niliambiwa Mke yupo labour kwa ajili ya kujifungua)
Kabla sijakaa sawa ikaingia simu sms fupi ya baba mkwe ambayo iligeuza furaha yangu kuwa DOA SMS ilisomeka
"......MWANANGU Kenge1 TUMEPOTEZA MKE NA MTOTO WALIPOKUA LABOUR HATUPO NAO TENA wote WAMEFARIKI DUNIA....."
Taratibu mwili ulianza kupata joto mithili ya injini ya gari lililotembea umbali mrefu,,,Akili ilisimama nisielewe kipi cha kushika na hata ivyo nguvu zote ziliisha na kupelekea kudondosha simu ambayo hata nilikua sijui nimedondoshaje..Nilijihisi labda nipo ndotoni??Au ni utani?? Lakini haikuwa na ujanja.ndio Uhalisia haikua ndoto.
Ndipo akili ilipoanza kuwaza mambo zaidi ya billioni saba kwa sekunde moja..Niliwaza watoto,Nikawaza ya dunia,Nikawaza ya akhera kwa ufupi hakuna kitu ambacho sikuwaza kwa mda ule..Usiku ulikua mrefu sana na nikaona isiwe tabu nikafunga Safari usiku uleule kuelekea ukweni
Nilipofika sikukuta kingine zaidi ya Vilio tu kina Mama walilia wengine walizimia na wengine walitoa maneno ya kumkufuru Mungu.Wakati bado nashangaa nisielewe nani wakumsalimia nani wakuongea nae baba Mkwe akanishika mkono na kunivuta pembeni na kunipa maneno ya kunifariji ambayo hata ivyo kwa wakati ule yalikua yanapitia kushoto na kutokea sikio la kulia..bila kupoteza muda nilimuomba jambo moja tu baba Mkwe(Kumuona Mke wangu) Baba mkwe aliniuliza "Unamoyo?? " Nikashangaa lakini nikajibu "ndio moyo ninao" basi akanishika mkono tukaelekea ndani ambapo pia nilikuta kuna Vilio mara mbili zaidi ya vile vya Nje
SHEM aliponiona tu akaanza kulia kwa yowe upyaa uku akisema "SHEM DADA AMEONDOKAAAA DADA AMEONDOKAA"" Kulikua na majirani waliokua wakituliza vilio ndani mule na wengine wakitoa nje watu waliozimia kiukweli ilikua ni HUDHUNI IMETAWALA..Basi moja kwa moja Mzee akanipeleka kwenye chumba ambacho pia tulivyofika mlangoni aliniuliza tena "Unamoyo??" Nikajibu ndio kwa ujasiri akaniamuru niingie ndani ya kile chumba..
Basi baada ya kuingia nilikuta Mtu kafunikwa shuka mpaka juu(Mwili mzima) na nilimkuta Mama mkwe ambapo alikua amelia mpaka sauti imekata yani ni kama anakoroma tu bila kutoa maneno..Basi mama mkwe hakuongea chochote licha ya kumsalimia Alichokifanya Alinifunulia tu yule mtu aliefunikwa shuka ndipo niliiona SURA YA MKE WANGU akiwa amelala USINGIZI WA MILELE sijui nilifikaje chini lakini nilijikuta nimekaa chini miguu inatetemeka,,Mwili wa baridii lakini Jasho linatoka mpaka kwenye ulimi mithili ya maji ya bwawa la Nyerere..Nisielewe kipi cha kufanya Machozi yamenilenga kwa mbalii,,Moyo unatamani kulia kwa sauti kubwa sana,Mdomo uko wazi(sauti haitoki) nisielewe kipi cha kufanya Na kuendelea kujiuliza maswali ambayo hata ivyo nilikosa majibu..
Eeh MKE WANGU kwanini umeondoka?
Kwanini hukuniaga Mke wangu??
Nani atalea watoto MKE WANGU?
Nani atapika chakula MKE WANGU??
Nani ataziba pengo lako kipenzi changu??
Rudi basi uwaage wadogo zako MKE Wangu??
Eeh mke wangu unheniachia basi ata zawadi ya uyo mtoto alietumboni,Sasa mbona umeondoka nae MKE WANGU??
Ntawajibu nini watoto wetu wakitoka shule Mke wangu?
IVI NI KWELI UMEONDOKA MPENZI??
Cc KENGE 01