Hivi Magufuli atakuwa mtu maarufu CCM baada ya Nyerere?

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,342
9,824
Hakuna majina makubwa tena CCM kwa sasa!
Yako wapi?
Ukiacha waganga njaa
Wako wapi wanazi wa CCM, wabadilishaji wa upepo wa siasa, wauzaji wa nembo, wavutaji wa halaiki ya watu, watu maarufu CCM wako wapi??

Hakuna aliyeonekana kwenye uchaguzi ulioisha, uchaguzi wa rais wa mioyo ya watu; Ndg; Edward Ngoyai Lowassa.

Ila ni rahisi kueleza hili kwa kuangalia matatizo yanayomshinda Magufuli;
#Bomoa bomoa
#Utawala usiofuata sheria
#Mkwamo wa kisiasa Zanzibar
#Uhusiano mbovu na masikini na matajiri

Tatizo la CCM nikuwa chama cha siasa bila ya wanasiasa

Kuondoka kwa Lowassa kulipigia mstari kifo cha wanasiasa ndani ya CCM.
Kumebaki matone ya matumaini (Lugola), matapeli (Mhongo, kijiko cha uaminifu (Magufuli), watu wabovu (Nape) na vichekesho vya wanasiasa (Kikwete).

Ila kinachokosekana ni mtu maarufu, mwanasiasa, kipenzi cha watu.
Mtu anayeleta furaha kwenye mioyo ya watu; mtu ambaye watu wanamwangalia kwa matumaini kipindi cha matatizo.
Hayo yote yaliondoka wakati Lowassa alipoondoka CCM, alipojiunga na chama cha watu, chama cha kisasa, chama cha vijana ~ CHADEMA.

Magufuli alitegemewa kuijaza hii nafasi.Ilisemekana alikiwa na kila sifa, jicho la utendaji na uwezo wa kuivuta mioyo ya watu.

CCM waliamini hivyo na wamiliki wa CCM wakamwona kama mtu anayeweza kuirudisha CCM sokoni.Wamemsaidia, wameelewa matatizo yake na wamekuwa wavumilivu maana hawakuwa na mbadala.
Uvumilivu wao haujazaa matunda na labda hautakaa uzae.

Je, ni wakati wa kumnyima rais uongozi wa chama?
Yetu macho!!!!
 
kamanda una chuki binafsi au umetumwa na mafisadi kuwasemea. huelewi unayoyasema unahitaji shule ya maana.
nadhani wewe ndio wale tulioitwa wapumbaf na malofa. kumbe wengi mpo. usicheze na maamuzi ya watanzania kama una ajenda yako ya siri pita nayo mbali kuleee.
hata Chadema asilia tulishatoa tamko la kumuunga mkono rais Magufuli. jana Sumaye kwa mdomo wake kamkubali Magufuli. Lowasa alishamtambua. wewe ni nani wa kuzungumza hayo
 
Chadema asilia ndio kiduku gani tena?
Acha hasira
Hili ni jukwaa la siasa.
 
amefanya nini cha maana mpaka awe maarufu
Vijana wanasema amekuja kama harufu ya pafyum, kabla hatujatuliwa akawa mrefu kama mkuyu, tulipomgundua akapotea kama zilipendwa.
Mwanasiasa wa uongo
Mtu wa matukio.
 
Chadema as! ia ndio kiduku gani tena?
Acha hasira
Hili ni jukwaa la siasa.
hakuna hasira kamanda. ndio maisha sasa ya Hapa ni kazi tuu ! unadhani angekuwa Lowasa haya mambo aliyoyafanya Magufuli angeyafanya? ? kwa sababu mafisadi wote ni rafiki zake na wamemchangia mapesa lukuki ya kampeni. angewezaje? ?? acha unafiki! kama umelipwa sawa ongea maana unatumikia pesa! kama alivyotumukia pesa Mbowe kwa kuuza utu wake kwa kusababisha Dr Slaa na Lipumba wajiengue. huu ni ufisadi mbaya kuliko fisadi zote zilizowahi tokea! malipo ni hapa hapa duniani!
Chadema asilia ndio wale wote waliokuwa nyuma ya Dr Slaa, chadema iliyokuwa imebeba ajenda ya ufisadi kwa nguvu zote, tofauti na hii chadema ya dot komu ambayo ilizika ajenda ya ufisadi kwa kupokea mafisadi waliokuwa wametemwa na ccm. pyuuuuuuf.....
 
hakuna hasira kamanda. ndio maisha sasa ya Hapa ni kazi tuu ! unadhani angekuwa Lowasa haya mambo aliyoyafanya Magufuli angeyafanya? ? kwa sababu mafisadi wote ni rafiki zake na wamemchangia mapesa lukuki ya kampeni. angewezaje? ?? acha unafiki! kama umelipwa sawa ongea maana unatumikia pesa! kama alivyotumukia pesa Mbowe kwa kuuza utu
wake kwa kusababisha Dr Slaa na Lipumba wajiengue. huu ni ufisadi mbaya kuliko fisadi zote zilizowahi tokea! malipo ni hapa hapa duniani!
Chadema asilia ndio wale wote waliokuwa nyuma ya Dr Slaa, chadema iliyokuwa imebeba ajenda ya ufisadi kwa nguvu zote, tofauti na hii chadema ya dot komu ambayo ilizika ajenda ya ufisadi kwa kupokea mafisadi waliokuwa wametemwa na ccm. pyuuuuuuf.....
Mimi nilimwamini Slaa ila sikuwahi kudhani kama anaweza kuwa Rais.Ni mtu
mwenye historia yenye utata.

