Hivi nani ni mshauri pale Azam Fc?

four eyes

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
904
1,398
Habari wadau wa jf,

Kwa muda sasa nimekuwa nikifuatilia mambo mbalimbali yanavyoenda ktk timu ya azam na najikuta na maswali kadhaa bila majibu

Azam ni timu ambayo ilipoanzishwa na kwa kuzingatia uwezo wa kipesa wa mmililiki niliona kabisa au nilitalajia ije iwe timu kubwa itakayokuwa ikinyang'anyana ubingwa na vilabu vya simba na yanga na pengine kuvizidi vilabu hivyo kwa mafanikio.

Nilidhani hivyo sababu kama nilivyoeleza hapo juu mmiliki ana uwezo wa kipesa lakini pia timu ni yake kwahyo hakuna zengwe la wanachama wala wazee wa club kwahyo anakuwa na fursa ya kufanya mambo kwa Uhuru.

Kinyume na matalajio yangu club hii imefeli Ku mature kama club na badala yake inafanya vitu visivyoeleweka na kufanya iwe ngumu kuelewa malengo yao ni nini.

Wakati azam ikiwa ktk kiwango kinacholeta matumaini ya ushindani ghafra iliamua kupunguza matumizi na kuachana na baadhi ya wachezaji wake wa kutumainiwa ambao wameenda kuinufaisha club nyingine kubwa,hapa nilijiuliza sana azam wanashauliwa na nani maana mpira wa sasa unahitaji pesa kupata mafanikio wao wanapunguza pesa mpaka wanaacha wachezaji wazuri wanaelekea wapi?

Msimu huu pia wameamua kuachana na chirwa mchezaji ambae ameonyesha uhai na kuwasaidia huku wakibakia na ngoma ambae ameonyesha kiwango kibovu kabisa,je mshauri wao ni nani au mwenye timu anaamua tu kulingana na alivyoamka?
 
Me naona wenye azam wenyew washakata tamaa, walifanya investments kubwa wakitegemea faida kubwa katika kipndi kifupi wakati haiko hivo kwenye soka inshort inaonakena walitegemea faida tupu na sio hasara.
 
Dah,ndio maana nauliza mshauri wao nani ina maana kwa uzoefu wao mkubwa wa kibiashara wameshindwa kuwa na mshauri atakayewapa ushauri nzuri kuhusu mpira na uendeshaji wake na kama wanatalajia faida wataipata VP na kwa matalajio ya baada ya muda gani?naona wanayumba sana kama hawana dira hivi na mipango
 
Wamejitahidi kwa kiasi chake tusiwalaumu
Kuendesha timu bongo ni gharama sana
Tatzo ni pale ambapo wanafanya maamuzi ya ajabu ambayo yanawarudisha nyuma na matokeo hata kile kidogo ambacho wangeweza kukipata hawakipati,na sidhani kama azam ana shida ya pesa nadhani tatzo ni ukosefu wa mshauri mzuri tu
 
Umejuaje kama hawana shida ya pesa? We unafikiri pesa ni kumwaga tu?

Ile ni group of companies kama unaelewa hapo utajiongeza

Mh kwakweli ulivyosema group of companies sijajua bado unamaanisha nn kwa kuhusisha hilo ktk hii mada,nachojua ni kwamba wamiliki ni wazoefu wa biashara na Nina imani hawakuingia kichwakichwa ktk soka walijua gharama za soka la kisasa na how much unatakiwa uinvest na sote tunajua bakhressa ana successful group of companies so bado sijapata mantiki yako,na uthibitisho wa kwamba hana tatzo kipesa ni aina ya investments alizofanya kwa timu,kujenga uwanja sio mchezo aisee
 
Kama hujui group of companies sishangai ndio maana unawalalamikia azam fc

Kwa ufupi tu azam fc inaendeshwa kawaida tu inalipa mishahara ya kawaida sana

Bajeti ya sio kubwa kwasababu vyanzo vya mapato vya timu haziusiani na hela za wawekazaji ndani ya azam group of companies

Huwezi ukachukua pesa ya azam juice ukapeleka kulipa wachezaji mishahara ahaha

Wale ni watu wanaojua biashara ukiona azam haisongi mbele kwa haraka km unavyotaka wewe ujue biashara ya mpira bongo ukitoa Simba na yanga ni ngumu sana
Ndio maana wawekezaji wanaruruana kukimbilia Simba na yanga tu hizo timu zingine wachezaji wanalipwa mshahara mpaka laki mbili kwa mwezi
Mh kwakweli ulivyosema group of companies sijajua bado unamaanisha nn kwa kuhusisha hilo ktk hii mada,nachojua ni kwamba wamiliki ni wazoefu wa biashara na Nina imani hawakuingia kichwakichwa ktk soka walijua gharama za soka la kisasa na how much unatakiwa uinvest na sote tunajua bakhressa ana successful group of companies so bado sijapata mantiki yako,na uthibitisho wa kwamba hana tatzo kipesa ni aina ya investments alizofanya kwa timu,kujenga uwanja sio mchezo aisee
 
TPL U20

AZAM FC 3
YANGA 0

MTIBWA 3
SIMBA 1

FAINALI
AZAM FC v MTIBWA SUGAR

MTIBWA anacheza Fainali mwaka wa 3 mfululizo!
 
Back
Top Bottom