Hivi Mawakala wa Vyama vya Siasa wanaofanya fujo vituoni wanajua wajibu wao?

Kinjekitile junior

JF-Expert Member
Apr 20, 2015
4,404
581
Mimi kwa uelewa wangu Wakala wa Chama cha Siasa kwenye Uchaguzi ni mtu anayeteuliwa na chama chake na kuwasilisha jina lake Tume kwa ajili ya kusimamia maslahi ya chama chake na mgombea wake wakati wa kupiga Kura, kuhesabu Kura na Kujumlisha. Wakala anayeteuliwa kwa kazi hii anakula kiapo cha kutekeleza majukumu yake chini ya Msimamizi au Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi.

Wakala ni mtu muhimu sana wakati wa Uchaguzi, Mgombea anapoteua Wakala atakayesimamia maslahi yake anakua amejiridhisha kabisa kuwa ameteua mtu makini mwenye Sifa zote zikiwemo za za Uteuzi kutoka kwenye Chama chake na kuwa na Kibali cha uteuzi, amekula kiapo cha kutunza Siri, Umri pia ni muhimu awe na miaka 18 na kuendelea pia Awe na Akili Timamu.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 57 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 ikisomwa na Kifungu cha 58 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, kwa pamoja na kanuni ya 48 ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2015 na kanuni ya 42 ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani) za mwaka 2015 kila Chama cha Siasa chenye mgombea wa nafasi yoyote kinaweza kuteua Wakala wake kwa kila kituo cha kupigia Kura.

Inashauriwa wakala awe ni mkazi wa eneo la kituo anachokisimamia hii inamsaidia wakala kushiriki pia katika Uchaguzi wa ngazi zote tatu za udiwani, ubunge na kiti cha Rais.

MAJUKUMU YA WAKALA, Wakala ana jukumu la Kutambua Wapiga Kura ndio maana anatakiwa awe mkazi wa eneo analolisimamia, Wakala anamwalikisha na kulinda maslahi ya mgombea au wagombea katika kituo na pia Wakala anashirikiana na Msimamizi wa Kituo na Msimamizi Msaidizi wa Kituo ili kuhakikisha sheria na taratibu zinazohusu upigaji Kura zinafuatwa katika Kituo.

Sote tunakubaliana kuwa Mawakala wa vyama Vya Siasa lazima wawe ni watu Makini na wenye akili Timamu wanaoweza kutekeleza kikamilifu jukumu Kuangalia mchakato mzima wa kpiga Kura, kuhesabu Kura, kujumlisha na kutangazwa matokeo ya Uchaguzi;

Wakala makini anatakiwa Kuwepo katika kituo wakati wa kufungua na kufunga kiyuo pia awepo muda wote wa upigaji wa kura na kuhesabu Kura.

Wakala anao wajibu wa Kuuliza au kutaka maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Kituo juu ya jambo linaloweza kutokea kituoni, katika hili anatakiwa azingatie sheria na kuepuka kutumia lugha za kuudhi, vurugu, nguvu au jambo lolote linaloweza kuzuia au kuvuruga utaratibu unaoendelea kituoni. Mawakala wengi wamekuwa wakichemka hapa wamekuwa wakifanya vurugu vituoni na matokeo yao ni kutolewa nje na kuishia kulalamika. Mwanzo nimesema mgombea au chama kinatakiwa kilete Mawakala makini wenye uwezo wa kuhakikisha maslahi ya vyama vyao yanalindwa na kusimamiwa kwa mujibu wa Sheria.

Wakala au Mgombea Kuridhika au kutoridhika katika Kituo cha kupigia kura.
Ukisoma Kanuni ya 59 ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2015 na kanuni ya 53 ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani) za mwaka 2015, Wakala au Mgombea atajaza fomu zifuatazo:

Fomu Na. 14 : hii ni Fomu ya Malalamiko au Ridhaa ya Wakala wa Upigaji Kura. Fomu hii hujazwa na Wakala kabla ya kuanza na baada ya kukamilika upigaji kura kuonyesha kuridhika au kutokuridhika na mwenendo wa upigaji kura.

