HorsePower
JF-Expert Member
- Aug 22, 2008
- 3,612
- 2,569
Jamani, kisa hiki nimekisikia around saa sita/saba kwenye radio Clouds, kwenye kipindi fulani na kiko hivi ....
Kuna jamaa ana mke na anaishi nyumba ya kupanga mahali fulani. Kumbe ktk nyumba hiyo hiyo kuna mpangaji mmoja wa kike ambaye jamaa kamgeuza ndo nyumba ndogo. So inasemakana kuwa jamaa alikuwa anatoroka mara kwa mara na kwenda kukutana na mpenziwe bafuni bila mkewe kujuwa.
Za mwizi arobaini, siku kadhaa zilizopita, jamaa aliaga usiku kuwa anaingia bafuni alipofika huko alikaa kwa muda kidogo ikabidi mkewe atoke kufuatilia. Alipotoka alimuona mumewe anatoka huko bafuni, na kabla hata hawajaingia ndani, yule mpangaji wa kike mwingine naye akatoka bafuni, ndipo mkewe akagundua kuwa kumbe alikuwa anaibiwa na jirani yake.
Sasa najiuliza, hivi mapenzi ni uchizi? Hivi mtu anawezaje kumtoroka usiku mkewe na kwenda kwa jirani kwa nini asimalizie mambo yake kwa mkewe? Maana naona vituko vya haya mambo vimezidi! Wenzangu mna comments gani juu ya hili tukio? :nerd:
Wenu,
HorsePower
Unashangaa dhambi hiyo tu! Kuna binadam wanatenda dhambi za ajabu mpaka yule Lucifer anashangaa anabaki kupena tano na mapepo wenza utaskia,"hebu cheki dhambi,duh! Huyu jamaa noma mi mwenyewe siwezi,hebu kula
tano pepo mwenzangu!"
Unashangaa dhambi hiyo tu! Kuna binadam wanatenda dhambi za ajabu mpaka yule Lucifer anashangaa anabaki kupena tano na mapepo wenza utaskia,"hebu cheki dhambi,duh! Huyu jamaa noma mi mwenyewe siwezi,hebu kula tano pepo mwenzangu!"
hahahahaUnashangaa dhambi hiyo tu! Kuna binadam wanatenda dhambi za ajabu mpaka yule Lucifer anashangaa anabaki kupena tano na mapepo wenza utaskia,"hebu cheki dhambi,duh! Huyu jamaa noma mi mwenyewe siwezi,hebu kula tano pepo mwenzangu!"
mbona kawaida sana, kuna jamaa ameoa alikua anamchukua msichana wa jiran ikifika usiku yule msichana anapiga mawe juu ya bati kama ishara ya kumuita jamaa.Jamaa taratibu anaamka na kuijfanya anaenda kuangalia mazingira huku akifoka mbele ya mkewe hawa vibaka wamezidi leo naenda kuwamaliza......................kumbe anaenda kujilia mzigo taratibu