Back to bar..
Pombe hawezi kujenga nchi ya viwanda bila matajiri, na biashara na siasa ni vitu viwili tofauti.
Magufuli ni mfugaji wa ng'ombe tena wachache wanaofugwa kiutamaduni na sio kibiashara.
Mtu asiye na sera ya nje wala ya ndani.
Mtu mwenye sera moja tu ya majipu.
Inaonekana yamemsumbua sana wakati wa kukua kwake au labda hata sasa.
 
Mleta mada ameandika utafikiri leo umebakia mwezi mmoja tu uchaguzi wa mwaka 2020 ufanyike. Endelea hivyo hivyo kuishi kama fisi anayesubiri mkono uanguke.
 
Fisi anayesubiri mkono kuanguka ni yule mtu anayesubiri makosa yafanyike ili aweze kupata cha kuongea au wakati mwingine kukosoa. Mtu atafutaye cha kuongea kutokana na makosa fulani ya watu.
Jibu swali bwana Philipo. Acha kurukaruka!
 
Kama unajibiwa halafu huelewi unataka usaidiwe vipi, hizi ni lugha ambazo kwa akili ya kawaida unatakiwa uwe mjanja kuweza kuzielewa. Naona unataka kuleta mada nyingine ambayo ni nje kabisa na mada ya mtoa hoja. Mimi nimemkumbusha mleta mada kwamba ni mapema sana kusema kuwa Magufuli hajafanya kitu, sasa wewe naona unapoteza muda kuleta maongezi yasiyo na tija kwako wewe na kwangu pia
 
Attention to details Mr.Philipo!!
 
Attention to details Mr.Philipo!!
Kaka nimeielwa vizuri sana mada ndio maana nikasema ni mapema mno kwa magufuli kupimwa kwa kazi ya miezi miwili, hiyo bomoa bomoa na mengi yaliyoandikwa huwezi ikapima impact yake kwa muda huu, yapo mengi sana na yamekaa kisera zaidi sio rahisi kuyapima kwa miezi miwili, na nikafikia maamuzi ya kusema hivi sasa sio mwezi mmoja kabla ya uchaguzi wa 2020. ndio nikaongelea habari ya fisi na mkono unaoonekana kukatika. Bado sana muda wa kuleta mada kama hii, kuna mengi sana yanayoambatana na utekelezaji wa sera, hayapimwi ndani ya miezi miwili baada ya CCM kushinda nafasi ya Urais. Watanzania tunakuwa mafundi wa kuongelea hatima ya kitu wakati kwa sasa kipo kwenye stages za kuanzishwa. Nimeielewa mada mkuu, tusipoteze muda kwenye issue hii moja tu.
 
Hivi Magufuli anaweza kweli kumudu nafasi ya mwenyekiti wa CCM?
 
kamanda una chuki binafsi au umetumwa na mafisadi kuwasemea. huelewi unayoyasema unahitaji shule ya maana.
nadhani wewe ndio wale tulioitwa wapumbaf na malofa. kumbe wengi mpo. usicheze na maamuzi ya watanzania kama una ajenda yako ya siri pita nayo mbali kuleee.
hata Chadema asilia tulishatoa tamko la kumuunga mkono rais Magufuli. jana Sumaye kwa mdomo wake kamkubali Magufuli. Lowasa alishamtambua. wewe ni nani wa kuzungumza hayo
anamatatizo kwenye ubongo wake mtoa mada.
anaambiwa CCM inawenyewe pamoja na wale na wewe mtoa mada
 
CCM kimebaki kuwa chama cha kutumia nguvu na kubebwa na vyombo vya ulinzi.
Inajivunia uoga wa watanzania na hizo sio siasa.
 
Mleta mada ameandika utafikiri leo umebakia mwezi mmoja tu uchaguzi wa mwaka 2020 ufanyike. Endelea hivyo hivyo kuishi kama fisi anayesubiri mkono uanguke.
Huyu dogo anahitaji msaada maana ana dalili zote za kuumwa. Bado haamini kuwa Watu hawakumtaka Lowassa na sasa Rais ni Magufuli. Ni aina fulani ya watoto waliokuwa wakitarajia kunufaika na swala la Lowassa kuwa Rais, sasa wanashindwa kucope na uhalisia.
Wa kulaumiwa ni huyo babu yao maana aliahidi mengi sana kwa kutafuta umaarufu ikiwemo vyeo.
 
Back
Top Bottom