Hivi mama yake Diamond anajua kiingereza?

Wabongo wengi tunaongea kingereza cha kuelewana wenyewe na tunakuwa tunajiamini sana na kutulia tukikimwaga cha malkia ila akija mwenye lugha yake sijui huwa kinapeperukia wapi ? mtu jasho linamtoka penye usaili huku kung-fu si kung-fu choir master si choir master basi tafrani mtu alitoka penye interview hoi kuliko wale makuli wanaotoa lumbesa ya nazi kutoka soko dogo la nazi kupeleka kisutu .
 
Huyu mwenzetu atakuwa anajua nchi zote za Uzunguni wanazungumza kiingereza.Uzunguni kuna lugha zingine kama kireno,kijeruman,...

Kujuwa "kizungu" ndiyo nini?

Kwa Tanzania ukisema kizungu Maana yake ni kiingereza. Japo sio msamiati rasmi, lakini imezoeleka na imepokelewa hivyo kwa miaka mingi. Nyinyi wasomi mtataka kubisha hili, lakini kwa watanzania wengi huo ndio ukweli.

Swala la kusema kwamba wazungu wanaongea lugha tofauti hapa halina nafasi. Tukisema anaongea kizungu tunamaanisha kiingereza kwasababu hata hao wareno, wajerumani, wadachi, wafaransa nk. Wakija Tanzania lugha zao wataziacha huko kwao na kutumia kiingereza tu. Na hapo ndio tunaposema kiingereza ndio kizungu
 
Back
Top Bottom