Hivi ni kweli fukufuku anafanya matiti yawe Makubwa ya kuvutia na kusisimua?

Enyagoloizi in Haya tongue,(Nyagoloizi/tropical swamp beetle in English). Hao ni kweli uchochea (stimulus after a sting) homoni za ukuaji wa viungo vyenye mafuta mengi. Kama ukiwa 'calling' ya 'spiritual entrepreneurship' endelea na mradi wako: matunda yake matamu, hutojutia kuyaonja japo itachukua muda kupata faida kwa ujumla.
Duh...
 
Kwan kuna faida gani kuwa na matiti makubwa kwa mwanamke? wao wamekataa sixpacks wanataka hela.
Salaam Wapenzi wangu,

Kuna wadudu wadogo wanachimba shimo sehemu penye mchanga, inadaiwa ukimchukua ukamung'atisha kwenye chuchu la titi, inarutubisha na kufanya ziwa liwe kubwa la kupendeza. Hata ukinyonyesha halilali na kuwa ndarandefu.

Wadudu wengine walioonesha mafanikio makubwa wanakaa kwenye maji. Wana rangi nyeusi, wanaogelea sana, Wanaitwa nderandera au wachora ramani au Wachora barua [Siwafahamu jina lakini la kitaalam wana rangi kama nyeusi hivi]. Ila wanaogelea kwa speed, sio rahisi kumkamata.

Wanawake wamekuwa wakiwatumia kwa matumizi ya kupendezesha au kukuza Matiti.

Asilimia kubwa ya wakina Dada wameng'atwa na hawa wadudu ili matiti yakue. Mimi nata niwatafute niwafuge nianze kuwauza.

Je, Ntatengeneza faida?

Kwa wale waliowakamata na kuwalazimisha wawang;ate chuchuchu, je ulifanikiwa kukuza matiti?

Naomba kujua kama fukufuku wanakuza matiti.

Fukufuku usipomuimbia hatoki. Lazima uwaimbie wimbo wake...Fukufuku toka baba yako kaja kakuletea Mkate... Wakati wa kumtoa shimoni unatakiwa uwe umekaa, ukiinama au kuchuchumaa huwezi mpata.

si upo kanda ya ziwa,
tafuta mwenyeji yoyote akuoneshe maana nakumbuka tulivyokuwa wadogo huyo mdudu ukikuta shimo lake, unaanza kupiga pembeni huku unamuimbia wimbo wa kumbeleza atoke na anatoka,
sijui ilikuwa sababu ya bugudha zetu lakini akitoka unashangilia kama umewin lotto vile hahaa

kingine ilikuwa wale ndege nyangenyage na wao walikuwa wakipita, mnaanza kuwaimbia huku mmenyoosha mikono juu mkiwaomba wawarefushie kucha 😁

wengine nao walikuwa wanaamini kuchanjia tango ili kuongeza maumbile

mambo ni mengi na utotoni nilikuwa naamini ila kwa sasa naona kama conspirancies tu
Mkuu wewe ni mtu wa sehemu za kusini ama ulikulia huko ukajua hiyo michezo ?
 
Salaam Wapenzi wangu,

Kuna wadudu wadogo wanachimba shimo sehemu penye mchanga, inadaiwa ukimchukua ukamung'atisha kwenye chuchu la titi, inarutubisha na kufanya ziwa liwe kubwa la kupendeza. Hata ukinyonyesha halilali na kuwa ndarandefu.

Wadudu wengine walioonesha mafanikio makubwa wanakaa kwenye maji. Wana rangi nyeusi, wanaogelea sana, Wanaitwa nderandera au wachora ramani au Wachora barua [Siwafahamu jina lakini la kitaalam wana rangi kama nyeusi hivi]. Ila wanaogelea kwa speed, sio rahisi kumkamata.

Wanawake wamekuwa wakiwatumia kwa matumizi ya kupendezesha au kukuza Matiti.

Asilimia kubwa ya wakina Dada wameng'atwa na hawa wadudu ili matiti yakue. Mimi nata niwatafute niwafuge nianze kuwauza.

Je, Ntatengeneza faida?