Fomu Na 16: Hii ni fomu ya Malalamiko au Ridhaa ya Mgombea au Wakala. Fomu hii hujazwa na wakala katika hatua za uhesabuji wa kura kuonyesha kuridhika au kutoridhika na utaratibu wa kuhesabu Kura.

Hizi Fomu ni muhimu sana zijazwe, Mawakala wengi wanakimbilia kulalamika kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii hawajazi hizi fomu, kwa hiyo hoja zao zinakosa nguvu kisheria na hata wakienda mahakamani wanapoulizwa kama wamejaza hizo fomu au wakiombwa copy ya hizo fomu wanaishia kutoa macho.

Chonde chonde Vyama vya Siasa na Wagombea chagueni Mawakala wenye uwezo wa kutetea Maslahi yenu kwa mujibu wa Sheria na sio kupigana vituoni.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Ungeanza kwanza kuwaelimisha wagombea wa Chama Chako Cha Majangili kuhusu hilo.
 
Hahahahhahahahahah pole kisu kimemkata mnoaji??Waleta fujo ndiyo niliyokutajia.Ukiwaeleimisha kuhusu hilo nitakushukuru.

Hakuna Kisu hapo na wala sioni hoja yako! kama haujaelewa uzi omba msaada!Pia jibu swali nililokuuliza Ulishawahi kuwa Wakala kwenye Chama chako?
 
Hakuna Kisu hapo na wala sioni hoja yako! kama haujaelewa uzi omba msaada!Pia jibu swali nililokuuliza Ulishawahi kuwa Wakala kwenye Chama chako?

Kwani kuna tuta hapo??Nimekujibu kulingana na inavyotakiwa kuwa.Nenda kwanza kaelimisha Chama Chako Cha Mafisi/Mashetani inclusive Polisi maana nalo ni tawi la CCM kisha uje upande wa vyama vingine.Bila hivyo hoja yako haina mashiko.

Wenye vurugu ni wagombea na wanachama wa Chama Cha Mazingaombwe ambapo wanategemea jeshi la polisi na tume ya uchaguzi
 
Duuh ama kweli kazi ipo, kwani mleta mada ametaja chama? mbona hoja zake ni makini na hazina mlengo wa chama chochote?au hicho the so called chama cha majangili hakina mawakala?

Nimemjibu kulingana na uhalisia wa issue na sijakurupuka.99% ya Kampeni na nyakati za UCHAGUZI CCM ndiyo vinara wa matusi na kutumia nguvu kubwa ya polisi na wanachama wa CCM kudhuru upinzani bila Polisi kuingilia wala kushughulikia.Tumeona Alphonce Mawazo ameuawa na Vijana wa CCM(UVCCM),tumeona kijana wa Chadema amepigwa risasi na tumeona mawakala wakifukuzwa kwenye vyumba vya kupigia kura waasisi wakiwa CCM na idara zake wakisaidiwa na polisi.

Na hawa wote wanaofanya vituko vya mauaji wanajulikana,je Polisi wamechukua hatua gani??Je Polisi wako fair kwenye hilo??

Ndiyo sababu kubwa nimemweleza ni bora aanze kukielimisha chama chake na wanachama wake sheria na mikataba wanayosaini ni lazima ifuate siyo hiari,ni lazima.

Nimejibu hoja kulingana na hali halisi ya kisiasa,wanachama wa CCM against wanachama wa upinzani.
 
Kwani kuna tuta hapo??Nimekujibu kulingana na inavyotakiwa kuwa.Nenda kwanza kaelimisha Chama Chako Cha Mafisi/Mashetani inclusive Polisi maana nalo ni tawi la CCM kisha uje upande wa vyama vingine.Bila hivyo hoja yako haina mashiko .

Naona unavibrate tu hadi unapoteza mwelekeo kwa kutanguliza mihemko mbele! Soma vizuri uzi acha kutokwa na maneno yasiyofaa
 
Back
Top Bottom