Rais Magufuli awatunuku vyeti wajumbe wa kamati za Makinikia; akanusha taarifa za mapato ya Serikali kupungua

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Oktoba, 2017 atawatunuku vyeti wajumbe wa kamati zilizofanya uchunguzi wa kiwango, aina na thamani ya madini katika makinikia na baadaye kufanya mazungumzo na kampuni ya Banick Gold.

Tanzania na Barrick Gold Corporation zilifikia makubaliano tarehe 19 Oktoba, 2017 na kutiliana saini mkataba wa kutekeleza mwelekeo mpya wa namna kampuni hiyo itakavyoendesha biashara ya madini ya dhahabu yanayochimbwa katika migodi yake hapa nchini, pamoja na kulipa takribani Dola za Marekani milion 300 za kuonesha nia njema ya kufidia madai ya upotevu wa mapato yaliyotokana na biashara hiyo.

Tukio hili litafanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 5:00 asubuhi na kurushwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya redio, televisheni na mitandao mbalimbali.

Mkungenzi wa Mawasiliano ya Rais,
IKULU Dar es Salaam
23 Oktoba, 2017

IMG_20171023_093022.jpg


UPDATES:




Cheti cha kwanza kimeenda kwa Spika wa bunge Mhe. Job Ndugai, kimepokelewa na Mke wake Bi. Fatma Ndugai

Kamati ya Makinikia ndio inapokea vyeti kwa sasa;
Prof. Mruma, Prof. Paramagamba, Ndugu Lusajo Kasubisye, Ndugu Adejen Mwaipopo, Ndugu Teddy Sikulwasha, Ndugu Moses Edward Moses ambaye ana huzuru na Cheti kinapokelewa na Paramagamba, Ndugu Andrew Mwangakala, Ndugu Michael Kambi, Ndugu Prof. Kiaruzi Rutastara, Dk othswadi, Ndugu Gabriel Malaki, Prof. Ruzaura Ikingura, Prof. Buchweshega, Dk Ngenya, Dk Ambrose Itika, Ndugu Mohammed Makongoro, Ndugu Eli Gombera

Sasa Prof. Paramagamba anatoa neno la shukrani kwa niaba ya kamati,
Tunatakiwa tuwe watu wa shukrani kwa Mungu wetu anayetulinda.

Kwa niaba ya kamati nasema asante sana

Namshukuru sana baba yangu ambaye kabla hajaenda mbinguni alinikabidhi kitabu cha sal akilichoaandikwa kwa lugha yake. Nayasema haya kwa sasababu Mungu hupanga mambo bila sisi kujua.

Nikishukuru Mhe. Rais maana tumetunzwa vizuri tumekunywa na kula vizuri, Napata wasiwasi tunapoenda huko ukituachia ila naamini utatuangalia angalia.

Tunashukuru wapishi, wahudumu na wafanya usafi wote na wasaidizi uliotupo.

Mafanikio tuliyoyapata ni makubwa sana, Wangazija wana msemo ukitaka kupima mafanikio ya mtu usiangalie urefu wa mtu bali kina alipotokea. Na nawaomba watanzania waangalie kina sio urefu

Na bila wewe kuthubutu Mh. Rais tusingefika hapa, ila umethubutu na tumetoka nje ya shimo

Mhe rais sikuhangaika sana na magazeti ya ndani ila magazeti ya nje, niliangalia gazeti la Zambia la Business Times na kukuta Bwana. Sinkala Charles ameandika kuhusu mafanikio yetu “That a good deal tell all African government who depend on tax”. Mwingine anasema huyu anaitwa Nyendwa “Now this is what I called good leadrership” mwingine anasema “big up Magufuli”

Quaran inasema kama huwezi kumshukuru binadamu mwenzako huwezi kumshukuru Mungu

Kwahiyo Mhe. Rais napokea maagizo yako utakayotupa na kufanyia kazi.

Sisi sote tunamshukuru Mungu, tunamshukuru Mhe. Rais kwa kuthubutu na pia nishukuru watu wote tuliofanya kazi kwa pamoja.

Magufuli anaanza kuongea sasa

Nami namshukuru sana mwenyezi Mungu kufika katika siku hii ambayo ni muhimu sana.

Swala hili mpaka lilipofikia leo shukrani za pekee zimuendee mwenyezi Mungu aliyetutangulia na wanatanzania wote.

Nimshukuru Mhe. Spika kwa kazi kubwa aliyofanya katika kutea kamati hizi, sikutaka kuwapa vyeti wote kwa sababu hizo zipo kwenye uwezo wa Spika sikutaka waanze kuongea tena.

Ni wakati muafaka wa kuletwa kwa hati dharura

Jeshi la polisi natambua kazi zenu japo sikutoa vyrti kwenu kwa usalama wa raia wote. Hata makinikia yaliyopo bandarini bado yapo mikononi mwenu mnayalinda

Kwa jambo kubwa kama hili wapo waliosema na nilitegemea yawepo ya kusemwa kwa sababu wapo waliolipwa kusema na washukuru watanzania pia kwa uvumilivu wao

Pia nawashukuru hawa niliwapa vyeti maana wali- sacrifice maisha yao. Kazi ya kumnyang’anya mtu mabilioni ya fedha ni kazi ngumu

Tulipoanza kazi hii tulijua tuna-deal na watu wa namna gani maana tulipata information zote walivyokuwa wanaiba jinsi walivyofungua maakaunti ya benki nje information zote

Kwa sababu ya evidence zote hata wangeenda mahakama gani sisi tungeshinda hata mahakama ya Malaika kwa sababu ushahidi tunao

Kwenye makubalinao yoyote lazima tukubaliane kwenye win win situation, kwaniaba ya watanzania siku na cha kuwapa ndio maana nikaona niwape vyeti maana mmefanya kwa niaba ya watanzania.

