Hivi mwanamke aliyewahi kukulaza lock up anafaa kurudiana nae?

kyagata

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
8,975
16,988
Kuna binti alikuwa mpenzi wangu, huyu bint baba yake ni kamishna katika jeshi la police, Sasa kuna kipindi tulikorofishana nikamnasa makofi na hata hayakua makofi ya nguvu nilimgusa gusa tu,

Binti akapiga simu kwa baba yake kuwa kuna mtu kamfanyia fujo, ebana simu ikapigwa kutoka makao makuu ya police kuja arusha, ndio nikaona matumizi mabaya ya jeshi la police, yani difenda iliyojaa FFU ikaja kunikamata mimi utadhani jambazi sugu na wkt hata wangenipigia kuniambia nijisalimishe mwenyewe ningeweza kufanya hivo.

Nilikaa lock up week mbili bila dhamana wala kupelekwa mahakamani. Nashukuru Mungu kuna mzee tunafahamiana akafight mpaka nikaachiwa. Sasa yapata miaka mitatu toka tukio lile litokee,yule binti ameanza kunisumbua kuniomba turudiane.

Je mtu wa aina hii anafaa kumrudia wakuu, maana nikikumbuka ile kukaa lock week mbili napata hasira sana.
 
kuna binti alikua mpenzi wangu,huyu bint baba yake ni kamishna ktk jeshi la police,sasa kuna kipindi tulikorofishana nikamnasa makofi na hata hayakua makofi ya nguvu nilimgusa gusa tu,binti akapiga simu kwa baba yake kuwa kuna mtu kamfanyia fujo,ebana simu ikapigwa kutoka makao makuu ya police kuja arusha,ndio nikaona matumizi mabaya ya jeshi la police,yani difenda iliyojaa ffu ikaja kunikamata mimi utadhani jambazi sugu na wkt hata wangenipigia kuniambia nijisalimishe mwenyewe ningeweza kufanya hivo.nilikaa lock up week mbili bila dhamana wala kupelekwa mahakamani.nashukuru mungu kuna mzee tunafahamiana akafight mpaka nikaachiwa.sasa yapata miaka mitatu toka tukio lile litokee,yule binti ameanza kunisumbua kuniomba turudiane.
je mtu wa aina hii anafaa kumrudia wakuu,maana nikikumbuka ile kukaa lock week mbili napata hasira sana.


Huyo ana hamu ya kukupeleka tena rumande kwani anahisi una furaha baada ya kuchiwa huru. Inaonekana huyo demu ni hatari sana.
 
Uliishi mara ya kwanza ukamgusa kofi lock up two weeks! Saiv anajua umenyooka mkirudiana utakuwa unamuogopa kwa kila jambo hivyo atakuwa amekunyoosha kisaikolojia unaweza mkuta anagegedwa na usimwambie kitu koz lock up itakuhusu! Wazaz wanaoingiliaga mapenz ya vijana huwaona kama dishi zao zinayumba, acha aolewe na huyo baba yake
 
Rudiana naye tu sahau ya lock up kama yeye alivyosahau makofi

Nakushauri rudiana nae... kama vile wewe ulivyopata hasira ukampiga (sio sawa kumpiga mtu yoyote), ndivyo na yeye alivyopata hasira kukushtaki kwa baba yake. Hiyo ya kukaa ndani nina uhakika yeye hakutaka ukae ndani wiki mbili, sema amri ya baba mjeshi ndio ilisumbua. Inaonekana huyu mwanamke anakupenda na wewe pia unampenda, rudianeni ila sasa muwe kama watu wazima, hasira za kijinga jinga acheni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom