Hivi kweli wamarekani wanataka kumpa Trump Urais?

KiongoziMkuu

Member
Sep 16, 2015
34
7
Wadau, naamini wengi wetu tunafuatilia chaguzi za marekani sasa ikiwa katika kipindi cha kampeni. So far, Trump anaongoza akiiwaacha Ted Cruz, Hillary Clinton etc kwa asilimia kadhaa.

Sasa ninapochoka na kuishiwa nguvu ni pale ninapoona kuna idadi kubwa ya wamarekani katika majimbo tofauti wakionyesha kumkubali Donald Trump pamoja na sera zake za kurudisha ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa dini.

Sambamba na wamarekani, kuna hadi watanzania ambao nao wanamkubali sana Trump akiwemo director wa miss universe Tanzania - Maria Sarungi.

Sasa hii ni ishara gani?
Ninachokiona hapa ni kuwa watu wengi hufuata upepo. Dunia nzima sasa inapambana na kuondoa kama si kupunguza ubaguzi wa rangi ambao umepelekea vifo vya raia wengi wa nchi mbalimbali. Nchini marekani polisi wa kizungu alimpiga bastola kijana mdogo mweusi bila hatia ikawa shida marekani. Sasa leo hii watu wapo tayari kumpigia kura mtu ambaye sera zake ni kuondoa watu weusi marekani,
Na kuzuia waislamu kuingia marekani akiamini hivyo anarudisha sifa na hadhi ya marekani!!

Jamani tujitambue. Kitu unachoweza kukiona ni kidogo kinaweza kuwa na impact kubwa sana ambayo hukutarajia.
Nawasilisha.
 
Hii kitu ndicho kilichotaka kutokea katika uchaguzi wa Tanzania mwaka jana! Wengi walifuata upepo kwenye mafuriko kama hayo ya USA kwa Trump! CCM walichofanya ni kumkata EL na huko USA naona Republicans wanataka kumkata Trump!
 
Hivi kweli Tanzania inapinga ubaguzi wa rangi? Mbona wale walioandika mabanga ya Machotara mpaka Leo hawakuguswa wala hawajadiliwi?
Mimi nahisi linapokuja suala la Ubaguzi wa rangi , waafrika ni bora tukanyamaza tu. Waafrika ni wabaguzi kuliko hao wazungu, Nenda Marekani, Nenda Uingereza kuna Waafrika wengi tu lakini hawabugudhiwi kama sisi tunavyowabugudhi Watanzania wenzetuambao wao na mababu zao walizaliwa hapa sababu tu wanarangi nyengine kuliko sisi
 
Nina hakika exposure ndio inafanya mpaka unasema hayo yote. Nenda Spain, nenda German ukaone kuwa mtu mweusi huwezi hata kumuongelesha mtu mweupe. HAGEUKII. Tanzania katika ubaguzi bado sanaa.. Hatujafika level za kuuana ovyoo kila siku.
 
Wadau, naamini wengi wetu tunafuatilia chaguzi za marekani sasa ikiwa katika kipindi cha kampeni. So far, Trump anaongoza akiiwaacha Ted Cruz, Hillary Clinton etc kwa asilimia kadhaa.

Sasa ninapochoka na kuishiwa nguvu ni pale ninapoona kuna idaidi kubwa ya wamarekani katika majimbo tofauti wakionyesha kumkubali Donald Trump pamoja na sera zake za kurudisha ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa dini. Sambamba na wamarekani, kuna hadi watanzania ambao nao wanamkubali sana Trump akiwemo director wa miss universe Tanzania - Maria Sarungi.

Sasa hii ni ishara gani?
Ninachokiona hapa ni kuwa watu wengi hufuata upepo. Dunia nzima sasa inapambana na kuondoa kama si kupunguza ubaguzi wa rangi ambao umepelekea vifo vya raia wengi wa nchi mbalimbali. Nchini marekani polisi wa kizungu alimpiga bastola kijana mdogo mweusi bila hatia ikawa shida marekani. Sasa leo hii watu wapo tayari kumpigia kura mtu ambaye sera zake ni kuondoa watu weusi marekani,
Na kuzuia waislamu kuingia marekani akiamini hivyo anarudisha sifa na hadhi ya marekani!!

Jamani tujitambue. Kitu unachoweza kukiona ni kidogo kinaweza kuwa na impact kubwa sana ambayo hukutarajia.
Nawasilisha.
Uongo mtupu maria sarungi anamsapoti ben sandres yeye yupo democratic
 
Pilipili usizokula zakuwashiani? Nyinyi juzijuzi tu hapa si mlikuwa mnajidai hamna mpango na Marekani,kwamba wafanye yao na ninyi mfanye yenu?
Lini? Kivipi? Embu fafanua. Na unaposema pilipili nisizokula zaniwashia nini ebu fikiria kuwa wewe ni Muafrika au Mzungu na kisha tafakari sera za Trump kama zitakugusa au la!
 
Hii kitu ndicho kilichotaka kutokea katika uchaguzi wa Tanzania mwaka jana! Wengi walifuata upepo kwenye mafuriko kama hayo ya USA kwa Trump! CCM walichofanya ni kumkata EL na huko USA naona Republicans wanataka kumkata Trump!

Mafuriko ya Trump yako kama ya Lowasa kabla ya kwenda kukatwa Dodoma.Staili anazotumia Trump ndio zile zile alizotumia Lowasa na yeye na wapambe wake kama Lowasa wanatishia Chama cha Republican kuwa wasimpompitisha Trump chama kitasambaratika na yeye anasema wakimkata atahama chama!!! Sijui naye ataenda UKAWA kama Lowasa !!!!.

Na Trump kuna kikao kama kile cha Dodoma kinamsubiri Dodoma ya kule marekani ya chama chake cha Republican.Yaliyompata Lowasa ndiyo yatakayomkuta Trump.Watakata jina na mbwembwe zake zote zitaishia hapo.
 
Kwenye maelezo yako umechanganya trump na Clinton wakati hao kila mmoja ana chama chake, pili trump hana ubaguzi wa rangi isipokuwa hawataki waislamu wenye siasa kali na katika hayo wengi tunamuunga mkono nikiwemo mimi
Natambua ni watu wa chama tofauti. Niliwataja wote wanaowania urais na sio kumaanisha wapo chama kimoja.
 
Mafuriko ya Trump yako kama ya Lowasa kabla ya kwenda kukatwa Dodoma.Staili anazotumia Trump ndio zile zile alizotumia Lowasa na yeye na wapambe wake kama Lowasa wanatishia Chama cha Republican kuwa wasimpompitisha Trump chama kitasambaratika na yeye anasema wakimkata atahama chama!!! Sijui naye ataenda UKAWA kama Lowasa !!!!.

Na Trump kuna kikao kama kile cha Dodoma kinamsubiri Dodoma ya kule marekani ya chama chake cha Republican.Yaliyompata Lowasa ndiyo yatakayomkuta Trump.Watakata jina na mbwembwe zake zote zitaishia hapo.
Asante!
 
Kwani Maria Sarungi anapiga kura? Wanaharakati uchwara wanajifanya Wanaharakati na huku wako upande wa chama kimoja.
Hapigi kura lakini unaweza kuona naona awarenes ya watu ni ndogo! Kama mtanzania anafurahia siasa za mbaguzi wakati Tanzania ni nchi inayosifika kwa amani then ITS A BIG PROBLEM.
 
Back
Top Bottom