Hivi ni kwa nini Karimjee pekee?

RugambwaYT

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2014
Posts
1,444
Reaction score
2,032
Nashindwa kuelewa kwa nini misiba "ya kitaifa" kama huu wa Mzee Mengi na ule wa Ndugu Ruge unapelekwa kwenye ukumbi mdogo kwama ule! Ni kweli una hadhi na heshima nchini lakini kwa upande wa ukubwa nafikiri hauyatendei haki matukio kama hayo.

Mzee Mengi ni mtu wa watu wote, wa hali ya juu na ya chini. Ilifaa apelekwe hata uwanja wa taifa ili watu wote wapate nafasi sawa ya kushiriki kikamilifu katika kumsindikiza kwenye safari yake mwisho, kuliko hapo Karimjee ambapo kama inavyoonekana ni padogo kwa kweli.
 
Mtu ashakufa mnaagaika kuaga aga!!! Haina maana wala faida yoyote kwa Mungu.
 
Mwanadamu ni Mavumbi hakika mavumbini atarudi.
Kuaga, kusafirisha, kuagwa na wengi au waxhache ni tamaduni na taratibu ambazo hazipaswi kutugombanisha
Nakubaliana na wewe. Ila kuna mambo ambayo yana haja kusemwa ili siku za usoni yasilete manung'uniko kwa watu. Mzee Mengi aliulizwa na mtangazaji wa Citizen TV kwamba kwa nini hapendi kujikweza bali anajiweka karibu na watu wa chini japo ana mali nyingi. Akasema akienda msibani huwa anaona watu wa chini ndio wanachimba kaburi, wanabeba mwili, wanalia kwa huzuni, ila watu wa juu wamekaa pembeni. Ndio maana nikasema ilifaa apelekwe kwa watu wa chini kama alivyowish.
 
nimekuelewa mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…