Kwa wale waliowakamata na kuwalazimisha wawang;ate chuchuchu, je ulifanikiwa kukuza matiti?

Naomba kujua kama fukufuku wanakuza matiti.

Fukufuku usipomuimbia hatoki. Lazima uwaimbie wimbo wake...Fukufuku toka baba yako kaja kakuletea Mkate... Wakati wa kumtoa shimoni unatakiwa uwe umekaa, ukiinama au kuchuchumaa huwezi mpata.

Hili jambo hata mimi nimepata kusikia wadada wakisema kwamba wao walipokuwa wasichana (teenagers) walikuwa wakichukua hao Fukufuku/Fukwe na kuwaweka wang'ate chuchu za matiti yao ili matiti yawe makubwa au yakue haraka nk,

Jambo hilo yawezekana likawa na ukweli na linahitaji tafiti za kisayansi ili kulithibitisha au kulipinga.

Utafiti wangu wa haraka/usio rasmi ni huu:-

Fukufuku ni mdudu anayeishi kwa kula wadudu wengine kama alivyokuwa buibui, nge nk, huyo yeye hutumia shimo lake kama nyumba yake na mtego pia kunasa wadudu, ukimchunguza utaona kichwa chake kimebeba hayo meno mawili marefu ambayo ndiyo silaha yake ya kukamatia wadudu mara mdudu anapotelezea humo shimoni mwake, humvuta mdudu na kumzamisha ndani ya mchanga, ninachofikiri ni kwamba hayo meno yake yatakuwa na sumu anayotumia kumuingiza mdudu ili afe haraka kabla hajamla jinsi nyoka anavyoingiza sumu kwa windo lake.

Sumu za aina hiyo zinaitwa Venom ambazo zinapatikana kwa Nyuki, Nyoka, Nge, aina fulani za buibui, Dondola,Nyigu nk, Sumu hizo kwa asili ni protein (protein in nature), na zinapoingia mwilini mwa mtu zinakuwa ni "antigen" kwa minajili hiyo mwili huzalisha "antibodies" kupambana na hizo sumu, tofauti ni hii; Sumu ya nge, nyoka, nyigu, nyuki ni kali sana (very stong) kulinganisha na sumu ya Fukufuku sumu ambayo ni kwa ajili ya kuua/ku paralyse wadudu wadogo mithili ya sisimizi ambao ndio chakula chake huyo Fukufuku, wadada wanaponatisha hao Fukufuku katika nyonyo zao, Fukufuku hung'ata na kuingiza Sumu mithili huyo Fukufuku anavyoingiza hiyo sumu kwa mdudu kwakuwa Sumu hiyo ni katika kiwango kidogo mno mnadada hasikii uchungu wa sumu bali husikia uchungu wa meno ya fukufuku tu na ile sumu huathiri eneo dogo la titi lililong'atwa na NADHANI hiyo sumu ni ile aina ya sumu inayoathiri damu na sio ile inayoathiri mishipa ya fahamu.

Kwakuwa Sumu imekuwa ni kitu kigeni katika titi basi Mwili taratibu huamsha askari kwenda huko kwenye titi (to the battle field) kuapeleka mashambulizi kwenye hiyo sumu kwa maneno mengine titi linakuwa ni uwanja wa mapambano kati ya Sumu na Antibodies (Askari wa mwilini).

Kama tunavyofahamu hali ya uwanja wa vita inavyokuwa kipindi cha vita ndivyo hivyo hali ya titi huwa katika kipindi cha mtifuano kati ya sumu ya Fukufuku na antibodies, ni katika hali hiyo titi linapovimba na hapo mdada ataona kuwa titi lake limekuwa.kubwa sababu ya Fukufuku.

Hali ya kuvimba kwa titi nayo hutegemeana na kinga ya muhusika.

Jambo la kujifunza ni hili; hata sumu ya nyuki, dondola,(sio za nge na nyoka) zinaweza kutumika kwa ajili ya Shughuki hiyo ni suala la utafiti zaidi tu.

Hii ni NADHARIA yangu binafsi kuhusu Fukufuku na nipo radhi kukosolewa na kujifunza zaidi katika kadhia hii.
 
Back
Top Bottom