Bujibuji mimi si msomi ila nina akili ambazo walioenda shule wengi hawana.
Kuna nadharia zangu mwenyewe naziamini kuliko za wana sayansi.
Naamini kwamba dunia siyo round kama mpira wa miguu ⚽ bali una umbo la mpira wa rugby.🏉
So jua linapochomoza hujikuta dunia kwenye ncha mchongoko. Hivyo halisi kali kwasababu mionzi yake inasafiri umbali mrefu zaidi hadi kufikia dunia.
Mchana dunia inakuwa imejizungusha hadi kwenye peak yake, ambapo ☀️ jua hufikia kwenye uso wa dunia ndani ya muda mfupi sana.
Jioni inakuwa kama ilivyokuwa asubuhi
1.So huko kwenye ncha mchongoko hakuna bara ?
2.Je,zile nchi za baridi kali, zipo upande upi wa huo mpira
3.Je,Jua ndiyo lazunguka ama dunia ?
4.Je,mwanga hata ukipiga kwenye mchongoko si bado limepiga kwenye dunia tu ,hiyo mda mrefu inakuwaje sasa.
5.Je,mwanga hutumia mda gani kufika duniani
6.Mbona hiyo shepu yako ya Rugby,haionekani kwenye Solar Eclipse
7.Kwenye Ramani ya dunia, huo mchongoko upo upande gani...?
8.Je,kwa nadharia yako kila ncha ya dunia inapata mwanga wa dunia kwa Idadi sawa ya siku
9.Je,kwenye kwenye miezi ambayo jua uwahi kuchomoza na kuchelewa kuzama, mzunguko wake ukoje...
10.Je.Katika solar system, sayari zote ni za mviringo ila dunia tu ndiyo umbo la rugby ?
11.Una ushahidi hata mitano ya ku-support nadharia hii...
12.Kwa nchi za Scandinavia,Kanada Kaskazini na Siberia, ambapo jua hujitokeza kipindi cha miezi sita tu kwa mwaka ,Kwenye huo mpira wako wa rugby ,hii imekaaje...?
13.Dira zote huelekea Kaskazini, Je ,kwenye rugby yako Kaskazini ni wapi...?
14.Halafu utujuze kwanini Genius kama wewe upo nchini na nchi haijui, itabidi tukujengee sanamu na kukupa ulinzi maalum....