Hivi ni kweli Tanzania tuna upinzani wa kweli?

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,215
3,683
Kwa wale wafuatiaji wa siasa za Tanzania tangu tumeingia mfumo wa siasa wa vyama vingi tangu 1995 hadi leo hii mtagundua siasa za upinzani zimebadilika.

Enzi za nyuma kipindi tukiwa kina Dk.Slaa, Lipumba, Mtikila, n.k wapinzani walikuwa na hoja na agenda kali za kupambana na ufisadi, wizi serikalini, kutete wananchi wenye kipato cha chini, katiba mpya, tume huru, n.k

Leo hii wapinzani wameacha agenda za msingi kila siku wamekuwa wakigombana wenyewe kwa wenyewe. Leo hii upinzani ukiangalia kuna team Lipumba, team Seif, team CHADEMA, team Zitto Kabwe.

Leo hii ndani upinzani wamekuwa wakitupiana kejeli wenyewe kwa wenyewe mara ruzuku, mara CCM B, mara huyu hivi mara huyu hivi mara huyu vilee kiukweli upinzani mimi najiuliza hapa hivi ni kweli bongo tuna upinzani wa kweli?
 
kama hawapo ni hatari kwa mradi wa B7 ajira itaota mbawa.ngoja upinzani ufe mwende ifakara mkalime mpunga.
 
1992 na siyo 1995. Upinzani upo muulize jamaa mmoja anaitwa nani sijui, anasuburi baada ya miaka mitano ndo aje kugombea urais.
 
1992 na siyo 1995. Upinzani upo muulize jamaa mmoja anaitwa nani sijui, anasuburi baada ya miaka mitano ndo aje kugombea urais.
kugombea uraisi sio tijaa mimi wasiwasi wang kila nikiwangalia wapinzani huwa ninapatwa wasiwasi ivi ni kweli upinzani upo au upinzani uliokuwepo ni miradi ya watu kutafuta chakula
 
Kwa wale wafuatiaji wa siasa za Tanzania tangu tumeingia mfumo wa siasa wa vyama vingi tangu 1995 hadi leo hii mtagundua siasa za upinzani zimebadilika.

Enzi za nyuma kipindi tukiwa kina Dk.Slaa, Lipumba, Mtikila, n.k wapinzani walikuwa na hoja na agenda kali za kupambana na ufisadi, wizi serikalini, kutete wananchi wenye kipato cha chini, katiba mpya, tume huru, n.k

Leo hii wapinzani wameacha agenda za msingi kila siku wamekuwa wakigombana wenyewe kwa wenyewe. Leo hii upinzani ukiangalia kuna team Lipumba, team Seif, team CHADEMA, team Zitto Kabwe.

Leo hii ndani upinzani wamekuwa wakitupiana kejeli wenyewe kwa wenyewe mara ruzuku, mara CCM B, mara huyu hivi mara huyu hivi mara huyu vilee kiukweli upinzani mimi najiuliza hapa hivi ni kweli bongo tuna upinzani wa kweli?
Tuna wababaishaji Tu upinzani wa kweli haupo. Tangu vyama vingi vianze viongozi Wao Ni walewale Kama masultani. Na mwingine kazuka hivi karibuni anajiita Kiongozi Mkuu i.e Supreme Leader, Kama ayatollah vile.
 
Haya kachukueni buku saba Lumumba fasta. Hongera kwa kuingiza kitu mfukoni.
 
Wapinzani halisi ni wale waliotoka ccm na kuunda ccm b. Yaani Kingunge, Lowasa, Sumaye na Guninita.
 
Wapinzani halisi ni wale waliotoka ccm na kuunda ccm b. Yaani Kingunge, Lowasa, Sumaye na Guninita.
kwani mpendazoe,slaa,mrema, shibuda,seif ivi walitokea chama gani wakaenda chama gani
 
Habari wakuu!

Tujadili hili jambo kwa dhati, kweli Tanzania kuna upinzani wa kweli? Napata mashaka nikifikiria hili, kwa sababu ni zaidi ya miongo miwili upinzani upo Tanzania lakini haujaweza kukiathiri chama tawala hata nusu yake tu, sioni dira ya upinzani ni nini, ni ukweli uliowazi kwamba chama tawala hakiwezi kutoka madarakani kwa mfumo uliopo wa katiba hii na mfumo wa tume ya uchaguzi uliopo, ni na uhakika kwa mifumo hii miwili chama tawala hata kikiweka jiwe ligombee na upinzani, jiwe litashinda tu wakitaka. Sasa kama kweli wapinzani wanayajua haya kwa nini hawayaongelei yarekebishwe? Kwa nini kila wakijifanya kushindwa uchaguzi ndio wanazungumzia tume sio huru, mara katiba, then wanakaa kimya kusubiri uchaguzi tena kwa makosa yaleyale, kweli kuna malengo hapo? Au ndio kusema wakina prof Babu, wakina kolimba na wengineo waliotangulia ndio walikuwa wapinzani wa kweli?
 
Back
Top Bottom