Kuna kawaida ya watanzania kuposti picha za walemavu kwenye mitandao na kukomenti Amin, Mungu amsaidie, Mapenzi ya bwana yatimizwe na vitu vya aina hiyo.
Sasa najiuliza kutimizwa kwa haya mapenzi ya bwana ni kwa kuteseka walemavu wa Tanzania tu? Mbona kwa wenzetu walemavu wote wana misaada mpaka utafikiri hawapo.
Watu elfu saba badala ya kukomenti Amin wakichanga elfu na mia tano kila mmoja zitapatikana shilingi milioni kumi na laki tano. Pesa ya kutosha kumnunulia mlemavu wheelchair na kumfungulia mfuko wa elimu mpaka chuo kikuu.
Na tunashindwaje kuanzisha shule za walemavu kwa michango ya wananchi? Kwa wenzetu kodi zinatumika kusaidia walemavu sisi tunaweza kujipanga wenyewe kibongo bongo angalau kila mkoa ukawa na vituo/shule moja ya walemavu. Wakuu wa mikoa changamoto hiyo