Hivi ni kweli serikali haipi??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni kweli serikali haipi???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nuru John, Nov 19, 2010.

 1. N

  Nuru John Member

  #1
  Nov 19, 2010
  Joined: Aug 26, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asalaam aleiykum ndugu zangu wa JF?

  Mimi sikumuelewa siku ile Mama yangu Anne Makinda alivyomjibu Tundu Lissu kuwa ile hoja ya Waziri Mkuu haikupelekwa Bungeni na Serikali wakati alimwita Mwanasheria Mkuu Mhs.Jaji Werema aende akatoe hoja ya serikali ya kumpitisha Waziri Mkuu.

  Kama nitakumbuka vizuri if not I stand to be corrected,Tundu Lissu alinukuu vipengele vya sheria vinavyotaka Kambi ya upinzani kupewa nafasi ya kuzungumzia hoja yoyote inayopelekwa na Serikali pale Bungeni kabla ya kujadiliwa,lakini kwa mshangao wangu niliona Mama yangu na Spika wetu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda alijibu kuwa kwa wakati ule kulikuwa hakuna Serikali na utaratibu uliendelea kama ilivyompendeza yeye.

  HIVI NI KWELI SERIKALI HAIKUWEPO KWA WAKATI ULE?Mhs.Jaji Werema aliingia Bungeni kwa Capacity ipi?

  Nijuavyo mimi kipindi chote ambacho Mhs.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kabla hajateua Mawaziri na Manaibu Waziri kama ilivyo kwa kipindi hichi cha sasa ambapo hakuna Viongozi hao wa kisiasa Makatibu Wakuu wa Wizara ndio wanaoendesha Serikali katika kipindi hiki cha mpito,sasa iweje watanzania tuambiwe kuwa hakuna Serikali au waliofia kuwa CHADEMA wanaweza wakawa so NEGATIVE kwa kutotambua uteuzi wa Rais kwasababu hawamtambui kama walivyotamka kupitia kwa mwenyekiti wao wa chama??!!!!

  Naomba tujadili hili ili nami nipate uelewa ambao labda sina.
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Huyo MAma kaingia kwa nguvu ya Mafisadi na kiukweli bila kusema mambo ya ubaguzi wa kijinsia, huyo mama hana uwezo wa kuliongoza bunge, siku hiyo ya mwanzo tu inaonekana bunge limeshamshinda, Huwezi kusema hakuna serikali na wakati kuna Raisi wa nchi (japo kaingia kimizengwe) na ndie aliyemchagua Mwanasheria huyo mkuu,
  Mama Makinda alichemsha na alitaka kujionyesha kuwa yupo sahihi
   
Loading...