Hivi ni kweli kuwa kila Mwana JamiiForums ana degree?

Kuwa na degree au la sio big deal, jambo la msingi ni uzito na weledi wa bandiko, wengine huku jamvini tunafuata kupata elimu, uzoefu wa watu na habari mbali mbali, sio kiwango cha elimu ya mtu kwani kuna watu hapa hawana elimu kubwa lakini ukisoma bandiko lake unasema yes! Unatoka na kitu, na kuna wanaojigamba wamesoma sana lakini ukisoma bandiko lake, ukaangalia hoja yenyewe na mtiririko wa mawazo; thought flow, unaona kabisa huyu "alihudhuria darasani tu" akatoka mtupu kama alivyoingia!
 
Mimi nnavyojua kigezo cha kujiunga JF sio degree. Ila kipindi cha awamu ya nne ya mheshimiwa Jakaya Kikwete vijana wengi wameenda vyuo vikuu kutokana na kuwa na vyuo vingi vinavyotoa elimu ya juu, pia utolewaji wa mkopo hadi kwa waliopata division three katika vyuo vya serikali.
Hivyo basi sioni ajabu kwa wanajf wengi kuwa na degree. lakn mtu kama kweli nina degree nafungwa na nini ninapoelezea au kutolea mfano wa kitu kilichofanyika chuo?
 
Kuwa na degree au la sio big deal, jambo la msingi ni uzito na weledi wa bandiko, wengine huku jamvini tunafuata kupata elimu, uzoefu wa watu na habari mbali mbali, sio kiwango cha elimu ya mtu kwani kuna watu hapa hawana elimu kubwa lakini ukisoma bandiko lake unasema yes! Unatoka na kitu, na kuna wanaojigamba wamesoma sana lakini ukisoma bandiko lake, ukaangalia hoja yenyewe na mtiririko wa mawazo; thought flow, unaona kabisa huyu "alihudhuria darasani tu" akatoka mtupu kama alivyoingia!
Pamoja na kuudhuria kweli chuon lakn hatuwezi kufananisha mtu wa darasa la saba na wa chuo kikuu.mimi nimesha mshuhudia mtu mmoja anavyoongea kama humjui unaweza sema kafika chuo kikuu na ana ka-kakiingereza ka kusomea mwezi mmoja. lol . kuna hoja anavyochambua unaweza vunjika mbavu.muda mwingine kuongea mbele ya hadhara ni kipaji. kuna siku alinambia kuwa mwanae wa alikuwa amepata daraja la PASS (kabla Ndalichako hajarudisha mfumo wa division) amemnunulia zawadi na anasubiri mwanae apangiwe high school.YELEUWIIIII nlickeka mpk akajisikia vibaya. sikumuonea huruma kwa kuwa hujafanya mjuaji
SOMO; Tuwape moyo vijana wetu wasome hadi elimu ya juu tusiwakatishe tamaa kwa kuwaambia kuwa kwa elimu yake kiduchu anaweza kujifananisha na mtu aliye na degree. l
 
Ilipashwa kua hivyo na tulivyoanza ilikua hivyo ndio maana JF pakaitwa mahali pa watu wa akili kubwa. Ila kwa sasa nikiona threads za humu na wachangiaji wanavyochangia au kujibu nina uhakika mia kwa mia kuna mpaka Ex STD 7 humu.
 
Ni kweli kila mtu humu ana stashahada yake
za uongo
Za umbea
Za wizi
Za ujuaji
Za ulozi ushirikina na mambo ya giza
Za umalaya
Za ushenzi
Za ukweli
Za heshima
Za hekima
Za ukorofi
Za upole nknk
Hakika ndani ya JF kila mtu ana degree yake
 
Back
Top Bottom