Katika mkataba huu sisi tuliamua kuzungumza na barrack maana wana asilimi 63.9 za umiliki wale wengine ambao hatuwajui hata hatujui wana umiliki wa asilimia ngapi. Na tuliambia tusizungumze na wapiga kelele

Idadi ya watanzania wataoajiliwa itakuwa kubwa, kodi zote zitalipwa.

Katika kuwa kwenye kama ka-partinership wakatoa bil 700 ambazo sisi hatukuwa navyo

Prof. Kabudi muanze kuangalia watu ambao wao kazi zao ni kubadili twakimu, kuna kifungu ambacho insema mtu akibadili twakimu za serikali anaweza kufungwa miaka miwili. Mtu anazungumza mapato yameshuka mtu kama huyu anatakiwa apelekwe mahakamani aka-justify

Katika hali ya kawaida tu kama mapato yanashuka unaweza kujenga reli ya standard gage ya kilometa karibu 700 kama mapato yameshuka wapi unapata hela? Pia kama serikali mapato yemeshuka unaweza kununu ndege mpya sita kwa mpigo? [Unadhani tulibadilishana kwa dagaa, au unadhani tulinunua kwa Migebuka]

Je unaweza kutangaza tenda ya mradi ambao uliachwa na baba wa taifa wa Stiegler’s gorge na ambao uta-cost trions of money na makampuni yaliyochukua tenda ni Zaidi ya 79. Kama huna pesa na makusanyo ni ya hovyo unapata wapi pesa za kungeza hela kwenye sekta ya afya to bil 31 mapka 200 na. Kama huna pesa unapata wapi pesa za kutangaza kununua meli katika ziwa Victoria

Kwa hiyo nitakachokusema watanzania muwapuuze watu wa namna hii wanataka tuzungumze mambo yao

Mtu anasimama macho amekodoa, mdomo unatoka mapovu anabeza jitihadi hizi, hata kama umetumiwa kwa kupewa hela si kula tu hela ukalale. Kwa sababu lengo lao ni nkuwagombanisha watanzania na serikali yao.

Siku zote nimekuwa nikisema nchi hii ni donor country tumekuwa tuki-donate bila kujua. Watu wanasema na kulia kuwa eti hawana mtaji kuzaliwa tu Tanzania ni mtaji wenyewe

Hivyo leo natoa tu shukurani kwa watanzania, viongozi wa dini na viongozi wote wa vyama vya siasa. Fedha zikipatikana nyingine hata ruzuku zenu zinaweza kuongezeka. Mtu anasimama anapinga tu kwa sababu yeye kapewa kazuruku kake ka mfukoni

Rais Magufuli amteua Prof. Luoga kuwa Gavana wa Benki Kuu;

Leo nimeamua kumteua Gavana katika hawa nilowapa vyeti leo. Nimemteua Prof. Luoga kuwa Gavana wa benki kuu mara baada ya gavana aliyepo kumkabidhi. Prof. Luoga ni Mtaalamu wa Taxation law

Sasa mkaendelee na kazi zetu kwa watu wa Almasi na Tanzanite na nimefurahi sana watu wa Tanzanite One wamesema wapo tayari kwa mazungumzo

Ndugu zangu niseme nawashukuru sana na kuwashukuru wote.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Oktoba, 2017 atawatunuku vyeti wajumbe wa kamati zilizofanya uchunguzi wa kiwango, aina na thamani ya madini katika makinikia na baadaye kufanya mazungumzo na kampuni ya Banick Gold.

Tanzania na Barrick Gold Corporation zilifikia makubaliano tarehe 19 Oktoba, 2017 na kutiliana saini mkataba wa kutekeleza mwelekeo mpya wa namna kampuni hiyo itakavyoendesha biashara ya madini ya dhahabu yanayochimbwa katika migodi yake hapa nchini, pamoja na kulipa takribani Dola za Marekani Bilioni 700 za kuonesha nia njema ya kufidia madai ya upotevu wa mapato yaliyotokana na biashara hiyo.

Tukio hili litafanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 5:00 asubuhi na kurushwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya redio, televisheni na mitandao mbalimbali.

Mkungenzi wa Mawasiliano ya Rais,
IKULU Dar es Salaam
23 Oktoba, 2017


Msigwa amerekebisha. Ni Shilingi Bilioni 700 sio Dola za Marekani Bilioni 700
 

Attachments

  • 20171023_082042.jpg
    20171023_082042.jpg
    78 KB · Views: 79
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Oktoba, 2017 atawatunuku vyeti wajumbe wa kamati zilizofanya uchunguzi wa kiwango, aina na thamani ya madini katika makinikia na baadaye kufanya mazungumzo na kampuni ya Banick Gold.

Tanzania na Barrick Gold Corporation zilifikia makubaliano tarehe 19 Oktoba, 2017 na kutiliana saini mkataba wa kutekeleza mwelekeo mpya wa namna kampuni hiyo itakavyoendesha biashara ya madini ya dhahabu yanayochimbwa katika migodi yake hapa nchini, pamoja na kulipa takribani Dola za Marekani Bilioni 700 za kuonesha nia njema ya kufidia madai ya upotevu wa mapato yaliyotokana na biashara hiyo.

Tukio hili litafanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 5:00 asubuhi na kurushwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya redio, televisheni na mitandao mbalimbali.

Mkungenzi wa Mawasiliano ya Rais,
IKULU Dar es Salaam
23 Oktoba, 2017


Zimefika Dola bil 700 tena? Kumbe matumaini ya Noah zetu bado yapo..
 
Back
Top Bottom