Hivi ni kweli CCM hakuna kiongozi mzuri?

Kiriku

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
345
134
Nimekuwa nikipitia mijadala mbali mbali kwenye jukwaa la siasa tatizo kubwa nililoliona watu wamekuwa na ushabiki mkubwa wa vyama vya siasa.

Kwa mtazamo wangu tuna haja ya kwenda mbali zaidi tukaacha ushabiki wa vyama tukawapima viongozi kwa ufanisi wao na sio kwa vyama vyao, ninaposema viongozi namaanisha kuanzia ngazi za chini mpaka ngazi za juu.

Naomba kuwasilisha tujadili bila ya ushabiki wa vyama karibuni.

Sent from my iPhone using JamiiForums mobile app
 
Ndiyo, kwa sasa hakuna hata mmoja!
 
Dr Kingwangara namkubali sana anaakili nzuri kuliko hata Maselle na Mwigulu huyu jamaa akiongea unajua kabisa yupo sehemu asiyostahili maana juzi aliongelea swala la IPTL wendawazimu wa ccm wakambezaa na kunanga.. Karibu Upinzani Dr
 
...mfumo wa siasa wa tanzania hauruhusu mawazo huru ndo maana ushabiki wa vyama unashika kasi sana. Tangu enzi za zidumu fikra za mwenyekiti vyama vimekuwa ndo miungu ya wanasiasa na wafuasi wao. Huwezi kufanya lolote zuri au baya bila idhini ya chama na ukikiuka unanyang'anywa kadi hata kama linamaslahi kwa wananchi. Mf.angalia wabunge wa ccm ktk suala la katiba mpya,wengi wanataka serikali tatu ila wanaogopa vitisho vya chama hatakama wanajua sio matakwa ya wananchi. Uhuru na ubora wa viongozi ambao wataweza kusimamia haki ni pale tutakapopata katiba mpya yenye kuruhusu uhuru wa kuhama chama bila kupoteza nafasi yako....
 
inapendezaaa
 
Taja mmoja nikueleza machafu yake,hata kama ni mtendaji kata.sijawahi kuona punda milia asiye na mistari.
 
Mkuu hapo nakuunga mkono kuwa kuna haja ya kupitishwa sheria ya kuwa na mgombea binafsi itawaondolea viongozi wetu ukiritimba wa vyama vya siasa.

Sent from my iPhone using JamiiForums mobile app
 
Taja mmoja nikueleza machafu yake,hata kama ni mtendaji kata.sijawahi kuona punda milia asiye na mistari.

Mkuu hakuna binaadamu ambaye ni kamilifu wapo kina Ally Mohamed Kessy, Kangi Lugola, Hamisi Kigwangala n.k.

Sent from my iPhone using JamiiForums mobile app
 
Tatizo lilianzia pale mlipoamua kuliua Azimio la Arusha na kupitisha kinyemela lile za Zanzibar.
 
Wapo wengi ila wale waadilifu hawapewi dhamana mkuu hilo ndilo tatizo sugu kwa magamba wezi na mafisadi ndio mashujaa wao tu
 
Dr Kingwangara namkubali sana anaakili nzuri kuliko hata Maselle na Mwigulu huyu jamaa akiongea unajua kabisa yupo sehemu asiyostahili maana juzi aliongelea swala la IPTL wendawazimu wa ccm wakambezaa na kunanga.. Karibu Upinzani Dr

Nimesikia Kigwangala naye ameanza kuzunguka kutafuta kuungwa mkono na wajumbe ndani ya Chama chake akifikiria kuwania Urais 2015...kazi ipo kwa wagombea vijana walioanza kujiamini kuwa wako peke yao, maana walau huyu ana nafuu kubwa sana humo ndani ya CCM
 
Wapo wengi ila wale waadilifu hawapewi dhamana mkuu hilo ndilo tatizo sugu kwa magamba wezi na mafisadi ndio mashujaa wao tu

Ni kweli. wanapeana Uwaziri na dhamana nyingine ndani ya CCM na taasisi mbalimbali kwa kujuana na kusaidiana, lengo kuu likiwa kugawana ulaji ama kulipana fadhila badala ya track record ya mtu kudeliver ama uwezo wake katika kusimamia ukweli na kutetea watu...ama hata ubunifu na uwezo wa kuchambua
 
mkuu tatizo kubwa la ccm ni mfumo wake , ni chama ambacho hakina watu wenye malengo ya kuleta maendeleo, hakina ! Wazazi wanataka kuwarithisha nchi watoto wao , wameifanya nchi hii kama shamba lao ! Wanaaminishana hata kwenye vikao vyao kwamba wao wanastahili zaidi kuliko wengine , BILA KUMUNG'UNYA MANENO nadiriki kusema tena kwa ushahidi usio na SHAKA KWAMBA CCM HAKUNA ANAYEFAA .
 
Nimekuwa nikipitia mijadala mbali mbali kwenye jukwaa la siasa tatizo kubwa nililoliona watu wamekuwa na ushabiki mkubwa wa vyama vya siasa.

Kwa mtazamo wangu tuna haja ya kwenda mbali zaidi tukaacha ushabiki wa vyama tukawapima viongozi kwa ufanisi wao na sio kwa vyama vyao, ninaposema viongozi namaanisha kuanzia ngazi za chini mpaka ngazi za juu.

Naomba kuwasilisha tujadili bila ya ushabiki wa vyama karibuni.

Sent from my iPhone using JamiiForums mobile app
Tatizo lako unaona ushabiki tu; Huchunguzi kwa nini hata kiongozi mzuri ndani ya CCM anageuka fisadi!... Hivi walioibua Richmond kwa ujasiri si ni akina Mwakyembe na Sitta? Walioizika hoja hii bila watuhumiwa kuwajibishwa ni kina nani?
Sasa msafi unayemuona wewe ni nani?!
 
MUNGU AKUBARIKI sana .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom